Allist

Member
Jun 17, 2019
7
45
Habari wana jamiiforum,

Kwanza kabisa namshukuru Mungu kwa kunipa afya njema hadi muda huu, natumai na ninyi ni wazima, kama ni mgonjwa mungu akupe nafuu uweze kupona.

Nimeamua kuchukua nafasi hii kuelezea athari za video za ngono (porn) katika ubongo wa mwanaadamu, hasa kwa sisi vijana tunaochukua muda mwingi kuangalia video hizi na jinsi zinavyosababisha upungufu wa nguvu za kiume na jinsi ya kutibu tatizo hili.

Ni ukweli usiopingika kuwa kutokana na maendeleo ya teknolojia na kuwepo kwa internet yenye spidi vijana wengi wamekuwa wakitumia muda mwingi au Mara kwa Mara kutembelea kurasa zenye video za ngono na kuangalia kwa muda mrefu bila ya kujua kuwa zina athari kubwa sana katika ubongo, japo jambo hili limekuwa likifumbiwa macho sana.

JINSI UBONGO UNAVYOATHIRIKA NA VIDEO ZA NGONO

Jinsi ubongo wetu ulivyoumbwa ni wenye kubadilika kulingana na tunavyoufundisha kwa vitendo tunavyovifanya mara kwa mara ubongo huvihifadhi na kuwa kama tabia.

Mfano kuna mwanasayansi alimfundisha mbwa, akawa anagonga kengele kisha anampa chakula kwa muda fulani, kisha siku akagonga kengele bila ya kumpa chakula mbwa alionekana kutoa mate, hii ilitokana kuwa ubongo ulishakariri kitendo cha kugonga kengele chakula kinakuja, vivyo hivyo ubongo wetu unayofanya kazi.

Video za ngono husababisha uzalishaji wa homoni inayosababisha mtu kupata raha (Depomine) kwa wingi sana katika ubongo hivyo hupelekea sehemu inayohusika na kutupa raha katika ubongo kuathirika kutokana na wingi wa homoni ya dipomine, hivyo husababisha ubongo kubadili sehemu hii kwa kuipunguzia uwezo wa kutafsiri (detect) homoni hii
hivyo ili mtu aweze kupata raha tena itambidi awe na kitu kitakachozalisha homini hii kwa wingi hapa ndipo mtu huzidisha kuangalia video za ngono kwa wingi tena tofauti tofauti na hii hupelekea ubongo kukariri kuwa kitu sahihi kinachokupa raha ni kuangalia video za ngono na kupiga punyeto na sio kufanya mapenzi na mpenzi wako ama mke.

Hivyo hii hupelekea mtu kukosa msisimko wa kihisia anapokuwa na mpenzi wake, na kupelekea kushindwa kusimamisha uume au hata akiweza husimama lege lege, na kwa wengine huweza kusimamisha lakini kushindwa kabisa kufika kileleni au kuchelewa kufika na wengine kufika kileleni maapema zaidi kuliko kawaida.

ATHARI ZITOKANAZO NA UANGALIAJI WA VIDEO ZA NGONO

Moja ya athari kubwa ni

1. UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME
Kuchelewa kufika kileleni na wengine kushindwa kabisa kufika kileleni hii inatokana na tendo la ndoa kushindwa na mwanamke kushindwa kumpa raha mwanaume ukilinganisha na raha anayoipata akiwa anaangalia video za ngono hii ni kwasababu sehemu inayo husika na kumpa raha mwanaume katika ubongo kuathiriwa na uangaliaji wa video za ngono

Uume kushindwa kusimama unapokuwa na mwanamke (mke au mpenzi) lakini husimama ukiwa peke ako au ukiwa unaangalia video za ngono. hii hutokea kwa sababu ubongo wako umekariri kuwa picha za ngono ndio sahihi kwako kukupa burudani na sio mwanamke halisi.

Ndio maana sasa kumekuwa na dawa nyingi sana za kuongeza nguvu za kiume mitaani lakini zimekuwa sio msaada kwa vijana, na vijana wengi wa umri mdogo wamekuwa tegemezi kwenye dawa hizi, wakati tatizo lao halilingani na umri wao,

Njia sahihi ya kuondosha tatizo hili kwanza ni kujua chanzo cha upungufu wa nguvu za kiume kisha ndo kutafuta suluhu, kama tatizo lako linatokana na uangaliaji wa video za ngono basi hakuna dawa itakayo kusaidia kama si kuacha kutazama video hizo.

2. KUKOSA MVUTO NA MWANAMKE WA KWELI
Waangaliaji wa video za ngono wengi wanakosa mvuto kwa wanawake, hawavutiwi sana na wanawake, na wala hawachukuulii tendo la ndoa kama ni kitu muhimu kwao, wao kupiga punyeto na kuangalia video za ngono ni bora zaidi.

3. MSONGO WA MAWAZO NA KUJITENGA NA JAMII
Kuwa na msongo wa mawazo na kukosa uwezo wa kufikili kwa kina (concentration) katika kazi, masomo n.k, Pia waangaliajia wa video za ngono Mara nyingi hutumia muda mwingi kukaa peke yao, ama ndani na kujitenga na zamii, wanashindwa kujichanganya na watu.

JINSI YA KUONDOKANA NA ATHARI ZA VIDEO ZA NGONO

Njia pekee ya kuondokana na athari hizi ni kuacha kuangalia video hizi japo kuwa ni ngumu lakini kuna mbinu ambazo zinaweza kukusaidia kuondokana na tatizo hili, kama ilivyo kwa mbwa baada ya mwanasayasi kuacha kumpa chakula kwa kugonga kengele, baada ya muda mbwa hakuonekanaa akitoa mate tena kwa kugonga kengele,

Vilevile hata ubongo wetu huweza kurudi katika hali yake ya kawaida na kurudisha uwezo wetu wa asili, nguvu zetu za asili kwa kuacha kuangalia video hizi na kupiga punyeto

Ili kurudi katika hali ya kawaida inategemea umeathirika kiasi gani na video za ngono, kama ulianza kuangalia video hizi ukiwa na umri mdogo (chini ya miaka 17) zaidi huchukua muda zaidi ukilinganisha na walio anza kuangalia wakiwa na umri mkubwa hii inatokana na ubongo wao tayari ulikuwa umeshakomaa

Kuna ambao hurudi katika hali ya kawaidi ndani ya wiki chache miezi michache wengina hadi mwaka au miaka miwili, inategemea na mwili wa mtu na ukubwa wa tatizo, lakini nashauri kima cha chini kiwe ni miezi mitatu ama siku 90.

MBINU ZA KUWEZA KUACHA KUTAZAMA VIDEO ZA NGONO

1. KUWEKA MBALI VISABABISHI
Weka mbali vitu nyote vinayopelekea kuanzangalia video za ngono mfano kama ulikuwa unaangalia kabla ya kulala, basi kabla ya kupanda kitandani zima simu na computer yako, kama ilikuwa ni pale unapokuwa peke ako basi epuka kukaa peke ako kwa muda.

2. JICHANGANYE NA JAMII
Kujichanganya na marafiki na jamii kutasaudia kupunguza muda wa kukaa peke ako na kuanza kuwaza kuhusu kuingia mtandaoni na kutafuta kurasa za ngono

3. FANYA MAZOEZI
Mazoezi ni muhimu sana kwa miili yetu hivyo itakusaidia kuurudisha ubongo kwa haraka katika hali yake ya kawaida ipi utapunguza msongo wa mawazo

4. JIFUNZE KILA SIKU JINSI YA KUBORESHA MBINU ZA KUACHA
Tafuta majarida mbali mbali na makundi mbali mbali ya watu walio dhamiria kuacha kuangalia video za ngono ili kupata mawazo mapya, na jinsi watu walivyo fanikiwa na kurudi katika hali yao ya kawaida

5. WEKA MIPANGO YA KUDHAMILIA KUACHA
Weka mpango wako wa kudhamilia kyacha Kwa kipindi Fulani kama ni miezi mitatu, minne au zaidi na jikumbushe mpango wako Mara kwa Mara na kupiga mabadiliko yanayo onekana.


MABADILIKO YATAKAYOJITOKEZA WAKATI WA KUACHA

Japo sio kwa wote wanaoweza kuona dalili hizi za kuacha

1. Maumivua ya misuli
2. kukosa usingizi
3. Kushindwa kupumua vizuri
4. Homa
5. Kukosa hamu ya kufanya mapenzi kabisa na muda mwengine uume kushindwa kusimama
6. Maumivu ya kichwa

Kutokana na ukomo wa maneno ya kuandika naomba niishie hapa japo bado kuna vitu Vingi sana kwenye hii mada, mana inapaswa iandikiwe kitabu kabisa ila kama unaswali naomba uliza utajibiwa

Pia ukitaka ushauri jinsi ya kuondokana na janga hili niandikie, tusaidiane kuondosha athari hizi katika jamii yetu. Tusiwe wajinga kushirikishana wala kuomba ushauri mana afya ni yetu na tunapokaa kimya sisi ndo tunao umia

USISAHAU KULIKE KUSHARE WENGINE WANUFAIKE NA KUNIPIGIA KULA
AHSANTENI MUBARIKIWE SANA
 
Upvote 1

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom