Achaniwa nguo na wapiga debe

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,268
33,040
MSICHANA mmoja jina lake halikuweza kupatikana maramoja alijikuta yupo kwenye wakati mgumu baada ya kuchaniwa nguo yake aliyovaa na wahuni na kumuacha na aibu kedekede na akiwa hana la kufanya kwa wakati huo. Tukio hilo la aibu lilitokea jana majira ya saa 2 usiku, maeneo ya Magomeni Kagera wakati msichana huyo akiwa kituoni hapo akisubiri usafiri.

Wahuni hao walianza kumshambulia kwea maneno dada huyo na msichana huyo kuwajibu jeuri na hivyo wahuni hao waliamua kumchania nguo yake ya isiyo na heshima aliyoivaa.

Msichana huyo alivaa nguo fupi kupita kiasi, alivaa blauzi tu na kuigeuza gauni hivyo kupelekea maungo yake ya mwili kuonekana ambapo wahuni hao waliamua kumfanyia uhuni kumchania ng uo hiyo ili atembee kama alivyozaliwa kabisa.

Wahuni hao walimshika dada huyo na kumchania gauni hilo na kupiga kelele na hakuna hata msamaria mwema mmoja aliyeweza kumsaidia wka wakati huo kwa kuwa hakuna mtu aliyependezwa na uvaaaji wake huo.

Wahuni hao ambao walikuwa zaidi ya wawili walishirikiana kwa pamoja kumshikisha adabu dada huyo na kumuacha akilia kituoni hapo na nguo yake kuichana.

“Tumeanza na wewe leo, na wengine watafuata tunataka mpate adabu si mteembee uchi tu” walisikika wakaka hao
 
kwa maadili nimeipenda!!imetulia,hata kama wanajiona wamependeza lazima wafikirie kuwa hawaishi wenyewe!!shime wahuni wachanieni zaidi hata kama ni wanangu!!
 
Ni halali yake kwa yaliyompata kama sketi ilikuwa fupi sana kiasi cha kukaribia chupi kuonekana
 
Hao mnaoita wahauni ni wazembe wa kupindukia na washamba sana sana,mtu yy anaruhusiwa kuvaaa atakavyo bora yeye mwenyewe ameridhika acheni mambo ya kijinga nyie wavuta unga halafu hamna hela.Badala ya kutetea maslahi ya wananchi kwa mfano kuandamana kudai mfumuko wa bei ya vyakula ushuke mmekalia kuangalia mademu za watu wamependeza mnawaonea kijicho kuweni wastaarabu nyambafu nyie hata hamjaenda shule inaelekea.Komaaeni na mafisadi waacheni mabinti wavae watakavyo bora wenyewe wameridhika na kumbukeni hawajavunja sheria za nchi kama MAFISADI wenu mnaowashabikia,Nikiambiwa nichague Mafisadi na Changudoa kura yangu itaenda kwa machangudoa kwa kuwa wao wanakula jasho lao na sio Mafisadi wenu waliojibandika ati wameshinda urais.amkeni nyie na nyie ati hiyo safi waliofanyiwa na kama angekuwa dadako
 
Ndugu yangu Mboko chonde chonde hapa sio ulaya,tuna mila na desturi zetu.Ulaya unaweza kutembea hata uchi kila m2 na time yake,sio hapa utakua unavunja mila na desturi.Imagine unatembea na mama yako mkawa mnaongozana na msichana kama huyo chupi nyuma iko nje,tunaona na vingine kwa chini inapendeza kweli.Acha bana wajirekebishe sio kuiga tu ulaya hapa bongo sio mila zetu hizo.I'm out
 
Na nyie Wanaume mnaotembea mmeweka Makalio nje iweje?

Mbona na hao hamshambulii???

p-low-slung.jpg

moz-screenshot-2.png
moz-screenshot-3.png
 
MSICHANA mmoja jina lake halikuweza kupatikana maramoja alijikuta yupo kwenye wakati mgumu baada ya kuchaniwa nguo yake aliyovaa na wahuni na kumuacha na aibu kedekede na akiwa hana la kufanya kwa wakati huo. Tukio hilo la aibu lilitokea jana majira ya saa 2 usiku, maeneo ya Magomeni Kagera wakati msichana huyo akiwa kituoni hapo akisubiri usafiri.

Wahuni hao walianza kumshambulia kwea maneno dada huyo na msichana huyo kuwajibu jeuri na hivyo wahuni hao waliamua kumchania nguo yake ya isiyo na heshima aliyoivaa.

Msichana huyo alivaa nguo fupi kupita kiasi, alivaa blauzi tu na kuigeuza gauni hivyo kupelekea maungo yake ya mwili kuonekana ambapo wahuni hao waliamua kumfanyia uhuni kumchania ng uo hiyo ili atembee kama alivyozaliwa kabisa.

Wahuni hao walimshika dada huyo na kumchania gauni hilo na kupiga kelele na hakuna hata msamaria mwema mmoja aliyeweza kumsaidia wka wakati huo kwa kuwa hakuna mtu aliyependezwa na uvaaaji wake huo.

Wahuni hao ambao walikuwa zaidi ya wawili walishirikiana kwa pamoja kumshikisha adabu dada huyo na kumuacha akilia kituoni hapo na nguo yake kuichana.

"Tumeanza na wewe leo, na wengine watafuata tunataka mpate adabu si mteembee uchi tu" walisikika wakaka hao[/QUOTE]

My take :Hii ni harassment ya hali ya juu sana! sasa hao kinawahusu nini?? ati tunataka mpate adabu! wao ni kama nani ktk maisha yake! haya mambo wa hawa wapumbavu wanaojichukulia sheria mikononi yanaturudisha nyuma sana! sisemi kwamba nnafagilia huyu dada kuvaa nguo fupi ila hii tabia yetu ya kibongo sijui kiafrica inatia kinyaaa wakati mwingine!mbona hawawavui suruali wanawake! maana hiyo sio mila na desturi yetu ati!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom