According to Waziri Lukuvi, gharama za kumtunza Rais ni sawa na kutunza mikoa 5!!

JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
32,973
60,444
Haya aliyasema alipokuwa akizungumza kule Kanisani Dodoma.

Wengi walikuwa occupied na kauli za udini-udini alizozitoa matokeo yake wakapitwa na madai mengine makubwa aliyoyatoa kwamba gharama za kumtunza Raisi ni sawa na gharama za kutunza mikoa mitano Tz.

Hiyo ilikuwa ni moja ya hoja zake za kupinga mapendekezo ya kuanzishwa kwa serikali ya Tanganyika.

Sasa hapa sijui kama Waziri Lukuvi alikuwa anazungumzia gharama za kumtunza KIKWETE kwasababu huyu tunajua alikuwa amekufuru ktk matanuzi, au alikuwa anazungumzia Rais yeyote yule.

Lakini la muhimu zaidi, ni kwanini Rais wa Tanzania aigharimu nchi kiasi kikubwa cha fedha na rasilimali kiasi hicho?

Swali la kujiuliza ni hili: GHARAMA ZA KUMTUNZA RAISI MAGUFULI NI KIASI GANI? NI SAWA NA KUTUNZA MIKOA MINGAPI?

cc Zitto, GalaxyS3, Mag3, Kitila Mkumbo, Nyani Ngabu, The Boss, Ben Saanane
 
Hata zikiwa gharama za kumtunza Magufuli ni sawa na gharama za kuhudumia mikoa kumi hiyo kwangu ni sawa, kwani so far we are getting value for our money sio sawa na enzi za DHAIFU tulikuwa tunaliwa tu!!
 
Ningekuwa business partner wako basi nisingekuacha,ujinga wako ungekuwa faida kwangu kukuibia!Eti kwasababu Rais anatimiza wajibu wake,si kama aliyepita dhaifu basi ni halali akiitafuna nchi kwa kiwango chochote,wewe hujali ni sawa tu!Fikra kama zako ni hasara kwa nchi!
 
Hata zikiwa gharama za kumtunza Magufuli ni sawa na gharama za kuhudumia mikoa kumi hiyo kwangu ni sawa, kwani so far we are getting value for our money sio sawa na enzi za DHAIFU tulikuwa tunaliwa tu!!

..inawezekana kinachopelekwa mikoani ni kidogo sana.

..wewe uko radhi Raisi agharimiwe sawa na mikoa 10, mwingine anaweza kusema tutumie zaidi ya hapo, au chini ya hapo.

..lakini ni vizuri tukajua gharama hizo ni kiasi gani.
 
Back
Top Bottom