Acha kufanya investiment kwa hawara, acha kufanya investiment kwa hako kamchumba

EllySkyWilly

JF-Expert Member
Aug 28, 2020
2,204
2,083
Yawezekana boyfriend wake wameachana kaamua kupost, hiyo ndio changamoto ya vibinti vyenye rangi. Kikianza kumwacha boyfriend hakitumii kanuni ya pythogras.

Inatakiwa unapomwacha mtu unaanza taratibu taratibu ili mtu asichanganyikiwe. tatizo hapo utakuta kalimtumia tu sms kuanzia leo mimi naww basi alafu kaka mblock.

Newton Third law of motion inasema to every action there's an equal and opposite reaction. Yaani kwamba kwa kila kani mkaabala kuna kani mrejeo inayofanana hiyo. Hiyo law ina apply hata kwenye maisha ya kawaida.

Kunakipindi penzi huwa linakoleaga mpaka mnahisi mko peke yenu kwenye sayari nyingine wala hamwoni watu wengine.

Ndio maana wengine wanasema mapenzi ni upofu wengine wanasema ni uchizi.

Hivyo wakati wa kipindi kama hicho wakati tension au kani mnyanyuo ya penzi ipo juu sana, mnaweza mkafanya lolote lile hata lisilo la kibinadamu. kwasababu ile kani inawafanya mwonekane kama mmerukwa na akili.

Ndio sababu utakuta mtu akiambiwa tuma na ya kutolea anatuma tu.

Chukulia mfano ndio kibinti kimetoka six, tu ndio kinaingia chuo, kibinti chenyewe kilikua kinafungiwa ndani tu kimesomaga shule za girls tu, kinaenda kuyaanzia mapenzi chuoni, kiboy nacho kilikua full msuli kimesoma sijui ni shule za boys hata hakijawai kujua radha ya mahusiano, ndio wamekutana chuo wanayaanza niambie hapo sasa hekima ya kufanya maamuzi chanya kwenye mahusiano inatoka wapi.

Hekima ya mahusiano inapatikana baada ya kuwa mzoefu kwenye mahusiano hapo ndio unajua maamuzi haya sio mazuri haya.

Utakuta lijamaa limechizika mpaka linafanya investment ya 100 percent kwa mwanamke.

Ndio sababu ulisha ambiwa usije mshauri ndugu yako kuwekeza kwa mwanamke. Investment ikiwa kubwa mwisho wake ndio huo.

Huyo boy kamalizia pesa yake hapo ndio maana kafanya yote hayo. Hata kama pesa inarudishwa. How about time, brain energy and immonational.

Unajua mtu mpaka mtu kufanya investment anakuwa kesha toa akili yote, muda plus energy. So hata ukirudisha pesa zake huwezi kumrudishia energy, time and immortional.

Mapenzi kweli ni utoto duu kama sio uchizi tena. Mpaka lijamaa linaamua kuchukua kamba kisa papuchi. Lijamaa linaamua kuvujisha picha kisa limenyimwa papuchi huo ndio utoto na uchizi uliomo ndani ya mapenzi.

Kuna kabinti kalisomeshwa na dereva wa bodaboda from first year to fourth year pale UDOM. Sasa return ya investment ya mshikaji pindi kanakaribia kuhitimu kalimwambia naomba uorodheshe vitu vyote ulivyo nisaidia plus pesa uliyo tumia kunilipia ada. Na kuanzia leo tusizoeane Jamaa akasema unasemaaa. Kakamjibu na naenda kukublock. Sasa mshikaji bwana alikua na mke wake na mtoto. Mshikaji anajipinda pesa yote anawekeza kwa binti yaani. Jamaa aliichukua kamba akaona isiwe kesi, akaamua kuharibu ushahidi.

Kweli mapenzi ni utoto na uchizi yaani jamaa limeenda mpaka dukani kununua kamba likajitundika. Unadhani lilikua linajielewa kani kani mkabaala kani mnyanyuo ndio ilikuwa inafanya kazi hapo.
Kani mkabaala mnyanyuo ikiwa kubwa sana matumizi ya akili kwenye mahusiano inakua negligible.

Acha kufanya investiment kwa hawala, acha kufanya investiment kwa hako kamchumba, fanya investment kwa mke wa ndoa na watoto ndio investment yenye positive return.
 
Sawa nimeelewa hapo mwisho, lakini issue siyo kufanya investment kwa hawala Bali ni kuwa na moyo wa kupokea Jambo zito na kulifanyia uamuzi, ukiwa a na na uwezo wa kufanya uamuzi sahihi...basi mengine hayatakusumbua...habari za kujiua, kusambaza picha hautakuwa nazo
 
"Third law of motion inasema to every action there's an equal and opposite reaction. Yaani kwamba kwa kila kani mkaabala kuna kani mrejeo inayofanana hiyo" ..........

Kwa mapezi sio, reaction ya kuachwa ni zito ×2 kuliko action yenyewe ushauri wangu nikwamba fall in love with the one you can afford to leave easily
 
Wanao jua mapenzi wanawekeza bila kutegemea return cha msingi wanapata wanachi hitaji wakati huo.. sema wanawekeza kwa akili ili wavune zaidi ya wanacho wekeza.

Usipowekeza hupati kitu.. wasichana wazuri siku zote hubebwa na matapeli waliowekeza kwenye mdomo.
 
Back
Top Bottom