Elections 2010 Achangiwa fedha kumkatia rufaa Limbu

Ng'wanza Madaso

JF-Expert Member
Oct 21, 2008
2,268
333
Achangiwa fedha kumkatia rufaa Limbu

Na Cosmas Mlekani
16th November 2010

Baadhi ya wananchi wa wilaya ya Magu mkoani Mwanza, juzi walikatiza hotuba ya aliyekuwa mgombea Ubunge wa Chama cha UDP, Karuzwe Julius Ngongoseke, na kumchangia fedha kwa ajili ya kumkatia rufaa mgombea wa Chama cha Mapinduzi (CCM), aliyeshinda ubunge wa jimbo hilo, Dk. Festus Limbu.

Wananchi hao walichukua uamuzi baada ya Ngongoseke kuwaambia kuwa amefungua kesi Mahakama Kuu kupinga ushindi wa Limbu, ambaye ushindi wake unadaiwa ulipatikana baada ya kuchakachua matokeo ya jimbo hilo na kupeleka msimamizi wa jimbo hilo, Kolonel Ludungi, kutoweka.

Akizungumza na wananchi wa jimbo hilo, Ngongoseke alisema waondoe fikra kuwa yeye alinunuliwa na CCM na kusisitiza kuwa kama angekubali hongo hiyo basi angeikubali toka mchakato wa kuchukua na kurejesha fomu ulipoanza.

Alidai kuwa katika mchakao huo kuna mtu (jina tunalo), aliahidi kumpatia Sh. milioni 70 ili asirudishe fomu ila alizikataa kutokana na kuwaonea huruma wananchi wa jimbo hilo kutokana na jimbo hilo kuwa nyuma kwa maendeleo.

"Kwa taarifa yenu sasa hivi nimefungua kesi Mahakama Kuu kupinga matokeo ya uchaguzi ya jimbo hili yaliyotangazwa Novemba 2," alisema Ngongoseki.

Alisema kuwa amefungua kesi hiyo kwa gharama ya Sh. milioni 15 na kudai kuwa hiyo ni gharama kubwa sana na yote hayo anayafanya kwa sababu ana haki ya kuwatetea wananchi wa Magu.

Ngongoseke alisema kuwa ana ushahidi kuwa ndiye aliyekuwa mshindi wa jimbo hilo na kudai kuwa aliongoza kata 11 katika mchakato huo, lakini kutokana na shinikizo alilopewa msimamizi, aliamua kumtangaza Limbu mshindi.

CHANZO: NIPASHE

Na bado mbona ni wengi tu,uchaguzi huu ndo tutaona mahakama zikiwezeshwa.
 
Huyu Mh. Ngongoseke alishinda kihalali na cha kushangaza msimamizi wa uchaguzi alishindwa kusoma matokeo mapema kwa kuogopa kufutwa kibarua,cha kushangaza baada ya kusoma matokeo alitimkia mbali je huko si kupoteza kibarua?
 
Huyu limbu si sisiemu????????????? Toa hela kuinua Pipooooooooooooooooooooooooooooos Pawaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaas ili kuleta maendeleo- siyo kukuza ufisadi/rushwa/ushirikina etc
 
Nenda Ngongoseke, tupo nyuma yako kukusaidia kupata hadi ya wapiga kura na chaguo la wapiga kura
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom