Wasalaam ndugu zangu wa JF.
Natumai ni wazima na wa afya tele huku tukiendelea na jukumu la kujenga taifa letu mama la Tanzania.
Ndugu zangu kwa masikitiko makubwa niliyokuwa nayo ni juu ya viwango vya malipo ya uthibitisho wa vyeti vya elimu ya juu vinavyotozwa na TCU. Hivi sasa TCU wanatoza gharama ya Tsh. 100,000-150,000 kuthibitisha ubora wa cheti ulichosomea. Ukiangalia gharama hii ni kubwa sana ukilinganisha na actual cost ya zoezi lenyewe.
Mathalani umesoma vyuo vya nchi jirani kama vile Uganda, Malawi, Zimbabwe ambazo hata katika ushindani wa Currency tumewazidi kwa maana ya kwamba fedha yetu ina thamani kubwa kulinganisha na ya kwao. Pamoja na kupata maarifa hayo mapya ukirudi nchini kwetu unaambiwa tunataka tuthibitishe ubora wa cheti chako tena wanakutoza gharama ya juu zaidi.
Mhe Waziri Ndalichako tafadhali kiangalie tena suala hili.