Acacia wazidi kusisitiza hawajawahi kuibia nchi na hawako tayari kulipa 108 trilioni

Naomba kuweka wazi kuwa, pamoja na juhudi za mazungumzo kati yetu na serikali ya Tanzania,hakuna makubaliano yoyote ya kulipa kama vyombo vya habari vinavyoendelea kuripoti. Kile kilichowasilishwa katika ripoti za kamati ya kwanza na ya pili sio matokeo sahihi, licha ya kile kinachoelezwa na kuaminika na wengi.

Hatujawahi kuiba, hatujawahi kukwepa kodi, hatujawahi kughushi nyaraka kukwepa kulipa mirabaha na hatujawahi kuendesha shughuli zetu kinyume cha sheria. Nitaeleza hapa chini kwanini madai yaliyotolewa jana siyo ya kweli na kwa nini Mheshimiwa Raisi kwa mara nyingine amekabidhiwa taarifa isiyokuwa sahihi na Kamati yake.

Tunaendesha shughuli za Acacia kama kampuni ya kimataifa, na kutarajia watu wetu wote kuwa na uadilifu wa hali ya juu. Tuhuma dhidi yetu haziwezi kuwa na ukweli wowote.

Tuziangazie tuhuma hizi kwa ukaribu zaidi: tumetuhumiwa kuendesha shughuli zetu kinyume cha sheria kwa miaka 19 iliyopita kwani kampuni ya Acacia Mining plc haijasajiliwa nchini. Hatuendeshi shughuli zetu kinyume cha sheria. Migodi yetu inamilikiwa na kuendeshwa na kampuni zilizosajiliwa nchini Tanzania na zinazotambulika kwa mujibu wa sheria.

Kampuni hizi (Pangea Minerals Limited, Bulyanhulu Gold Mine Limited na North Mara Gold Mine Limited) zinalipa kodi zote stahiki na huwasilisha taarifa zake za mapato kwa TRA. Kampuni hizi kwa ujumla wake humilikiwa na Acacia Mining plc, ambayo ni kampuni mama ya kundi la makampuni ya Acacia. Acacia ni chapa ya kampuni nchini Tanzania. Acacia group inajumuisha makampuni mbalimbali duniani kote, ikiwa ni pamoja na nchi nyingine za Afrika ambapo tuna miradi: Kenya, Burkina Faso na Mali.

Acacia ni kampuni iliyoanzishwa na kusajiliwa nchini Uingereza. Naomba ifahamike kuwa tumekuwa tukijaribu kuielezea TRA kwa miaka kadhaa kwamba Acacia Mining PLC ni kampuni iliyoorodheshwa katika masoko ya hisa ya London na Dar es Salaam na inamilikiwa na mamia ya wanahisa.

Muundo huu wa uendeshaji ni sawa na ule uliopo katika makampuni mengi ya kimataifa yanayoendesha shughuli zake nchini Tanzania na haupo kinyume cha sheria wala haujalenga kukwepa kodi kwa njia yoyote ile. Muundo huu pia sio suala la siri. Tumekua tukitoa taarifa juu ya muundo huu kwa umma katika taarifa zetu zilizofanyiwa ukaguzi za mwaka, na kwa TRA na kwa wakala wengine wa serikali.

Muundo huu uliunda sehemu ya mafungamano “memorandum” yaliyopitishwa na Mamlaka ya Masoko ya Hisa na Mitaji (CMSA) wakati wa kipindi cha uorodheshwaji katika soko la hisa la Dar es Salaam (DSE) mwaka 2011.

Tulituhumiwa pia kwa kutokulipa kodi inayofikia Dola za Kimarekani bilioni 50 (TSH110 trilioni). Hii sio kweli. Hebu tuweke namba hii katika mtazamo. Kama idadi hii ni sahihi, na kwa kutumia kiwango rahisi cha kodi cha 30% ya mauzo (ambayo sio faida inayokatwa kodi) ingeashiria kuwa tumekuwa na mauzo ya zaidi ya Dola za Kimarekani bilioni 150 (TSH330 trilioni) kwa miaka 15 iliyopita. Kuweka rekodi sawa - kama hii ingekua na ukweli, tungekuwa kampuni kubwa ya uchimbaji ulimwenguni (sio madini ya dhahabu tu).

Kampuni kubwa ya uchimbaji madini duniani ni BHP, ambayo ina karibu migodi 20 katika nchi 10 na ina thamani ya zaidi ya Dola za Kimarekani bilioni 90 (TSH200 trilioni). Ni dhahiri kwamba hii haiwezi kufikiwa na migodi yetu mitatu. Thamani ya kampuni yetu kwa ujumla hadi kufikia leo ni karibu Dola za Kimarekani bilioni 1.2 (TSH2.6 trilioni) na tunaombwa kodi inayofikia Dola za Kimarekani bilioni 50 (TSH108 trilioni). Haileti maana.
Juni 15, 2017
Brad Gordon
Mkurugenzi Mtendaji

Taarifa kufuatia matokeo ya Kamati ya Pili
www.acaciamining.com
Kwa uhalisia jumla ya mapato tuliyopata kutoka Bulyanhulu na Buzwagi tangu tumeanza uzalishaji ni chini ya Dola za Kimarekani bilioni 6 (TSH13.2 trilioni), hii ikijumuisha tofali za dhahabu. Kama ni makinikia pekee, thamani yake ni Dola za Kimarekani bilioni 3.3 (TSH 7.2 trillion) kwa takribani miaka 15.

Kama mnavyofahamu, tunakaguliwa hapa nchini na kimataifa (na makampuni ya ukaguzi yanayotambulika kimataifa yanayo kagua kampuni nyingi katika sekta tofauti duniani kote), huku tukiuza tunachozalisha kwa wafanya biashara na wachenjuaji wanaotulipa thamani halisi ya kinachopatikana na kukitangaza kwa uwazi. Tungeweza vipi kukwepa kodi yenye thamani mara kumi ya mauzo yetu? Hili lisinge wezekana.

Sitaelezea tuhuma zote hapa, ila nataka kueleweka, tumetangaza kila tunachozalisha na kuuza. Kwa mfano, hatujajaribu kuficha idadi ya makontena tunayouza. Hata hivyo hili lisinge wezekana ukichukua idadi kampuni na taasisi za serikali zinazohusika katika usafirishaji, kushughulikia huduma za bandarini, usafirishaji kwa meli na uchenjuaji.

Siku ya jana ilikuwa ya kufedhehesha na kusikitisha kwa kuwa inatishia uhai wa kampuni yetu. Matokeo ya uchunguzi wa kamati ya pili unaonekana kutegemea matokeo uchunguzi wa kamati ya kwanza ambayo tumerudia kupingana nayo, na hayashabihiani na vipimo vilivyofanywa kwa zaidi ya miaka 20 na vyombo huru vya utafiti vya kitaifa na kimataifa zikiongeza kwa kiasi kikubwa kiasi cha madini katika makontena. Tunapiga matokeo ya uchunguzi wa kamati ya pili, kama tulivyopinga matokeo ya uchunguzi wa kamati ya kwanza.

Tumeomba nakala ya ripoti ya kwanza ya uchunguzi ili kujaribu kuelewa jinsi walivyofikia matokeo yao, lakini kwa bahati mbaya, bado hatujafanikiwa kuona ripoti hiyo. Pia tumeomba kupata nakala ya ripoti ya kamati ya pili ili tuweze kuelewa matokeo yaliyo tangazwa jana, huku tukitarajia serikali itatupatia nakala za ripoti hizi. Tumeomba ukaguzi huru wa makinikia ili kuweza kuondoa dhana iliyojengeka kuwa tunaiba, wakati hatujashiriki katika wizi wowote; ombi hili bado halijatekelezwa.

Kwa mwenendo wa shughuli ya jana na ripoti katika vyombo vya habari leo, imedhihirika kwamba tunaonekana kama siyo wazalendo, huku tukiiba madini ya watanzania kwa mikataba mibovu. Hii si kweli, sisi ni mashujaa wa uchimbaji madini Tanzania. Miaka ya hivi karibuni tumefanya mabadiliko ya hiari katika mikataba iliyotiliwa sahihi miaka ya nyuma ili kuhakikisha faida zaidi inawafikia watanzania, hata kabla ya wawekezaji waliolipia gharama za migodi hii kujengwa, hawajalipwa gharama zao za uwekezaji.

Tumekuwa tukilipa kodi kabla ya muda, huku tukiongeza viwango vya tozo za mrahaba, na tozo za ushuru wa huduma na kuwekeza zaidi katika jamii zinazotuzunguka, kuliko makampuni yote ya madini yakijumuishwa. Tuna watanzania wengi katika nafasi za juu ndani ya kampuni zetu, huku zaidi ya asilimia 96 ya wafanyakazi katika migodi yetu ni watanzania. Watumishi hawa wamepatiwa mafunzo ya hali ya juu na kuendelezwa kwa miaka mingi, huku tukiwa tumewezesha wataalamu wanaoongoza katika fani mbalimbali hapa nchini.

Ilivyo sasa, matokeo yasiyo sahihi yaliyochukuliwa kutoka katika sampuli zilizochaguliwa kutoka makontena 44 kati ya maelfu yanatumika kuharibu sifa ya mwekezaji mkubwa wa kimataifa, ambaye pia ni moja ya waajiri wakubwa katika sekta binafsi na mmoja ya walipa kodi wakubwa nchini.

Tumewekeza zaidi ya Dola za Kimarekani bilioni 4 (TSH 8.8 trilioni) katika nchi hii katika ujenzi na uendelezaji wa migodi yetu, huku tukitumia zaidi ya Dola za Kimarekani bilioni 3 (TSH 6.6 trilioni) kwa wafanyabiashara wa kitanzania kusaidia kuendesha biashara yetu na kulipa zaidi ya Dola za Kimarekani bilioni 1 (TSH 2.2 trilioni) kulipia kodi na mrabaha.

Sisi ni washirika wa muda mrefu wa Tanzania na tumekuwa tukifuata sheria. Tuna amini tuna nafasi ya kushirikiana na serikali katika kufika lengo moja la kuwezesha watanzania kufikia malengo ya maendeleo. Tutaendelea kutafuta muafaka kupitia mazungumzo na serikali.

Kama haitawekezana, itakuwa ishara mbaya kwa wawekezaji waliopo sasa na wanaotazamia kuwekeza nchini. Naamini ukweli utatawala na nitaendelea kujaribu kufanikisha hilo. Mpaka hatua hiyo, naomba muendelee kustahimili na kuwa salama.

Brad Gordon.
Tanzania tunaongea na mfuga Mbwa sio Mbwa,Mbwa asubiri amri ya kufungwa au kufunguliwa kwenye kamba. Jibu la mwisho litapatikana baada ya mazungumzo na Barrick Gold, sio ninyi Acacia.Ninyi ni wezi kwa kuwa you are mining illegally in Tanzania.Infact you are supposed to be behind bars according to international law.Acheni kuhangaika we do not recognize you.
 
Tanzania tunaongea na mfuga Mbwa sio Mbwa,Mbwa asubiri amri ya kufungwa au kufunguliwa kwenye kamba. Jibu la mwisho litapatikana Barrick Gold, sio Acacia.Waache kuhangaika.
Safi sana acacial kuna jambo walikua wanalificha,wao si waturie tu.hivi boss wao mkubwa si bado yupo?
 
Imetoa msimamo gani???? Acheni kupotosha walishasema mazungumzo bado na hakuna waliposema wamekubali ripoti za tume!!!!

Anyway kuna kitu sielewi hivi kma makinikia yalizalisha trilion 100 je matofali ya dhahabu yatatoa shingapi?? Wewe kma wwe unaamini dues zinafika trilion 100????

Pia unaposema waliiba labda nikuulize TMAA na Usalama wa taifa walikuwa hawajui?? Kma walijua iweje miaka yote waliiba huku taatifa za TRA na TMAA zikionyesha data zake hazitofautiani na walichonacho acacia???? Huoni kma ssi watu weusi ndio tuliwapa mwanya wa kuiba maana siamini kma wanaweza kuiba bila ssi kujua!!!
Hivi kwa akili yako, nyumbani kwako ukiwa na walinzi na mbwa wakali unadhani huwezi kuibiwa? Eti kwa sababu tuna TRA na TMAA basi madini yetu hayawezi kuibiwa. This is a very shallow way of using your mind.

Halafu sijasema kuwa hiyo trillion 100 ni thamani ya makinikia. Nimesema ni thamani ya dhahabu iliyoko eneo hilo la Bulyanhuru, be it in makinikia form or other forms.
 
Kwani acacia na Barick ni nani mwenye hsa nyingi na km hmhuski bis wa barik amefuata nn Hpa na kma mnaonewa mbona hamuendi kufungua kesi Mahakamani kupinga uwonevi mnaofanyiwa km ni mtqji wenu itakuwa mmesharudisha na faida mmepta tangia mlikoanza kuchimba Madini bac ondokeni tu tuachieni hyo mashimi ytu
 
Mzungu sio mjinga amechimba kwa mikataba hawezi kulipa hizo hela hata siku moja. Mwisho wa siku tutaambiwa kalipa ili tu kulimaliza hili kama tulivoambiwa Zanzibar wameanza kulipa umeme wakati hicho kitu hakipo hivo
 
Hivi kwa akili yako, nyumbani kwako ukiwa na walinzi na mbwa wakali unadhani huwezi kuibiwa? Eti kwa sababu tuna TRA na TMAA basi madini yetu hayawezi kuibiwa. This is a very shallow way of using your mind.

Halafu sijasema kuwa hiyo trillion 100 ni thamani ya makinikia. Nimesema ni thamani ya dhahabu iliyoko eneo hilo la Bulyanhuru, be it in makinikia form or other forms.
Hahhahhha thamani ya dhahabu au Usoro alisema ni income tax tunayodai??? Mbona reasoning yako haiendani na ID yako?? Hivi kweli income tax ni trilion 100 ?? Ina maana jamaa wametengeneza faida ya trilion 300 kwenye dhahabu walizoiba leave alone walizosafirisha kihalali??? Ina maana kma faida ni trilion 300+ je mauzo yatakuwa shingapi?? Trilion 500 ama??? Hhhahahahha kweli usoro kawaingiza chaka sasa si ungekuwa mgodi mkubwa zaidi duniani???

Anyway nachosema ni kwamba hoja ya kuwa ACACIA wameiba haina mantiki kma hamkubali kuwa TMAA na TRA na usalama wa taifa walirihusu hilo litokee maana wao wanakagua wanashindwaje kujua tunaibiwa?? Ina maana wao wanafaidika pia na huo wizi?? Kibaya zaidi ushahidi wa kuhonga hamna na in turn jamaa wana certified copy za ukaguzi wa makontena by serikali hivo hatutaambulia trilion hizo 100 dah ila nyie ccm natamani wote mswekwe ndani na huyo dikteta wenu mnyooke maana mnafanya ushenzi unaokuja kutucost huko mbeleni

Shame on u
 
Ndiyo maana Kikwete yupo Canada kwa sasa kujadiliana na hawa jamaa namna ya kuepuka kulipa serikali na kuwafundisha maujanja ya kuishinda serikali ya Tanzania. Kwa kweli Magufuli anafanya madhambi kutowakamata kina Mkapa na Kikwete kwani hawa ndiyo wahusika wakubwa wa huu wizi wote. Mdogo hawezi kuibia taifa bila mwenye nchi kujuwa. Kikwete yuko Canada kisirisiri toka majuzi kujadiliana na ACACIA ili wasihusishwe/kutajwa yeye na Mkapa. Magufuli usifanyie hili suala kiunafki Mungu anakuona.....bado haujatutendea haki watanzania.
 
Kama kweli hawajaiba kwann wanaangaika kutoa ufafanuzi, wasitulie na kusubiri kutoa huo ufafanuzi sehemu husika kama mahakamani au kwenye vikao vya usuruhishi/majadiliano kama vitakuwepo kuliko kuhaha kwa kupayuka payuka mitandaoni? Hii ni dalili tosha kuwa hawana ujasiri na wana kesi ya kujibu.
 
Sawa na fisi anasubiri mkono wa binadamu udondoke audake. Hivi watalipa kwa kuwa wao wajinga au? Mikataba mlisaini au la? Mlisaini mkiwa under some sort of influence?
 
Hayawi, hayawi yamekuwa.....hatimaye USHUZI umepata mjambaji. Huyo ndiye Professa bhana, hawezi kukubali kulipa kitu kisichokuwepo. Kama atalazimishwa, atavunja mkataba na kuitaka serikali imlipe matrilioni ya shilling mbele ya mahakama ya kimataifa ya usuluhishi wa kibiashara. Na mkae mkijua kwamba ile mahakama huwa haipokei ushahidi wenye mashaka. Hapo ndipo watanzania mtaimba na kusaga meno!
 
Back
Top Bottom