Acha kubisha bisha kwa kitu usichokijua....

Michael Chairman

JF-Expert Member
Apr 11, 2015
922
581
Kuna mambo mengi nchini kwetu kwa nyakati kama hizi huenda yanakwenda kama kutokujua ama yanakwenda kama taarifa za moto moto ama mpya zinazovuma, na wadadisi wa mambo na waona mbali hutoa tahadhari juu ya kujiweka karibu na ulaji wa taarifa maana kuna lundo la taarifa huja kuibua hisia zako za kitashitwitwi na kukufanya utake kusikiliza , kuona ama kujihusisha nazo taarifa hizo.
Hapo ndiyo tunasema kwamba acha kubisha bisha kwa kitu usichokijua...... maana majibu mengi kwako yatakuwa ni bado!!? sasa angalia mlongo mlongo wa taarifa hizi ujipime kama unaweza kubisha ama unaweza kujibu bado.


1. Wasaliti ndani ya chama kuvuliwa uanchama na kupewa tena uachama wao umewahi kuona ?

2. Rais kufanya kazi na kubarikiwa na Mungu mpaka akamshangaa Mungu kwa Baraka alizo mtunuku kufanikisha mambo makubwa kwa kipindi cha muda mchache wenye mfanano wa miaka 30 umewahi kuona?

3.Wapinzani kuhoji tena ujio wa ndege na kukufuliwa kwa shirika lilowahi kufa na wakahoji kwa miaka mingi uzembe wa serikalia kushindwa hata kuwa ndege moja , zikaja ndege kama tano wakaja na hoji tena kwamba kwanini ndege tena umewahi kuona ?

4. Mamlaka kuwanyima wanaodhani watakuwa washindani wao wakibiashara kwa kuwanyima usajiri wa kuendesha biashara zao hapa nchini kwa kutumia sera za vyama vya upinzani za huko nyuma za kuitaka serikali kulinda soko la ndani kwa kuzuia bidhaa toka nje ya nchi hafu wakati huohuo wapinzani kuhoji tena kwanini shirika lile linanyimwa usajiri wa kurusha ndege zake hapa umewahi kuona?

5. Salamu za kufungia mwaka kutoka kwa watu wa kiroho zikilenga mambo ambayo huenda ni makubwa kwenye jamii ama ni madogo kabisa kwenye jamii umewahi kuona?

Tiririka nawe kama tunaweza kusaidiana kuwahi kuona.......?
 
Back
Top Bottom