ACACIA njia panda, yahaha kuficha ukweli wa uendeshaji wake

Maramla

JF-Expert Member
Jan 8, 2014
581
642
*Acacia Njia Panda, Yahaha Kuficha Ukweli wa Uendeshaji Wake*

Uchunguzi wa hivi karibuni unaeleza kuwa Bodi ya Wakurugenzi wa kampuni ya Acacia nchini Uingereza wamekuwa wakihangaika huku na kule kujaribu kuwahakikishia wanahisa kwamba kampuni hiyo ipo imara na yenye mwelekeo wa ustawi.

Gazeti hili limepata nyaraka zinazoonesha kuwa ujumbe ambao usambazwa na kujirudia mara kwa mara katika ripoti za Acacia ni kwamba hazina ya madini katika mgodi wa dhahabu ambao kampuni hiyo inachimba Tanzania bado ni kubwa na kwamba uongozi umehakikisha kuendelea na uchimbaji na uzalishaji wa dhahabu katika mgodi huo. Hata hivyo mengi hayasemwi.

Kwa mujibu wa vyanzo vyetu vilivyopo London, wakati suala la utawala bora na uhusiano mzuri umekuwa ndio msingi wa kujiendesha kwa faida nchini Tanzania, Bodi ya Acacia ilitakiwa kujua ukweli halisi kuhusu mustakabali wa Acacia nchini Tanzania.

Kwa mujibu wa vyanzo vya kuaminika jijini Londani, Uingereza, vinathibitisha kwamba Bodi ya Wakurugenzi, kwa taarifa hizo za utendaji za Acacia, inataka kuonesha kuwa sasa ina uwezo wa kukaidi hata baadhi ya makubaliano ya Serikali ya Tanzania na Barrick Gold.

“Kuwahakikishia wanahisa juu ya ulinzi wa maslahi yao, Bodi ya Wakurugenzi ya Acacia imepuuza hatua zilizochukuliwa na Kampuni Mama ya Barick Gold ambayo inataka kumaliza mgogoro kwa njia ya mazungumzo, mgogoro ambao ulisababishwa na Acacia kukiuka Sheria, Sera na Mamlaka za nchini Tanzania,” anasema mpashaji mmoja ndani ya Acacia.

Hata hivyo, kinyume na tashwira wanayoionesha mbele ya Bodi ya Wakurugenzi huko Uingereza, baadhi ya taasisi za umma na makampuni binafsi yenye utaalam na masuala ya uchimbaji madini yameweka wazi kwamba kampuni ya Acacia inatafuta uhalai baada ya kuchafuka.

“Mazunguzo kati ya Barrick na Serikali ya Tanzania yalicheleweshwa na kusimama kwa karibu miezi nane. Wakati Serikali ya Tanzania ikifikiria kusitisha mazungumzo moja kwa moja, Barrick na Rondgold ziliungana na kuleta ari mpya ya kuendelea na mazungumzo kumaliza utata,” anasema Mtaalam wa Madini aliyebobea katika hatua za majadiliano.

*Acacia Wajhaha Kuficha Ukweli*

Inaonekana suala la kuficha ukweli limeendelea kufanywa na Bodi ya Wakurugenzi wa Acacia kwa kiwango cha kukithiri. Ni wakati wa kuchunguza kupata ukweli zaidi sasa.

Kwanza ni kujua kama hali ya Acacia ipo sawa katika uchimbaji madini nchini Tanzania?

Bahati mbaya Bodi ya Acacia haioneshi kujali au kutaka kujua picha halisi ya kampuni hiyo katika uchimbaji madini nchini na haioneshi kujua kuwa bila ushirikianao na Serikali nchini Tanzania hakuna Acacia.

Gharama zinazidi kuwa juu na muda mfupi ujao itashindwa kujiendesha.

Bodi pia inaelezwa haifahamu kuwa Acacia imelimbikiza kodi kubwa na kupitia hukumu ya mahakama ambayo imeishatanganzwa na inasubiri utekelezaji wake muda wowote pale mazungumzo kati ya Barrick/Randgold yatakapokwama.

Bila ushirikiano kwa Serikali ya Tanzania Acacia haiwezi kufika popote, anasema mtaalamu huyo. Kwa zaidi ya miaka miwili iliyopita baadhi ya maeneo ya uchimbaji yenye faida yalisimamishwa kwa ajili ya matengenezo.

Bodi ya Acacia haiweki wazi gharama halisi za kuufungua upya mgodi wa Bulyanhulu. Mgodi wa North Mara upo katika hatari ya kufungwa kutokana na kukiuka Sheria za Mazingira.

Ripoti za uchafuzi mkubwa wa mazingira na madhara ya sumu inayotokana na shughuli za uchimbaji madini katika mgodi huo huziathiri jamii zilizo jirani, unazilazimu Mamlaka za Uthibiti kuufunga mgodi huo.

Mahitaji ya kurekebisha mifumo ya mazingira ni makubwa kuifanya Acacia kumudu kuendelea na uchimbaji nchini Tanzania.
Inaelezwa kuwa matokeo ya hatua za Mamlaka za Udhititi zimeidhoofisha kwa kiwango kikubwa na pengine kuondoa thamani ya Acacisa kuchimba madini.

Pili ni kuchunguza kama Acacia inaweza kuendelea kuchimba madini nchini Tanzania.

Bodi ya Wakurugenzi ya Acacia imekuwa na dharau na kiburi dhidi ya Serikali ya Tanzania kufikia kiwango cha, kwa mujibu wa vyanzo vya kuaminika, Serikali imeapa kwamba ili Acacia iendelee kuchimba madini nchini lazima kampuni hiyo isitishe kabisa shughuli zake na kuanza upya kwa utaratibu utakaokubalika.

Wakati Barrick imefanya mazungumzo na kukubaliana utaratibu kulinda maslahi ya Acacia, Bodi ya Acacia inasemekana imetingwa na kampeni mbaya dhidi ya Serikali ya Tanzania na kuielezea kama Serikali isiyovumilika katika dunia ya waliostaarabika. Hii haitawasaidia. Hawajui tu.

Bodi ya Acacia inatamani Serikali iliyopo madarakani iondolewe ili tu kulinda maslahi ya wanahisa wake. Hii ni hatua mbaya sana ya uhusiano wowote na Serikali inayokuhifadhi.

Kinachooneka ni kuvunjika kwa wazi kwa uhusiano baina ya Acacia na Serikali.

Serikali ya Tanzania inaeleweka kwa kuweka wazi kwamba hakutakuwa na majadiliano na Acacia. Bodi ya Acacia inatumia mbinu zisizo kubalika kujipenyeza kwa Serikali, labda kutaka kuonesha jinsi Serikali inavyokosea namna ya kushughulikia mgogoro huo, anaeleza mtaalam wa mahusiano ya Serikali na wadau wa madini.

Jaribio ni kushawishi Serikali kwamba inaweza kuingia gharama kubwa kama Acacia haitaruhusiwa kuendelea na uchimbaji wa madini na kwamba matokeo ya usuluhishi yatakuwa na madhara.

“Ni wazi inachokifanya Acacia na kinyume na matarajio, ni kuweka ugumu kwa Serikali ya Tanzania ishindwe kulinda maslahi ya Watanzania dhidi uroho na dharau za Acacia, lakini wanakosea sio kwa utawala huu,” anasema mtaalam wa masuala ya madini.

Swali ni kwamba, Je, Acacia inaweza kufanikiwa na kuendelea na uchimbaji hapa nchini bila kukubali yaliyokubaliwa na kampuni yake Mama kwa Serikali?

Barrick imefanya yote yanayopaswa kufanywa na kwa pamoja na Randgold wanafanya juhudi kuona kampuni inaendelea na uchimbaji hapa Tanzania.

Hivi karibuni, vyanzo vinavyofahamu kuwepo kwa makubalinao, vinathibitisha kwamba Serikali imeombwa kusitisha kwa muda hatua za kuibana Acacia katika kodi kubwa wanayodaiwa.

Serikali imeipa Barrick muda kuainisha vikwazo vyote vinavyotishia kukwamisha mazungumzo kabla haijaufunga mgodi wa North Mara kwa kukiuka sharia za mazingira. Ni wazi kuwa suala hili ni la muda tu kabla mgodi wa North Mara haujaamriwa kusitisha shughuli zake hapa Tanzania.

“Ni bahati mbaya ukweli ambao Bodi ya Wakurugenzi ya Acacia imekuwa ikihangaika kujaribu kuuficha, umejulikana.

Serikali imesisitiza kwamba kuna ushaihidi usiopingika wa ukwepaji mkubwa wa kodi uliofanywa na Acacia,” anaeleza John Mbutta, Mtaalam Mshauri wa masuala ya kodi.

Kuna ushahidi kwamba Acacia imekataa kabisa kufuata masharti ya mkataba wa kuendeleza madini kuhusu kuendesha akaunti za fedha nje ya nchi ambazo kwa kiwango kikubwa zimetumika katika kafanya udanganyifu. Hata hivyo, taratibu dunia imeanza kuielewa Tanzania.

Kuna ushahidi kadhaa pia kuwa Acacia walijaribu kutafuta msaada wa kimataifa dhidi ya Serikali ya Tanzania na kusahau kuweka mazingira mazuri ya majadiliano ndani ya nchi.

Dunia imeanza pia kukubali kwamba kuna uhalali wa kile Serikali ya Tanzania inajaribu kukipata hasa kwa manufaa ya wananchi.

Ujumbe wa wazi uliopo ni kwamba msimamo wa Bodi ya Wakurugenzi ya Acacia unaifanya Acacia isiwe endelevu tena nchini Tanzania. Ni suala la muda tu pale Acacia itakapoanza kumeguka. Walioona mapema hali hii walishaondoka.

Bodi ya Wakurugenzi ya Acacia wanafahamu hali ya kampuni lakini kwa kutumia mbinu ovu wanajaribu kwa nguvu zote kuisifia Acacia ili kufanya bei ya hisa na kuuhadaa umma kuwekeza katika kampuni inayoelekea kufa.

“Tanzania imefungua milango ya biashara lakini kwa vigezo vya usawa. Rais anatekeleza ahadi zake kwa faida ya wananchi. Barrick imeonesha dira na uongozi wenye ari mpya ya kujenga ushirika wa haki. Ni wakati wa kufanya mabadiliko katika sekta ya madini,” anasema Mtaalam wa Madini kutoka Durban, Afrika Kusini.
-Mwisho-

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Mpaka machozi yanatoka jinsi nchi yetu inavyofanywa kama njia ya kushibia
 
Kuna Kobe zinaweza zisikuelewe lkn upo sahihi
Wanasiasa wa upinzani wanapaswa wawe wanasimama na serekali ili kutetea maslahi ya nchi yao na sio kusaidiana na mabeberu

Jiwe alikuwa amejikamatia zake mabeberu lkn Kobe moja ikajifanya inajua saana sheria

All in all sikubaliani na kupigwa risasi kwa wanasiasa Tanzania pia msaliti kinachomstahili ni navichok aise
Inauma sn.tena anapotokea na Tanzania mwenzetu anaamua kutushambulia na kuwa upande wa mabeberu!!!!! INAUMA SN

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using my iPhone using jamiiforum app
 
Kuna Kobe zinaweza zisikuelewe lkn upo sahihi
Wanasiasa wa upinzani wanapaswa wawe wanasimama na serekali ili kutetea maslahi ya nchi yao na sio kusaidiana na mabeberu

Jiwe alikuwa amejikamatia zake mabeberu lkn Kobe moja ikajifanya inajua saana sheria

All in all sikubaliani na kupigwa risasi kwa wanasiasa Tanzania pia msaliti kinachomstahili ni navichok aise

Sent using my iPhone using jamiiforum app
Waliosaini hiyo mikataba mibovu....sukuma ndani...walikuwa wamepewa rushwa na Mabeberu.....
 
Japo habari ni ndefu lkn mleta habari yupo upande mmoja sana wa serikali...wale Acacia walifile case ktk arbitration court London lkn wakasimama kupisha mazungumzo hasa baada ya watendaji wake wakuu kuwekwa ndani kwa kukwepa kodi na money laundering charges...case ambazo zipo kisiasa zaidi...ninaona hujabalance habari...mm nimehighlight ili uibalance...haitusaidii kuficha ukweli ambao hata waziri wa sheria aliukubali...
 
Kuna Kobe zinaweza zisikuelewe lkn upo sahihi
Wanasiasa wa upinzani wanapaswa wawe wanasimama na serekali ili kutetea maslahi ya nchi yao na sio kusaidiana na mabeberu

Jiwe alikuwa amejikamatia zake mabeberu lkn Kobe moja ikajifanya inajua saana sheria

All in all sikubaliani na kupigwa risasi kwa wanasiasa Tanzania pia msaliti kinachomstahili ni navichok aise

Sent using my iPhone using jamiiforum app
Hivi kumbe hizi kobe za upinzani ndio ziliwafukuza wabunge wa ccm bungeni kisha zenyewe zikapitisha sheria mbovu za madini kwa mbwembwe
 
Kwanini kwanza upinzani wakubari kuondoka bungeni?

Si wangegoma humohumo tu
Hivi kumbe hizi kobe za upinzani ndio ziliwafukuza wabunge wa ccm bungeni kisha zenyewe zikapitisha sheria mbovu za madini kwa mbwembwe

Sent using my iPhone using jamiiforum app
 
Ilinipita hii habari. Walipe kodi zetu kwanza. Ujanja ujanja wao kwisha. Mchanga umewaumbua sana. Bado hawajafuatiliwa kiundani wametumia misamaha ya kodi kinyume.
 
Japo habari ni ndefu lkn mleta habari yupo upande mmoja sana wa serikali...wale Acacia walifile case ktk arbitration court London lkn wakasimama kupisha mazungumzo hasa baada ya watendaji wake wakuu kuwekwa ndani kwa kukwepa kodi na money laundering charges...case ambazo zipo kisiasa zaidi...ninaona hujabalance habari...mm nimehighlight ili uibalance...haitusaidii kuficha ukweli ambao hata waziri wa sheria aliukubali...
Unafikiri wasinge minywa naniliu kama hivyo wasingeendelea na hiyo kesi yao huko arbtration court?

Wamejua ukipita huku serikali ya TZ inapita kule alafu mwisho tutajua nani amepata maumivu makali.

Uki piga kulia yenyewe inapiga kushoto.
 
Kuna Kobe zinaweza zisikuelewe lkn upo sahihi
Wanasiasa wa upinzani wanapaswa wawe wanasimama na serekali ili kutetea maslahi ya nchi yao na sio kusaidiana na mabeberu

Jiwe alikuwa amejikamatia zake mabeberu lkn Kobe moja ikajifanya inajua saana sheria

All in all sikubaliani na kupigwa risasi kwa wanasiasa Tanzania pia msaliti kinachomstahili ni navichok aise

Sent using my iPhone using jamiiforum app
Navichok aise ndiyo mdudu gani huyo mkuu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Acacia waache kukwepa kutumia akaunti za bank za hapa nyumbani-Tanzania ,BOT mpo wapi katika kufanikisha hili ili kujuwa kipato chao harisi na halali.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sababu hakuna cha chau chau, ACACIA hawana ujanja...ni kampuni ya kitapeli mno, watatuelewa tu..
 
Back
Top Bottom