Acacia inataka mazungumzo ya moja kwa moja na serikali na sio kupitia madalali.

Mukulu wa Bakulu

JF-Expert Member
Aug 12, 2014
4,052
12,906
Mazungumzo ya serikali na kampuni ya Barrick yamechukua muda mrefu, kila mbinu imetumika kuyamaliza lakini hakuna njia muafaka iliyofikiwa hadi sasa.

Kampuni ya Acacia inasema inataka mazungumzo na serikali moja kwa moja bila kupitia kwa mtu wa kati(hapa ni Barrick). Muda mrefu Acacia imekua ikiituhumu Barrick kuwatenga katika mazungumzo huku Barrick akijua wazi kabisa hakuna kitakachofikiwa bila kuridhiwa na Acacia wenyewe. Acacia alivyo mbabe amemgomea Barick kumnunua.
 
Hii ngoma bado mbichi sana kila part ina interests zake Barrick ana interest yake, Acacia ana interest yake na Tanzania ina interests zake, navyoona kesi hii lazima itaamuliwa na mahakama ya kimataifa.

Huwezi kuikana Acacia wakati ndiye mliingia naye mkataba, Acacia ni entity company imesajiriwa hata kama Tanzania haiitambui lkn ndiyo inayolipa kodi zote siyo Barrick.
 
Wengine Wale watakuja hapa na hoja kua ACCACIA wametupia magoti. Make mazungumzo na ACCACIA nayo itachukua 2 years alafu mazungumzo unaombwa kati ya Barrick..ACCACIA na serikali alafu kesi inaenda mahakamani wakati huo muda wa JPM umeshaisha tunakamuliwa kama 900bilion.
Wale akina Wakudadavua na kampani yake wanabadilisha tena ID na Kuja na ID na hoja ya kuwashangilia ACACIA.
 
Kuna watu wabishi sana huko ccm na huwa wanabishania jambo wasilolijua hata kidogo! Acacia anatawaumbua na huenda tubaki na mshangao kwa yatakayojitokeza na tunayoaminishwa yakatoweka! Wakaribishwe na wasikilizwe tumalize huu utata!
 
Mazungumzo ya serikali na kampuni ya Barrick yamechukua muda mrefu, kila mbinu imetumika kuyamaliza lakini hakuna njia muafaka iliyofikiwa hadi sasa.

Kampuni ya Acacia inasema inataka mazungumzo na serikali moja kwa moja bila kupitia kwa mtu wa kati(hapa ni Barrick). Muda mrefu Acacia imekua ikiituhumu Barrick kuwatenga katika mazungumzo huku Barrick akijua wazi kabisa hakuna kitakachofikiwa bila kuridhiwa na Acacia wenyewe. Acacia alivyo mbabe amemgomea Barick kumnunua.
Kama nilielewa vzr serikali iligoma kuwatambua acacia..
Kama ndivo ni vema kwa serikali kubaki na msimamo wake hawa jamaa watatuona sisi mabwege. Move waliyofanya Barick inaeleweka kwani alijaribu kulinda maslahi yake. Ikitokea Acacia kaathirika mhanga mkubwa ni Barick anayemiliki takriban theluthi mbili ya acacia.
Ni bora hata kulipa fidia lakini tujenge nidhamu na misingi ya winwin situation going foward. Kama sehemu ya mkakati
Ikibidi wote waliohusika na udanganyifu ule wa makinikia ni kusukuma ndani kwa uhujumu uchumi wakiwemo Directors..
Waache dharau kabisaa
 
Loud and clear
 
Prof Kalamaganda yuko wapi?Tunaaminishwa vitu vingi sana,Mwananchi wa kawaida ni vigumu sana kujua na kuelewa haya masuala
 
Yani nikiikumbuka ile Siku ilipo wasilishwa Ripoti ya Makinikia sina hata hamu ,nnaona wana endeleza mapicha picha tu kuanzia mwenye Mali mpaka mmbebaji/mchukuaji.Mh sana na mtukufu aliaminishwa/akaaminisha Raia wake lakini matokeo yake ndio haya ,dana dana kama za mpira wa kusuka bana 😎
 
Back
Top Bottom