Acacia wakitulipa matrilioni yetu napendekeza tulipe deni la taifa kwanza

cacacuona

JF-Expert Member
Feb 24, 2017
661
1,000
Wandugu mimi nimechoka kila siku tunafedheheshwa na hesabu ya deni la taifa. Mara utasikia kila mtanzania anadaiwa laki nane.

Sasa mimi naona endapo ikithibitishwa Acacia kutulipa yale matrioni tuliyoambiwa na mkuu naona tumalize deni la taifa kwanza tubaki na uhuru tupumue.
 

brazoo

JF-Expert Member
Sep 28, 2014
708
500
Tufanye investment Kubwa Kama za kilimo cha kumwagilia kila sehem zenye mito na maziwa, tujenge mabarabara ya lami kuingia mashambani, kwenye mbuga zetu za utalii, tuhakikishe maji yanapatikana ya kitosha kila kijiji, umeme upo wa uhakika, secta ya afya na elimu pia,return yake ndio tuanze kulipa deni ila baadhi ya secta return yake huwezi iona ila inamchango mkubwa sana
 

Brigedia Chan-ocha

JF-Expert Member
Mar 7, 2014
1,211
2,000
Tulipwe tu hata Trilioni 50 tu za Tanzania inatosha kabisa, kwanza, Tujenge SGR nchi nzima hadi kigoma, ni kama Trilioni 15 HIVI Za Tanzania.

Fedha zingine, Tuwekeze kwenye UMEME, Ikiwemo mabwawa ya maji kwa ajili ya kuzalisha umeme wa kutosha hasa Mega watt 10000 Hapa ni kama Trilioni 8. Zinamaliza kabisa tatizo la umeme nchini

Fedha zingine, kilimo cha umwagiliaji nchi nzima, miundombinu ya umwagiliaji ijengwe kila wilaya na sheria itungwe kusimamia hili swala na kila wilaya ijenge GHALA lake la kuhifadhia Chakula, mazao ya kibiashara nayo yalimwe kila wilaya, hapa ni Trilioni 2 tu.

Zingine, Barabara zote zinazounganisha mikoa na mikoa ziishe kabisa, na zile za wilaya kwa wilaya nazo ziishe kwa kiwango cha lami, zile za vijijini zinazounganisha na wilaya zijengwe kisasa hata kama si kwa lami, hapa ni Trilioni 3.

zingine, kila kanda ijengwe hospitali ya kisasa kama ile ya mloganzila ikiwa na huduma zote na vifaa vyote muhimu. hapa ni Trilioni 1.5 tu.

Zingine, shule zote za msingi zenye majengo ya zamani zibomolewe zijengwe upya, na kila shule ya msingi iwe na vyumba 15 vipya vyenye madawati, vitabu na kila shule iwe na maktaba, maabara, nyumba za walimu nk. sheria itungwe kabisa, shule za sekondari hivo hivo.

Zinazobaki, tulipe deni tu sasa.
 

mindpower

JF-Expert Member
Oct 1, 2016
1,055
2,000
Mm nishaanza kutengengeza parking ya Noah!
Den la nn watalpa hata vitukuu vyetu
 

sultanrama

Member
Jul 11, 2015
87
125
Naona mnapanga matumizi kabla pesa hewa haijaingia,hongereni mimi hata buku poa tu,maana sijawahi kupata mgao kutoka huko.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom