Acacia wakitulipa matrilioni yetu napendekeza tulipe deni la taifa kwanza

Wandugu mimi nimechoka kila siku tunafedheheshwa na hesabu ya deni la taifa. Mara utasikia kila mtanzania anadaiwa laki nane.

Sasa mimi naona endapo ikithibitishwa Acacia kutulipa yale matrioni tuliyoambiwa na mkuu naona tumalize deni la taifa kwanza tubaki na uhuru tupumue.
Mimi nataka NOAH yangu, madeni si huwa yapo tu? Tutalipa tu!
 
KJ kaenda kuweka mambo sawa.......Siyo ajabu kama watalipa 5tr.
Kitakachowafanya walipe hizo trilioni 5 ni ni nini? maana hata assets zao hapa bongo hazifikii hizo hela , nachoona ni mgodi kufungwa tu..
 
Tulipwe tu hata Trilioni 50 tu za Tanzania inatosha kabisa, kwanza, Tujenge SGR nchi nzima hadi kigoma, ni kama Trilioni 15 HIVI Za Tanzania.

Fedha zingine, Tuwekeze kwenye UMEME, Ikiwemo mabwawa ya maji kwa ajili ya kuzalisha umeme wa kutosha hasa Mega watt 10000 Hapa ni kama Trilioni 8. Zinamaliza kabisa tatizo la umeme nchini

Fedha zingine, kilimo cha umwagiliaji nchi nzima, miundombinu ya umwagiliaji ijengwe kila wilaya na sheria itungwe kusimamia hili swala na kila wilaya ijenge GHALA lake la kuhifadhia Chakula, mazao ya kibiashara nayo yalimwe kila wilaya, hapa ni Trilioni 2 tu.

Zingine, Barabara zote zinazounganisha mikoa na mikoa ziishe kabisa, na zile za wilaya kwa wilaya nazo ziishe kwa kiwango cha lami, zile za vijijini zinazounganisha na wilaya zijengwe kisasa hata kama si kwa lami, hapa ni Trilioni 3.

zingine, kila kanda ijengwe hospitali ya kisasa kama ile ya mloganzila ikiwa na huduma zote na vifaa vyote muhimu. hapa ni Trilioni 1.5 tu.

Zingine, shule zote za msingi zenye majengo ya zamani zibomolewe zijengwe upya, na kila shule ya msingi iwe na vyumba 15 vipya vyenye madawati, vitabu na kila shule iwe na maktaba, maabara, nyumba za walimu nk. sheria itungwe kabisa, shule za sekondari hivo hivo.

Zinazobaki, tulipe deni tu sasa.
kitakachowafanya walipe hizo hela ni nini? maana assets zao hapa bongo hazifikii thamani hiyo, wakiona mnawadai hela nyingi wanaaawchia mgodi wenu.. pengine watakuja na mgongo wa wawekezaji wengine kuingia contract mpya
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom