Acha kukimbizana na kila fursa inayokuja mbele kabla ya kwanza haijasimama

Makirita Amani

JF-Expert Member
Jun 6, 2012
1,781
3,074
Kuna fursa mpya imekuja, umeshawishiwa kwamba ni nzuri na ukafanya maamuzi ya kuingia kwenye fursa hiyo. (fuga kware)

Umeamua kuingia, wakati unaanza kufanya unakutana na ugumu fulani, kabla hujaanza kutatua ugumu uliokutana nao, unasikia kuna fursa nyingine bora zaidi ya hiyo ya kwanza. Hii ya sasa ni ya uhakika zaidi inalipa zaidi na haisumbui. (fuga sungura, ndiyo habari ya mjini).

Unaingia kwenye fursa ya pili nayo unaianza, ukiwa na matumaini makubwa, lakini pia unakutana na baadhi ya changamoto kwenye fursa hiyo, ambazo awali hukuambiwa. Wakati unaanza kufanyia kazi changamoto hizo, unasikia kuna fursa nyingine kabambe, hiyo siyo ya kukosa, ni nzuri, na haikuhitaji wewe ufanye kazi kabisa, ni kukaa kwenye mtandao tu kwa dakika chache na kuingiza fedha. Oh, tena huhitaji kufanya, wewe unaweka tu hela na wataalamu wanakusaidia kufanya unasubiri kupokea tu faida (fanya forex au cryptocurrency).

Kama mpaka sasa hujaelewa kinachoendelea hapo, una tatizo, na nipo hapa kutatua tatizo hilo.

Iko hivi rafiki, kila fursa ni nzuri na ina changamoto zake, kila fursa ina ugumu ambao lazima ukutane nao, uuvuke na ndiyo uweze kufanikiwa.

Sasa unapokutana na ugumu kwenye fursa moja, usikimbilie kwenye fursa nyingine, badala yake tatua ugumu huo na kuendelea na fursa hiyo mpaka ufanikiwe.

Ninachokuambia leo ni hiki; ACHA kukimbizana na kila aina ya fursa mpya inayokuja. Hutafanikiwa kwa kujaribu kila fikra, bali utafanikiwa kwa kuchagua fursa moja na kuifanyia kazi kweli mpaka kufanikiwa, na hapo utakutana na magumu na changamoto nyingi, katika kuyavuka magumu hayo ndiyo utafanikiwa.

Bilionea Richard Branson amewahi kusema fursa ni kama daladala, ukikosa moja jua kuna nyingine inakuja. Hivyo ACHA kabisa kukimbizana na kila aina ya fursa, chagua kitu kimoja na kifanye, weka kazi, weka muda na kuwa na subira na ung’ang’anizi mpaka upate kile unachotaka.

Na kwa kumalizia, ukiona unakaribishwa kwenye fursa ambayo unaahidiwa kupata fedha bila ya kufanya kazi yoyote ile, yaani wewe unaweka tu fedha halafu kwa namna fulani zinazaliana na unavuna faida kubwa na kwa haraka, basi jua hili; WEWE NDIYO FURSA YENYEWE.

ACHA kukimbizana na kila aina ya fursa, chagua kitu kimoja au vichache utakavyofanya mpaka ufanikiwe.

Usomaji wa vitabu ni njia bora ya wewe kuweza kufikiri kwa usahihi na kuepuka kugeuzwa kuwa fursa kwa wengine.
 
Usomaji wa vitabu ni njia bora ya wewe kuweza kufikiri kwa usahihi na kuepuka kugeuzwa kuwa fursa kwa wengine. Karibu ujiunge na channel yetu ya SOMA VITABU TANZANIA ambapo kila wiki unapata vitabu vizuri pamoja na uchambuzi wake kwa kina. Jiunge sasa na channel ya SOMA VITABU TANZANIA
Uzi Bora tangu najiunga jf
 
Unajiunga vpi sasa kwenye huo mtandao wenu
 
manengelo Mama wa kila fursa
😅😅 ww unasumbukaga sana na mm!...huwez nielewa kijuu juu !...ww ubahis mm nimeanza mishe ukubwani!so ukiona nimekoment kwenye biashara fulan unahis nazengua ..mwenzako nimezaliwa kwenye familia ya biashara nakazi!...nna mambo mengi sana nayajua!relax!

Then hata km ww unaumia nn na mm!nimewah kukuomba hta buku!
Relax!
 
Achana naye mwehu hyo..daily kunifata fata km ananidai .tena ngoja nimuignore!.

Na ukiona pesa unafundishwa kuitafuta kwenye makaratasi jua siku zote field utafeli, lazima uanguke mara nyingi ukomae hadi ukipata hasara kichwa hakiumi tena hapo unakua mkomavu na mtu akitaja kitu fulani unakua unakifahamu vizuri , nakuunga mkono kwenye kutafuta tunapitia mengi tena watu au mtu asikubeze kabisa kwa hustlers tunajua faida ya kujichanganya kwenye issue nyingi.
 
Andiko hili ni zuri lakini hapa chukua mawazo asilimia 20 halafu themanini utaziona field ndio maana hata watafiti huanzia field kwenye maandishi wanachukua kanuni za utafiti na sio utafiti wenyewe
 
Wewe mwandishi na wale wanaotoaga maada au midahalo hua mnachofanya ni kutoa historia ya waliofanikiwa na sio kutoa mbinu za kufanikiwa maana na ninyi hua hamuelewi mambo mengi kwenye kutafuta pesa zaidi utanieleza uniuzie kitabu hapo ushanigeuza fursa tayari na pesa haifundishwi kutafuta darasani hapo ndio wasomi wanapofeli utaanza mambo ya risk taking mara uogope hasara wakati mwenzako ashaenda zambia kuchukua Dragon ashaziingiza kwa njia za panya na kapiga pesa kawekeza kwingine unakuja shtuka na vibali vyako ishakua sio biashara tena
 
Naamini tu mwenye kujiamini watu wengi hupata pesa lakini kuimiliki pesa ndio mtihani lazima ujiamini na uwe na roho ngumu kweli kweli, jiulize kama wazungu wanakuaja na mitaji mikubwa na bado wanakwepa kodi je wewe mwenye mtaji wa tia maji tia maji itakuaje? Na hakuna mfanyabiashara duniani kote anaelipa kodi akiwa amefurahi maana lengo la mfanyabiashara ni kuongeza faida unapoipunguza ile faida hapo unamfanya abuni njia mbadala ya kuiongeza kwa mfano kupunguza kipimo cha bidhaa au namna nyingine
 
Na kwa kumalizia, ukiona unakaribishwa kwenye fursa ambayo unaahidiwa kupata fedha bila ya kufanya kazi yoyote ile, yaani wewe unaweka tu fedha halafu kwa namna fulani zinazaliana na unavuna faida kubwa na kwa haraka, basi jua hili; WEWE NDIYO FURSA YENYEWE.
🔨🔨🔨🔨
 
Na ukiona pesa unafundishwa kuitafuta kwenye makaratasi jua siku zote field utafeli, lazima uanguke mara nyingi ukomae hadi ukipata hasara kichwa hakiumi tena hapo unakua mkomavu na mtu akitaja kitu fulani unakua unakifahamu vizuri , nakuunga mkono kwenye kutafuta tunapitia mengi tena watu au mtu asikubeze kabisa kwa hustlers tunajua faida ya kujichanganya kwenye issue nyingi.

Anadhan ndo wale wakukimbilia biashara za kware bahat mbaya sijawah fanya biashara za mikumbo hata siku moja!anitue!
 
Fursa zinasimama...

Ukiaanza kuisikia fursa kila sehemu na kila mtu anaiongelea ujue ushachelewa..., and more times than not utaambulia makombo.., fursa haitangazwi wala kupewa fursa inanuswa na mnusa fursa inabidi ajue atai-monetize vipi.., wewe unaweza kushindwa mwingine akaweza, kila kitu kina siri zake (secrets of the trade)
 
Back
Top Bottom