ACACIA watakiwa kutoa trilioni 35 kama kishika Uchumba cha Mazungumzo

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,483
54,853
Heshima kwenu wakuu,

Hakika tuna njaa njaa. Gazeti la mwananchi limeandika, Baadhi ya wabunge waitaka Acacia ilipe angalau trilioni 35 kama kishika uchumba kabla ya mazungumzo ili kuongeza heshima ya nchi.

Najiuliza kama wasipotoa kishika uchumba wasikae?

Baada ya Kamati ya pili ya kuchunguza madini, mwenyekiti ya Barrick Gold alifika nchini kuonana na rais Magufuli.

Baada ya kuonana naye alisema kampuni yake ipo tayari kufanya mazungumzo na Serikali ya Tanzania yatakayozingatia maslahi ya pande zote mbili ikiwa ni pamoja na kulipa fedha zote ambazo inatakiwa kulipa kwa Serikali ya Tanzania.

Sasa Wabunge wanataka kishika uchumba

======

Dodoma. Sakata la mchanga wa madini katika makontena 277 yanayoshikiliwa bandarini, limeendelea kuwa gumzo ndani na nje ya bunge, huku baadhi wakitaka ripoti zilizotolewa na kamati zote mbili alizounda Rais John Magufuli ziwekwe hadharini li zijadiliwe na wananchi.

Pia wapo wabunge waliotaka Acacia walipe kwanza angalau Sh35 trilioni commitment fee (kishika uchumba)kabla ya mazungumzo ili kuongeza heshima kwa nchi.

Mjadala huo umechagizwa zaidi na ujio wa hivi karibuni wa Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni mama ya Acacia, Barrick Gold, Profesa John Thornton, aliyefika nchini na kufanya mazungumzo na Rais John Magufuli.

Baada ya kikao kilichofanyika Ikulu, taarifa zilieleza kwamba mwenyekiti huyo amekubali kufanya mazungumzo ya kutafuta muafaka ikiwa ni pamoja na kulipa fidia inayostahili.

Akitoa msimamo wa chama jana, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Vincent Mashinji amesema ripoti hizo zinapaswa kutolewa kwa umma ili jadiliwa kwa vile zimeacha maswali mengi yanayokosa majibu.

Mbali ya hilo, pia chama hicho kimependekeza wale wote waliohusika kwa njia yoyote katika upitishwaji wa mikataba mibovu na kulisababishia Taifa hasara wawajibishwe bila kujali nafasi zao wala vyeo walivyokuwa navyo.

Mashinji alisema moja ya eneo ambalo halijawekwa bayana ni kuhusu sampuli zilizochukuliwa, utaratibu uliotumika katika maabara kwenye kupima sampuli husika na njia iliyotumika kufikia hitimisho la kiwango cha dhahabu na madini mengine kwenye mchanga husika.

Alisema eneo hilo limeacha utata mwingi kwa vile takwimu zilizotolewa na tume zinaonyesha kuwepo kiwango kikubwa cha dhahabu wakati takwimu za wamiliki wa migodi pamoja na wakala wa serikali wa madini (TMAA) zikionyesha kiwango cha madini kwenye mchanga huo ni kidogo.

Alihoji iwapo kama kamati iligundua makanikia hayo yalikuwa na thamani ya Sh trilioni 108 mbona haijaelezwa kiwango cha dhamani ya fedha kilichopatikana tangu uchimbaji wa dhahabu uanze mwaka 1998.

“Iwapo takwimu hizo ni sahihi hivi dhahabu ambayo tumeshauza kama Taifa tangu mwaka 1998 ina thamani kiasi gani na sisi kama Taifa tumepata kiasi gani,” alihoji.

Alidai kuwa iwapo Tanzania inataka kunufaika na rasilimali zake na kushinda vita vya kutetea utajiri wake inapaswa kwanza kurejesha katiba iliyopendekezwa na Jaji Joseph Warioba na wala siyo vinginevyo.

Mjadala huo bado umeendelea kulitigisha bunge jana ambapo Mbunge wa Kiteto, Emmanuel Papian alitoa sharti ambalo anataka lizingatiwe kabla mazungumzo hayo hayajafanyika.

“Kabla mazungumzo hayajaanza, Acacia walipe kwanza walau Sh35 trilioni kama (kishika uchumba) commitment fee. Hii itaongeza heshima kwa nchi yetu.”alisema

Kampuni ya Barrick ya Canada ndiyo kampuni mama ya Acacia inayosimamia migodi ya Bulyanhulu, Buzwagi na North Mara hivyo kuifanya kuwa mchimbaji mkubwa wa dhahabu nchini.

Mbunge wa Msalala, Ezekiel Maige alisema Serikali inapaswa kuhakikisha inaimarisha mapato yake kwa kuweka misingi imara itakayowashirikisha wananchi. Katika kufanya hivyo, aliipa kipaumbele sekta ya madini ambayo alieleza kwamba ina fursa nyingi zinazoweza kuwanufaisha wananchi pia.

Akihusisha hoja yake na marufuku ya usafirishaji wa mchanga wa madini, alisema baada ya hatua za awali kuonyesha mafanikio sasa mtambo wa kuchenjua madini utajengwa nchini kama ambavyo Profesa Thornton amesema baada ya kikao chake na Rais Magufuli.

“Tunaomba (Mtambo wa kuchenjua madini) smelter ijengwe maeneo ambako Bulyanhulu. Tuambieni ardhi kiasi gani inahitajika ili tuanze kufanya maandalizi. Sitarajii smelter itajengwa sehemu nyingine zaidi ya Kahama,” alisema Maige.

Alifafanua kwamba hatua hiyo itaongeza tija kwa wananchi wanaozunguka maeneo ya miradi husika. Akiwasilisha ujumbe wa wananchi wake alisema wanataka masuala yao yazingatiwe kwenye mazungumzo hayo ya kutafuta muafaka.

Wapinzani kwa upande wao hawakupinga vita vilivyoanzishwa na Serikali lakini walitahadharisha kwamba ushirikiano wa Watanzania wote unahitajika kuvishinda kwa mafanikio badala ya kutanguliza maslahi ya vyama.

Mbunge wa
 
Watanzania tufanye kazi. Pesa za bure Dunia hii hazipo. Kama kuna stahili yetu, ufanyike utafiti. Ikithibitika haki yetu ni trillion 100 tulipwe, kama ni trillion 1 tulipwe, kama ni million 1 tulipwe, kama hakuna tunachostahili kulipwa, pia tuukubali ukweli.
 
Yaani pesa wale viongozi wa Ccm kwa njaa na uroho wao halafu Acacia wabebe mzigo wote?Hakuna kitu kama hicho, hili litapita kama lilivyopita la Bashite!
Rais hapati chochote hapo maana hata kamati yenyewe imefanya kazi kwa kujipendekeza pendekeza na kukomoana.Magu kama ana uchungu ni nchi alete mikataba ya bara bara,uuzaji wa nyumba, vyeti vya Bashite nk.Akimaliza hapo ndio twende kwenye madini ambayo chama chake kilipitisha mikataba yote.Asitutafutie migogoro ya watu ambao chama chake iliwapa maeneo ya kuchimba kwa mbwe mbwe nyingi.
 
Sijui wabunge wa CCM wanakuwa na dawa gani hadi wanachaguliwa huko majimboni mwao mara kwa mara? Wao ndiyo waliosababisha "wezi wanaume" watuibie na leo wanataka hao wezi watoe kishika uchumba ili wafanye nao mazungumzo, hivi hawa zimetimia kweli?

Hadi sisi wanaume tunadai kishika uchumba? Waache upuuzi wao hakuna Mtanzania anayetaka kuolewa na hao wezi wao wa Kizungu!!
 
Watanzania tufanye kazi. Pesa za bure Dunia hii hazipo. Kama kuna stahili yetu, ufanyike utafiti. Ikithibitika hali yetu ni trillion 100 tulipwe, kama trillion 1 tulipwe, kama ni million 1 tulipwe, kama hakuna tunachostahili kulipwa, pia tuukubali ukweli.
Haswa,pesa za bure dunia hii hakuna.....

Hao jamaa sio kama akina bakhresa,lake oil na wengine tuliowatishatisha na kuwabambika makodi,

Ilani ya ccm haitekelezeki akiwa ni pamoja na ujenzi wa reli,sasa tumeamua ku-blackmail makampuni tupate hela za kutekeleza bajeti

Maisha ya ujanja ujanja na kupiga dili rahisi hayapo dunia hii
 
Wazungu hawajawa vilaza kiasi hicho wakati treaties CCM mlizisainia mahotelini wenyewe
Sidhani kama kuna clause inayoruhusu gross misdeclaration of quantities. Ningekuwa mimi ningepambana nao kwenye customs law, criminal law, mining law na sheria nyingine yoyote ambayo wamekiuka. Bado naamini JPM amewahurumia.
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom