ACACIA: Tutafunga mgodi kama hakutakuwa na makubaliano hadi kufikia Septemba

mwasu

JF-Expert Member
Jul 13, 2011
10,184
2,000
Mbona hii vita kama ya majogoo?1 Kila mtu anaparua chini tu hakuna anaemwamia mwingine njoo kesho tuzungumze, mzee kule kigoma kasema wasipoamua kuyazungumza mapema anafunga mgodi, ACCACI ( ambayo ni kampuni hewa) inasema wasipotaka tulizungumze mapema nafunga mgodi, haaaa hii ni nini sasa kwa nini hakuna anaepata siku ya kukutana waongee?! Maajabu nchi hii ni zaidi ya simba kunyonyesha mtoto wa chui..
 

MAPUMA MIYOGA

JF-Expert Member
Jan 30, 2013
3,771
2,000
Tanzania tanzania matatizo na uongo uongo hautufikishi popote! Wengi hatuna facts bali tunafanyia kazi hearsay!
 

Kimweri

JF-Expert Member
Apr 16, 2008
3,999
2,000
Mnaosubiri kampuni yenye thamani ya bilioni 1 ilipe bilioni 50 mkapimwe akili kwa mkemia mkuu.
 

August

JF-Expert Member
Jun 18, 2007
7,426
2,000
Pamoja na kuyasema hayo, Mkurugenzi wa ACACIA, Brad Gordon amesisitiza kuwa majadiliano ya Barrick Gold na Serikali ya Tanzania yatawashangaza wengi kwa sababu ana matumaini makubwa pande zote mbili zitakubaliana kutokana na ukweli kuwa kila upande una mengi ya kupoteza kama hawatakubaliana kwa kupitia meza ya majadiliano.

Hata hivyo anasikitika kwa kampuni yake ya ACACIA kuachwa kuingizwa kwenye mazungumzo na anadai kama pande mbili zitakuwa hazijakubaliana kufikia septemba inawabidi wafunge mgodi na kusubiri hatma ya majadiliano ili kupunguza mrundikano wa makanikia na gharama za utunzaji.
kwenye taarifa sahihi ni hapa hizo zingine za kufunga au kutaka kufunga ni hadithi za kufikiria..
 

rodrick alexander

JF-Expert Member
Feb 12, 2012
10,874
2,000
wamesema majadiliano yatawashangaza wengi na kila upande unaweza kufaidika au kupoteza, tunaweza tusipate tilioni 108 zilizoelezwa lakini dalili zinaonyesha kuna kitu tutapata cha muhimu kila upande unapoingia kwenye majadiliano watambue kitu hicho
 

Lu-ma-ga

JF-Expert Member
Sep 21, 2010
4,608
2,000
Pamoja na kuyasema hayo, Mkurugenzi wa ACACIA, Brad Gordon amesisitiza kuwa majadiliano ya Barrick Gold na Serikali ya Tanzania yatawashangaza wengi kwa sababu ana matumaini makubwa pande zote mbili zitakubaliana kutokana na ukweli kuwa kila upande una mengi ya kupoteza kama hawatakubaliana kwa kupitia meza ya majadiliano.

Hata hivyo anasikitika kwa kampuni yake ya ACACIA kuachwa kuingizwa kwenye mazungumzo na anadai kama pande mbili zitakuwa hazijakubaliana kufikia septemba inawabidi wafunge mgodi na kusubiri hatma ya majadiliano ili kupunguza mrundikano wa makanikia na gharama za utunzaji.

Ieleweke kuwa majadiliano yatahusu Barrick Gold na Serikali ya Tanzania kwa sababu Barrick Gold ndiye mwenye hisa nyingi.

Matokeo ya Ijumaa yameonyesha kuwa mapato kwa miezi sita yameshuka mpaka $176 milioni kutoka $318 mwanzoni mwa mwaka kwa sababu hawawezi kuuza makanikia yenye ounces 127,000 za dhahabu na unga.

Kwa muda wa miezi sita mpaka Juni, mapato yameshuka kwa asilimia 22 na kuwa $391.7 milioni wakati faida kabla ya kodi ilishuka kwa asilimia 2 na kuwa $99.5 milioni.

Hisa zimeendelea kudondoka na kuanzia Machi hisa za ACACIA zimedondoka kwa asilimia 50 na bei ya kampuni kwa sasa iko chini ya £1 bilioni.

Kwa wale mnaojua kiingereza mnaweza kusoma zaidi;

Source: Financial Times Newspaper.

Hawana ubavu wa kufunga wale, wanataarifa zote kuwa deposits of gold mineral is still abundant in Tanzania, wanajua kuwa Tanzania bado Ina madani kibao kati ya nchi cha he kabisa duniani, wataenda wapi??? Fidia yetu watailipa na wataendelea kuchimba na kujenga mahusiano mapya kwa future yao.JPM kawashika pabaya na bado kawapo onyo in case of any delay to commence negotiation
 

Danny Jully

JF-Expert Member
Jul 29, 2013
4,420
2,000
Aiseee haya bana hivi si walisema mazungumzo yanaanza sijui kesho kutwa... kumbe hiyo kesho kutwa haijafika hadi leo
Mkuu kama tuliambiwa kwamba wamekubali kulipa, kumbe walikubali kukaa kwenye meza ya mazungumzo, sasa hapo unategemea sarakasi zitaisha? Baada ya mkwara wa kuwatimua usishangae tukaambiwa tena hawatatimuliwa kwa sababu walienda kuomba msamaha. Na kwa kuwa sisi ni watu wastaarabu sana hasa kwa hawa wezi wa kizungu basi tumeamua tu kuwasamehe.
 

Hute

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,545
2,000
kama hisa zimedorora, ni kutokana na jeuri yao, wangekuwa na adabu zisingedorora. wajue kuwa hapa kuna nchi wao wapo chini hawajaja tz kufanya biashara halafu watupande mabegani kwasababu tu sisi ni waafrica. wakifunga migodi yao, wafungue na mavyuma yao yooote ili kwenye migodi yao turuhusu wachimbaji wadogowadogo wakatifue wenyewe au waungane pamoja au tuite wawekezaji wengine etc. acacia wana kiburi na hawatakiwi kuendelea kuwekeza tz.
 

mzushi

JF-Expert Member
Mar 9, 2012
3,094
2,000
kulu alisema jana wakichelewa kuja kwenye mazungumzo tutafunga mgodi. acacia nae jana hiyo walisema september bila makubaliano tunafunga mgodi. sasa ngoma inanoga hapa. watuachie tu madini yetu hamna namna
Mkuu waache madini au mashimo
 

kipara kipya

JF-Expert Member
May 2, 2016
10,364
2,000
Wafunge tu wakati walikua wakizalisha sikufaidika waliofaidika nao ni wale waliokuwa bungeni wanapata posho na bado wayanatetea hayo majizi!
 

mysterio

JF-Expert Member
Sep 9, 2011
6,395
2,000
Kinachoonekana ni kama utoto sasa. Kampuni ina mapato zaidi ya mara kumi ya mapato ya serikali? Common sense inakataa
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom