ACACIA Mining PLC: We do not agree with President Magufuli Committee's findings...

hatua inayofuata, naomba serikali yangu imekamate huyo mzungu wa acacia na wamrudishe kwao kama yule bosi wa UNDP. halafu hio kampuni ya Acacia waifute tu, wanyanganywe mgodi, watafute mwekezaji mwingine ambaye ni mwaminifu. Halafu na hawa wafanyakazi wa Acacia waanze kutafuta kazi sehemu nyingine tu na ndio muanze kuisoma namba kama sisi tunavyosoma huku mtaani , yaani hawa wafanyakazi wa acacia ni watu wa ajabu sana mnapokea mishahara minono huku madini yetu yanaondoka bure!!!??? foolish.
 
WHY DO I LIKE DUTERTE! RODRIGUEZ DUTERTE NI RAIS WA UFILIPINO! ALIWEZA MWAMBIA RAIS WA MAREKANI BILA WOGA KUWA WE NI MTOTO WA KAHABA NA MIE MWANAUME SIOGOPI! MPAKA ZIARA YA OBAMA KWENDA MANILA IKAHAIRISHWA!

DUTERTE WASHITAKIWA NA WATUHUMIWA WA MADAWA YA KULEVYA HAKUTAKA MJADALA NA MTU WALA MASWALA YA UCHUNGUZI NA MAHAKAMA ALIWAUWA WOTE! ANAUWA MAJAMBAZI WOTE! WALA RUSHWA MPAKA LEO UKIBAINIKA UNAPOTEA!INDONESIA KUNA MAKOSA HATA UFANYEJE RISASI UNAKULA KAMA YA RUSHWA NA MADAWA YA KULEVYA, VIVO IVO CHINA UKIKUTIKANA NA KASHFA TENA YA UHUJUMU UCHUMI NA RUSHWA UNAKULA RISASI! RAISI WA KOREA KASKAZINI ALIAMURU MJOMBA WAKE ALIWE NA MBWA KWA SKENDO YA RUSHWA!

BILA MAAMUZI MAZITO KAMWE NA NEVER WATU HAWATAOGOPA WALA KUJALI! KWANZA MUESHIMIWA RAISI ATOE AMRI MAENEO YOTE NYETI ANZIA SASA PALINDWE NA JWTZ JESHI LA WANANCHI HAWA HATA UMUONGE VP RUSHWA HAPOKEI! JWTZ WALINDE BANDARI!MALIASILI!MADINI!UHAMIAJI!TRA!TRL!AIR PORTS!ETC

VIJIKUNDI AMA VI SECURITY KAMPAN VISIPEWE TENA TENDER ZA ULINZI MAHALI NYETI WALA POLICE! INUNULIE SKANA KUBWA ZA KISASA ALAFU NGOME YA NCHI AMA JWTZ WAPEWE MAMLAKA YA ULINZI, MBONA BANDARI YA KENYA INALINDWA NA JESHI LA KENYA NA PANAKWENDA FRESH HATAR! NAWAAMINIA JWTZ HATAR
Well said mkuu nipe tano kasoro ilo la Jamaa kumwambia Obama mtoto wa .................
 
Screenshot_2017-05-25-23-30-39.png
 
Mpya ya ACACIA hii hapa:

*Boss wa ACACIA anasema wazi kuwa mikataba tuliyoingia nao ilikuwa legal lakini haikuwa ya faida kwa Tanzania.*

“The industry can be its own worst enemy when it sits down and agrees these terms, it’s gonna come back and bite us. And in this case it has,” Gordon says. Those early arrangements, while perfectly legal, “were not equitable”, he adds.

Acacia boss Brad Gordon: The mining industry can be its own worst enemy
 
si kweli,wewe umechukua vipimo vya TMAA usipotoshe mkuu,ile report inadispute analysis za tmaa na sio za acacia
Utakuwa una yako..Hukusoma taarifa yao ya awali wakisema walitoa ushirikiano kwa tume...au unataka kusikia moyo wako unachotamani...Hivi unadhani hao ma prof. hawajui ku triangulate information hadi wachukue kijuju tu huu uchunguzi? Ebu acheni masihara...
 
Twendeni taratibu, container bado zipo na hata hao Acacia kama hawariziki wanatakiwa wawalete wataalam wengine kuchunguza, Hakuna cha SGS wala ACE wote hao wapiga dili bandarini, Sampuli inayochukuliwa wanaipeleka maabara KENYA but ripoti inayotoka kule inatunzwa tu kwenye makabrasha na kutumwa ulaya.

Hata kama kuna kilichoongezeka hawakitoi wanakiwasilisha kama kilivyo kwa waliowapa kazi (ACACIA)
SGS ni jipu kubwa. Wajanja wajanja sana. Nawajua vizuri
 
Mkuu mie sio mwanasheria nmejaribu kuexplain alichosema maana www unaleta upotoshaju basi hayo ya mkataba unasemaje ngoja waende ICSID ndio tutajua mbivu na mbichi ila msije mkalaumu maana lisu amesha watahadharisha!!!! Choice is urs
Unyonge mbaya sana.. makosa yako wazi yametajwa na tume, bado tuogope AGDR sijui HGTK vyanini sasa??
 
Unyonge mbaya sana.. makosa yako wazi yametajwa na tume, bado tuogope AGDR sijui HGTK vyanini sasa??
Lakini mikataba si mlisaini wenyewe au mlilazimishwa???? Ndio maana nasema muda ndio utakaoamua na mambo yote yatakuwa wazi uzuri kuna null hypothesis na alternative so findings za mwisho ndio zitaamua nani mkweli kipindi sakata hili likifika ICSID
 
Huyu bwana angetulia kwanza. Mbona sindano ndiyo kwanza? Atulie tuli! dawa imwingie. Na bado.

Mbona walishavuna sana bado tu wanataka status quo iendelee?

Jamaa wamekuja.....

By Brad Gordon | Chief Executive Officer | Acacia Mining PLC

Response to this morning’s Press Conference and presentation of the First Presidential Committee’s report on the export of metallic mineral concentrates to the President of Tanzania.

Many of you would have seen this morning’s press conference held at State House at which the First Presidential Committee presented its findings on its investigation into the export of gold/copper concentrates.

The Committee has stated that Acacia has not fully declared all of the minerals contained in the concentrate that it exports and the directive halting the export of metallic mineral concentrates remains in place.

We do not agree with the Committee’s findings which state that the value of minerals within the concentrates in the containers currently at the Dar-es-Salaam port is more than 10 times the amount we declare. We are confident in the accuracy of our declarations which are checked and verified by SGS, which is one of the world’s largest testing companies. The concentrate we produce has some small variances, and each container has different declared quantities of concentrate, but we firmly believe that each container contains on average around 3,000kg of copper, 3 kg of gold and 3 kg of silver. Together, these metals are worth an average of Tsh300 million per container.

We are also a listed company with our accounts being audited extensively by PWC, which verifies that we are fully transparent in everything we do. The revenues we state in our audited accounts match the amount of gold that we declare we produce and sell. If the amount of gold in our concentrates was in line with the Committee findings, then it implies that both Bulyanhulu and Buzwagi would produce more gold than any other mine in the world. Sadly this is not the case.

I appreciate that when events like today happen it creates uncertainty and makes people question who to believe. I want to reassure you that Acacia fully declares everything of commercial value that we produce. We also pay all appropriate royalties and taxes on all of the payable minerals that we produce and that the exporting of the concentrate takes place in full compliance with Tanzanian law and the legal agreements that we have with the Tanzanian Government.

Whilst we have listened to today’s presentation and seen a transcript of the press conference, until we receive a copy of the full report it is difficult to comment on or reconcile the specific numbers and values attributed to Acacia’s metallic mineral concentrates by the Committee, but I repeat, we believe in the numbers we declare.

Whilst we await the report I will respond to one question about royalties that has been raised among the workforce. Under the mining act the Government receives royalties of 4% of the minerals of commercial value namely gold, silver and copper contained in the concentrates. Acacia has always paid the royalty and there is a robust audit trail to demonstrate this. Whilst there are other minerals contained in the concentrate, these are of no commercial value. This is due to the small quantities and the cost to extract them exceeds their value, and so no royalty is due.

Obviously today has been a difficult day for everyone at Acacia. I can assure you that we are doing everything we can to ensure that all of our stakeholders believe in the integrity of Acacia. We have fully declared everything that we produce and have done so since Barrick first entered Tanzania over 15 years ago. We have not cheated the country that we operate in and whose people make up 96% of our workforce. Please continue to work safely as that is the most important thing and I will continue to provide you with updates and hopefully clarity as we move through the coming weeks.


View attachment 513955
View attachment 513956
 
Kwahiyo hapo cha kutisha ni kipi? Wanataka tukapime madini kwa wahuni wenzao SGS ambao sisi hatutakubali,tutapeleka kenya na majibu yatawabana tu wakwepa kodi hawa.
 
28th Machi 2017

Acacia Mining plc

LSE:ACA

("Acacia" or the "Company")

Ufafanuzi dhidi ya tuhuma za ushafirishaji wa makinikia ya dhahabu/shaba

Zimepita wiki tatu (3), tangu kutangazwa kwa zuio la ghafla la ushafirishaji wa makinikia ya dhahabu/shaba lililotangazwa tarehe 2 Machi. Tangu kutangazwa kwa zuio hilo kumekua na upotoshwaji mkubwa wa taarifa kwenye vyombo mbalimbali vya habari. Hadi sasa, Acacia haikutoa tamko lolote hadharani, sababu tumekua tukielekeza jitihada katika kutafuta muafaka na Serikali juu ya nini kifanyike. Lakini, kutokana na kiwango kikubwa cha taarifa potofu na zisizo sahihi zenye uvumi mwingi ambao unaweza kutuletea taswira mbaya kwa kampuni, kwa wafanyakazi wetu na pia kwa Tanzania kwa ujumla, tumeamua kuweka wazi hali halisi juu ya hoja mbalimbali.

Acacia inapinga vikali kuhusika na madai yaliyotolewa mwishoni mwa wiki wakati wa ziara ya ukaguzi bandarini – Dar Es Salaam kwamba sisi tulikua tukifanya njama za kutorosha makontena yenye makinikia ya dhahabu/shaba nje ya nchi licha ya katazo lililotangazwa na Serikali. Ukweli ni kwamba si Acacia wala wateja wetu walijaribu kusafirisha makinikia haya nje ya nchi.

Kabla ya kutangazwa kwa zuio hilo, makontena, 256 ambayo sasa yamehifadhiwa ZamCargo (zamani ikijulikana kama Mofed - ambaye ni wakala wa usafirishaji wa forodha Customs Freight Services, CFS) yalikuwa tayari yamesafirishwa kutoka migodi ya Bulyanhulu na Buzwagi, na makontena mengine 21 yaliyokutwa katika bandari ya Dar es Salaam yakiwa tayari yameidhinishwa na idara ya forodha ya Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) na yalikua tayari kusafirishwa. Zoezi hili huwa linajumuisha TRA pamoja na Wizara ya Nishati na Madini (MEM) ambao kwa pamoja wanahusika katika mchakato wa kusafirisha mikinikia nje ya nchi kwa utaratibu maalum.

Acacia imekuwa ikisafirisha makinikia nje ya nchi kutoka mgodi wa Bulyanhulu tangu mwaka 2001 na kutoka mgodi wa Buzwagi tangu mwaka 2010 huku ikiweka bayana mapato yote yanayohusiana na makinikia ya dhahabu/Shaba na kuwasilisha Serikalini. Mapato haya pia yamekua yakitolewa kama mrahaba na malipo mengine kama kodi ya mapato kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA). Sheria za Tanzania zinaruhusu migodi ya Bulyanhulu na Buzwagi kuuza nje ya nchi makinikia ya dhahabu/Shaba, sambamba na kusafirisha makinikia ndani ya makontena. Migodi hii imekua makini kukidhi vigezo vyote vya kisheria na matakwa ya vibali vya usafirishaji (Export Permits).

Tunapenda umma ufahamu kua kila kitu tunachokifanya kinathibitishwa na Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA). Kila kontena la makinikia linalosafirishwa linachukuliwa sampuli chini ya uangalizi wa idara zote za usimamizi ambazo ni TMAA na Kampuni ya huduma za maabara (SGS) ili kwamba Acacia na Serikali ziweze kukadiria wingi wa madini ya dhahabu, shaba na fedha yaliyomo. Matokeo ya sampuli hizi hupelekwa TMAA, TRA, Acacia na kampuni zenye mitambo maalum ya kuyeyusha na kuchenjua makinikia (Smelters) ili kubaini mrahaba wa awali ambao Serikali italipwa kabla ya kusafirisha makinikia.

Ni pale tu ambapo upimwaji wa sampuli umekamilika, na mrahaba umeshalipwa kwa Serikali, ndipo makontenta yanafungwa kwa lakiri maalum za TMAA, MEM na TRA, na makinikia yanaweza LSE:ACA www.acaciamining.com


kusafirishwa kutoka migodini. Kisha makontena husafirishwa wa magari ya kubebea mizigo hadi kituo cha forodha cha Isaka ambako nyaraka za mwisho za kusafirisha nje ya nchi hutolewa na MEM pamoja na TRA, na makontena kuidhinishwa kwa safari ya kwenda bandari ya Dar es Salaam.

Baada nyaraka zote kukaguliwa na kuhakikishwa na maafisa wa forodha, kila kontena hukaguliwa kwa kutumia mtambo maalumu wa kieletroniki (Scanner) ili kuthibitisha kua ndani yake hakuna kitu kingine chochote isipokua makinikia ya dhahabu/Shaba tu. Baada ya hapo makontena huhifadhiwa a chini ya ulinzi wa maafisa wa forodha mpaka hatua za mwisho za upakiaji wa makontena kwenye meli tayari kwa kusafirisha nje ya nchi.

Acacia iko tayari kushirikiana na Serikali kutafiti uwezekano wa Tanzania kua na kiwanda cha uchenjuaji ambacho kitatoa ajira na kuleta maendeleo kwenye sekta hii. Maendeleo ya teknolojia yanaweza kutoa muelekeo stahili juu ya uwezekano huu.

Hadi hivi sasa, migodi ya Bulyanhulu na Buzwagi imeendelea na uzalishaji kama kawaida hata baada ya zuio la Serikali na makinikia haya yamehifadhiwa katika maeneo maalumu migodini. Lakini hali hii haiwezi kua ya kudumu kutokana na umuhimu wa kukusanya mapato yatokanayo na biashara ya makinikia kwa migodi hii miwili.

Acacia inaunga mkono kikamilifu jitihada za bila kuchoka za Mh. Rais Dkt. John Pombe Magufuli na Serikali yake kuwekeza katika maendeleo ya nchi kupitia elimu, ajira na viwanda. Acacia ni mwajiri mkubwa nchini Tanzania na sasa tumetoa ajira za moja kwa moja za zaidi ya wafanyakazi 5,000 pamoja na wakandarasi na ajira zingine 55,000 katika uchumi, zinazofaidisha familia na jamii kwa ujumla. Kati ya waajiriwa wote wa Acacia, zaidi ya asilimia 96 ni Watanzania. Migodi yetu inasaidia kuendeleza wazawa kupitia idara yetu ya ugavi ili kuwapatia fursa endelevu za kibiashara.

Tunapenda kuendelea kuwakaribisha maafisa wa serikali kuja kutembelea migodi yetu ili waweze kufahamu mchakato mzima wa kuzalisha madini, kukusanya sampuli na kusafirisha makinikia ya dhahabu/shaba nje ya nchi.

Kwa Taarifa:

Tembelea tovuti yetu : www.acaciamining.com
 
*Boss wa ACACIA anasema wazi kuwa mikataba tuliyoingia nao ilikuwa legal lakini haikuwa ya faida kwa Tanzania.*

“The industry can be its own worst enemy when it sits down and agrees these terms, it’s gonna come back and bite us. And in this case it has,” Gordon says. Those early arrangements, while perfectly legal, “were not equitable”, he adds.

Acacia boss Brad Gordon: The mining industry can be its own worst enemy
 
Sasa si hapo juu jaman kasema kuwa hajapitia ripot nzima, snw mpaka waipate yote ndo wanaweza kuzungumza na kutoa muafaka wao. mi nashndwa kuelewa maelezo yote ya nini hapo kwa kukana uhalali wa ripot wakat anakil kuwa hawajaipata yote. Pia tulitalajia kuwa lazima wataipinga tu, kwakuwa hakuna mwizi wala muuaji anaeweza kukubali makosa yake moja kwa moja.
 
Sasa si hapo juu jaman kasema kuwa hajapitia ripot nzima, snw mpaka waipate yote ndo wanaweza kuzungumza na kutoa muafaka wao. mi nashndwa kuelewa maelezo yote ya nini hapo kwa kukana uhalali wa ripot wakat anakil kuwa hawajaipata yote. Pia tulitalajia kuwa lazima wataipinga tu, kwakuwa hakuna mwizi wala muuaji anaeweza kukubali makosa yake moja kwa moja.
 
Back
Top Bottom