Acha kukimbizana na kila fursa inayokuja mbele kabla ya kwanza haijasimama

Makirita Amani,

Nimependa sana hili bandiko ila nitachangia mambo mawili matatu kupigia msumari. Nafikiri moja ya changamoto ya kizazi hiki chetu cha sasa ni SUBIRA/UVUMILIVU.

Kizazi hiki kinataka matokeo makubwa na ya haraka. Sasa sisemi kuwa matokeo ya haraka hayawezekani ila kila kitu duniani kina mchakato na ili ufanikiwe lazima kuhakikisha unafuata mchakato husika na unakuwa na subiri kuhakikisha unaona mwisho wake.

Mafanikio ya kudumu yanahitaji muda wakati mwingine. Mfano Unakuta anaanza kazi leo baada ya miezi 2 anakuambia natafuta kazi nyingi, sijaipenda kazi yangu.

Sasa ndani miezi 2 hata kazi hujaelewa, hujatengeneza mahusiano ya maana na watu sehemu ya kazi matokeo yake unaishia kutangatanga huku na kule huoni matokeo.

Mimi nasema kama kijana fanya kazi kwa bidii, fanyia kazi mawazo ikiwezekana wazo kwa wakati na hakikisha unafikia hitimisho kabla ya kujaribu hiki na kile.

Utaishia kuwa kama fisi aliyetaka kula chakula kwenye sherehe mbili alizoalikwa akaishia kukosa misosi pande zote mbili. Hizi stori mzirudie zilikuwa zina mafunzo makubwa sana jamani!
 
Watu hawapendi kusikia changamoto, wanataka kusikia habari nzuri nzuri tuu kuhusu biashara fulani, ukimwambia changamoto anaipiga chini.
 
Lakini msisahau ushauri wa wataalam wanaosema pia usiweke mayai yote kwenye kapu moja!!!

Hawa wote wanauzoefu kuhusu maisha!
 
Makirita Amani,
Mkuu umemuibia Ontario kule Instagram ungempa credit japo kdogo mana idea yote umeshuka nayo nzimanzima japo umebadili majina ,
 
Mkuu umemuibia Ontario kule Instagram ungempa credit japo kdogo mana idea yote umeshuka nayo nzimanzima japo umebadili majina ,
Mkuu,
1. Sipo Instagram.
2. Simjui Ontario
3. Nimekuwa naandika mambo haya kwa zaidi ya miaka mitano sasa.
Hizi ni baadhi ya makala zinazoendana na hizi ambazo nimeandika miaka ya nyuma;
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom