Acha niitwe mchochezi: Uchumi wa Tanzania ulijengwa na Mkapa, Kikwete akatuuza hivi na Magufuli naye Mhh

britanicca

JF-Expert Member
May 20, 2015
15,635
29,967
Deni la Taifa kwa sasa ni trillion 41 ambako uchunguzi unaonesha kwamba kila awamu ina mchango katika deni la Taifa , lakini awamu ya kikwete ilitia fora

1.Mwalimu Julius Kambarage Nyerere 3 trillions
Huyu mzee deni lake limekuja mwaka 1979 wakati wa vita lakin kipindi cha nyuma alikuwa na.clean sheet
Nitaanzia kumchambua Mwinyi Mkapa na Kikwete, Maana ubovu wa mwinyi alirekebisha Mkapa , Kikwete akaturudisha kwa Mwinyi

2.Ali Hassan Mwinyi 18 trillions

Inamaana mwinyi amekopa Trillions 15

3.Mkapa huyu mr clean alipokuja alifuatiliwa na sana na mwalimu nyerere na kumpa maelekezo kurekebisha ya mwinyi kupitia aliyofanya Mkapa utagundua yapi yalikuwa madhaifu ya Mwinyi

Mkapa alipokuja akalipa na kushusha deni la Taifa mpaka 10 trillions,

Mkapa amepokea nchi mwaka 1995, huku ukuaji wa uchumi ukiwa asilimia 4.2. Alipoondoka madarakani uchumi ulikuwa asilimia 6.7

mwaka 1995 mfumko wa bei ulikuwa asilimia 21 lakini mwaka 2005 kipindi chote cha Mkapa mfumko huo ulishuka mpaka asilimia 4.

Mkapa alipokea serikali riba ya benki ikiwa asilimia 30 hadi 26 mwaka 1995. Mwaka 2005 riba ya benki ilishuka hadi asilimia 14.

Mkapa kapewa nchi ikiwa haikopesheki mwaka 1995. Mwaka 2005 deni la taifa lilikuwa Sh 10 trioni. Leo miaka 10 katika utawala wa Rais Kikwete, deni lilifika Sh. 35 trioni. Ziada ya Sh. 25 trioni na kilichofanywa na deni hakionekani

wakati Mkapa anaingia madarakani mwaka 1995, akiba ya fedha za kigeni zilikuwa za miezi miwili; hadi mwaka 2005, akiba hiyo ilifikia ya miezi nane.


4.Jakaya kikwete amekopa mpaka 35 trillions inamaana trillions 25 amekopa kikwete

chini ya utawala wa Kikwete, riba ya benki imepanda hadi asilimia 18.

ukilinganisha na Mkapa alipewa nchi ikiwa haikopesheki mwaka 1995. Mwaka 2005 deni la taifa lilikuwa Sh 10 trioni. Lakin miaka 10 katika utawala wa Rais Kikwete, deni lilifika Sh. 35 trioni. Ziada ya Sh. 25 trioni

Mkapa aliacha nchi ikiwa inakusanya mapato ya ndani zaidi ya asilimia 14 ya pato la taifa mwaka 2005. Kwa kwa kikwete, kodi iliyokusanywa ni asilimia 12 ya pato la taifa.


KWA UPANDE WA MAGUFULI
5. Mpaka sasa Magufuli kakopa trillions 6, kwa miaka 2 aliyoingia

Bongonewz Magazine: MMH!! SERIKALI YA KIKWETE YAONGOZA KWA KUKOPA: DENI LA TAIFA LAFIKIA TRILIONI 21

RICHARD KAMNDE: DENI LA TAIFA LAFIKIA TRILION 40 IMF YAIONYA SERIKALI

Deni la taifa Tz laongezeka hadi trilioni 40

Kafulila: JK kavunja uchumi aliouweka Mkapa

Angalia kuporomoka kwa shillingi tokea tumepata Uhuru
 
Mkuu mimi nakua usd ilikuwa shillingi tano tu.Vita ya Kagera inaanza shilingi yetu ilikuwa ngangarini shilingi 8 kwa usd.Sasa hivi shililingi imeshuka kwa kiwango kikubwa kwani hatuzalishi tumegeuzwa omba omba.

Mkuu mfano wako umekosa mantiki,uje hapa na maelezo yenye mashiko sio kuleta figures tu.
 
Mkuu mimi nakua usd ilikuwa shillingi tano tu.Vita ya Kagera inaanza shilingi yetu ilikuwa ngangarini shilingi 8 kwa usd.Sasa hivi shililingi imeshuka kwa kiwango kikubwa kwani hatuzalishi tumegeuzwa omba omba.
Mkuu mfano wako umekosa mantiki,uje hapa na maelezo yenye mashiko sio kuleta figures tu.
kaanzishe uzi wako wenye mashiko ili tujifunze mkuu
 
1 Nyerere kaikuta hela ya mkoloni kwenye account ya nchi ndio imemsaidia sana.

2 Mwinyi nae alikuja na ari ya mzee ruksa, alinyayua maisha ya Watanzania. Kutoka kuvaa matenge na kula mahindi.

3 Mkapa huyu kaiuza nchi mpaka nyumba za serikali na mali zote za umma. Amefikia kujirisisha mgodi na kujipa tenda bandarini pale.

4Kikwete huyu nae sijui alikuwa mgogo? Manake alikuwa anaomba hataree na mali zote kuwapa wanawe.

5 Magufuli huyu sitaki kusema mengi ndio kwanza hajamaliza muda wake. Lakini nae ana historia ya kuuza nyumba za serikali, na kufanya maamuzi ya ajabu sana.

Siwezi kumpa makosa kwa sasa mpaka muda wake umalize ndio tutajua wapi kapatia na wapi kakosea.


Ndukiiiii
 
Ukweli ni kwamba kikwete ametuaribia nchi na kina Nyalandu wake, kutwa marekani kupiga picha na chrisbrown, nani mshamba kati yake na Magufuli??

Maana ukikua una desire kununua sub woofer na hauna hela siku ukinunua utawasumbua wapangaji na loud music, na hapo ndo ushamba uonekana
 
8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom