ACACIA: Tumekula hasara bilioni 40 kwa wiki mbili baada ya kuzuia kupeleka mchanga nje. Tutawafidia?

iparamasa

JF-Expert Member
Nov 14, 2013
13,437
14,924
Kampuni ya Acacia imedai kula hasara ya bilioni 40(dola milioni 17 baada ya mkataba wake wa kupeleka mchanga nje kuvunjwa.

Wamesema wanaangalia "options" zote zilizo upande wao,nadhani la kwenda mahakamani kudai fidia pia liko mezani

Wiki mbili bilioni 40,je mgogoro huu ukimaliza mwaka au miaka miwili itakuwa pesa ngapi na riba na magharama ya usumbufu? Atalipa nani,kwa kuzitoa wapi?

Bado kuna symbion power,mgodi wa dutwa...........

Tusubiri tuone filamu hii
IMG-20170317-WA0000.jpg
 
Kwa maana hiyo ni wastani wa 20bn/- kwa wiki. Maana yake ni kwamba kwa mwaka ni 20bn x 52 = 1040bn/=. Kwa miaka mitano ni 1020bn x 5 = 5.2 tr./= ambapo watafungua kesi kudai fidia ya kuvunja mkataba. Kwa mwendo huu kuna siku hii nchi itafilisika rasmi. Hope mkataba uko vizuri in favor of the public interest na sio kama ile ya IPTL, Symbion, et. al.
 
Siri imebumbuluka DK ya 2 tu ya mchezo.....

Kumbe mnavuna sana, sasa tumejua kuwa mlikuwa mnapiga Kiasi gan kila siku,
maana kila mlipoulizwa kwa uwaz mlidai Yale ni masalia tu na mavumbi vumbi hayana dili kuuuubwa na yanawatia hasara kubwa sana kuyasafirisha, kumbe janja ya nyani tu ,

mkibanwa mnaachia data zote wazi wazi, na sisi tushapata majibu ya maswali waliyokuwa wakishuku wananchi na hii serikali sikivu.

Mlikuwa mnajifanya "sizitaki hizi mbichi" kumbe mnajua ila mnaficha tu kiasi cha mabilioni mnayopata, sasa hiyo ni dozi tu ya wiki mbili tayari 40 billion, je tukiwapigia kwa miaka yote mliyokaa, si ndio mtazimia kabisa kwa mshangao wa ukwasi mtaotakiwa kitu rejeshea. Ipendeni nchi yenu kama mnavyopenda faida mnayopata , na vile vile chukieni wizi wa maliasili za serikali kama mnavyoogopa hasara mnayopata baada ya dili kubuma.
Asante Rais Magufuli kwa mbinu zako. Hii ndio serikali tunayoitaka sasa .
 
Kwa maana hiyo ni wastani wa 20bn/- kwa wiki. Maana yake ni kwamba kwa mwaka ni 20bn x 52 = 1040bn/=. Kwa miaka mitano ni 1020bn x 5 = 5.2 tr./= ambapo watafungua kesi kudai fidia ya kuvunja mkataba. Kwa mwendo huu kuna siku hii nchi itafilisika rasmi.
Kwa pesa hizo ulizoorodhesha walikuwa wanarudisha kiasi gani kwa wenye madini ambao ni watanzania?
 
Back
Top Bottom