Acacia Buzwagi ichunguzwe namna inavyowahudumia Wafanyakazi waliopata ugonjwa wakiwa kazini! Wengi hawapati huduma stahiki

Mr.Thinker

Senior Member
Dec 13, 2013
125
137
Habari za humu wanajamvi,

Naamini mu wazima wa Afya, leo naomba kuwashirikisha kuhusu kile ninachokiita unyanyasaji wa hawa Acacia ambao ni mshirika wa African Barrick Gold(ABG) ambao wanamiliki migodi ya dhahabu kama vile Buzwagi Gold Mining, Geita Gold Mining na Bulyanhulu Gold Mining huko Kakola

Kutokana na kazi mbalimbali za mgodini, hutokea Wafanyakazi kupata ajali au ulemavu. Kwa mfano kuwa kiziwi, kuvunjika viungo vya mwili, matatizo ya uti wa mgongo, hii hutokea kutokana na uendeshaji wa mitambo mikubwa ndani ya mgodi.

Baada ya mfanyakazi kupata ulemavu, Acacia huwaweka katika makundi mawili, temporary disability na permanent disability. Kisha huwaachisha kazi kwa sababu za kiafya(medical reason)

Sasa makundi mawili yote hulipwa fidia, lakini yule mwenye temporary disability yeye hupata tiba, mfano aliyevunjika mguu, akishapata matibabu na kupona, analipwa fidia tu. Mwenye permanent disability yeye hulipwa fidia, lakini ACACIA wanaendelea kumtibia na kumlipa hela ya matibabu ikiwemo na kumsimamia tiba ya vitendo(physiotherapy)

Kutokana na gharama kubwa za fidia, Acacia inadaiwa hukwepa gharama hizo kwa baadhi ya Wagonjwa kwa kuwafukuza kazini kwa sababu ya utoro au kumsingzia wizi. Hili linanishangaza sana sababu hii ni kampuni kubwa, wamiliki ni wazungu, viongozi wa Acacia kwa sasa wengi ni wabongo, hawa hawa wabongo ndo huwachapa rungu wafanyakazi walemavu na wagonjwa kwa kuwafukuza / kuwaachisha kazi kwa reason ya utoro ama kuwasingzia wizi

Pia ili kukwepa gharama za kuwahudumia Acacia inaelezwa kuwa huwalipa fidia chache tu wahanga, pia baadhi ya watu waliopata permanent disability huacha ghafla kuwasimamia matibabu endelevu kwa daktari wa kampuni kudaiwa kufanya yafuatayo;

1. Kuidhinisha/kupotosha kuwa mgonjwa kapona

2. Kutoa rushwa kwa physiotherapist wa hosptali za rufaa ili watoe ripot kuwa mgonjwa kapona

3. Kutoa rushwa kwa watendaji ama medical officer wa OSHA(Hii ni mamlaka inahusika na kusimamia haki za wafanyakazi walioumia katika mazingira ya kazi) sasa huyu daktari wa OSHA hupotosha kuwa ULEMAVU WA MGONJWA HAUJATOKANA NA KAZI ZA BUZWAGI.

4. Aidha, Acacia wanadaiwa huhonga Mahakimu ama Mawakili wa wagonjwa ili kesi iishe haraka. Kwanini? Ili Acacia isichafuliwe mbele ya Serikali kuwa inanyanyasa wafanyakazi.

Na inadaiwa huwa wanawatamkia wagonjwa waziwazi kuwa hata ukifungua kesi hutafika popote.

Mgonjwa akiwa na BACK-UP KUBWA, huwa wanamuita na kumwambia aifunge kesi ili wamlipe kiasi akitakacho Mfano Milioni 200 ili kesi iishe, kisha walalahoi wasokuwa na back~up hufyekelewa mbali.

Baadhi ya wagonjwa hawa hukomaa na kesi, mwishowe hela za kusafiri kwenda mahakamani huwaishia(Mahakama Kuu au ya Rufaa) huwa wanakuwa watoro kesi zikitajwa hivyo Acacia huibuka mshindi.

Kwa hiyo kuna kundi kubwa la wafanyakazi walopata ulemavu kazini, wakatelekezwa na kampuni.

NB: Katika Acacia na migodi mingine mikubwa, wafanyakazi wote hupimwa afya ya mwili na akili, hii ni pamoja na utimamu wa viungo vya mwili, mtu akifuzu vipimo hivi maridadi ndipo husainishwa mkataba na kampuni, kwa hiyo mtu akiwa na tatizo kimwili ,kiafya kamwe hawamwajiri.

Nimekulia mazingira ya migodi hii ya ACACIA, na baadhi ya wahanga nawajua, wiki hii nimebahatika kukutana na mmoja wao, ambaye ni mama wa watoto wawili, yeye aliajiriwa na AFRICAN BARICK GOLD,(kipindi hicho bado ACACIA hajachukua madaraka)

Ilikuwa ni 2012, alifuzu vipimo vya mwili, afya na akili, hivyo akaajiriwa kuendesha mitambo mikubwa mikubwa(Heavy Machine Operator), (miezi mitatu ya kwanza unakuwa chini ya uangalizi baada ya hapo unakuwa permanent employed.)

Alifanya kazi kwa weledi wote, lakini miaka miwili baadaye, alianza kupata maumivu ya mgongo, ilikuwa 2014, mwanzoni wa 2015 aliletwa Dar es salaam, MOI kwa vipimo,alisafirishwa na ndege ya kampuni akiwa na wafanyakazi wengine wagonjwa.

Baada ya kupimwa MRI NA CT SCAN ilijulikana kuwa mifupa ya uti wa mgongo iliyo L3&L4(L=lumbar area) imesagika, mild bifecetal arthritis.. hivyo akaandikiwa dawa na ahudhurie physiotherapy. Madaktari wa Muhimbili, MOI walisema chanzo mojawapo cha tatizo ni kuendesha mitambo yenye mitikisiko mikubwa.

Alirudi Kahama, akaendelea na dawa na kuhudhuria physiotherapy(Akitumia bima ya kampuni, Acacia wanatumia bima ya afya ya AAR

Alipokuwa akijiuguza ilipelekea asiende kazini, hivyo HR wa Acacia akamuachisha kazi kwa sababu ya utoro na arirudsha ID ya bima ya AAR. lakini huku Acacia wakijua ni mgonjwa.

2015 akafungua kesi Mahakama ya mwanzo Kahama, kesi ikahamishiwa Shinyanga, baada ya mikiki mikiki ya kesi. 2017 yeye na wenzake baadhi walishinda kesi hivo Acacia wakawalipa fidia ya kuwasababishia ugonjwa kazini.

Lakini pia huyu mama ilitakiwa aendelee kupatiwa matibabu na Acacia ambao waligoma kuwa Disability haijasababishwa na kazi, mwaka 2017 kwa gharama zake binafisi alikuja Dar es salaam, MOI, kurudia vipmo vya MRI, NA CT SCAN ambapo madaktari wa MOI wakagundua madudu mengne ambayo yalifichwa na ripoti ya mwanzo iliyoratibiwa chini ya usimamizi wa Acacia, madaktari wakasema siyo tu kuwa ana bifecetal arthritis between L3 na L4 bali pia ana DISC PLORAPSE BETWEEN L3 na L4
hivo anahitaji operation haraka la sivyo hatatembea tena akikawia operation. Operation inagharimu zaid ya Millioni 4.

Hivyo huyu mama Jane Feza arirudi Acacia kuomba wamtibie kama sheria na Katiba inavyosema, wakakataa kuwa tatizo lake halijatokana na kazi, Bi Jane Feza alienda kuwashitaki OSHA. Huko OSHA nao walimzungusha na dalili za rushwa zikionekana.

Wiki ilopita Acacia walimpigia simu kuwa aende OSHA kufata conclusion ya suala lake, sintofahamu nyingine ni kuwa walimpatia nauli elfu 60 nauli ya Bus kutoka Kahama kuja Dar es salaam. Kwanini mgonjwa wa uti wa mgongo asafirishwa kwa basi? why asilipiwe ndege kama awali? basi Jumapili kaja Dar.

Walimlipia hoteli, jumatatu apumzike, jumanne aende OSHA kufata majibu. Jumanne tarehe 8 Januari 2019 alifika Ofisi za OSHA Kinondoni, wailimpatia ripoti ya suala lake kuwa halijatokana na kazi za Buzwagi. Tafsiri ni kuwa Acacia isihusike na kumtibu, Baada ya kupata ripoti hiyo Bi. Jane Feza alizimia, Daktari wa OSHA akampeleke hospitali jirani ya Kinondoni ambapo alipata first aid, akazinduka

Hospital ikahitaji malipo, OSHA wakadai mwajiri wake Acacia watalipia, kweli wanalipia care anayopata hapo kinondoni hospital, madaktari wa hapo wameshauri wampe rufaa kwenda MOI ili apate operation ya tatzo lake, maana sasa ananyanyuka kwa shida, akikawia hatatembea tena, ACACIA WAMEGOMA KUGHARAMIA OPETATIPN, WANATUMIA RIPOTI YA OSHA KUMNYANYASA.

Hakika kuna harufu ya rushwa toka ACACIA kwenda OSHA. Nimemuuliza, Acacia wanalipa gharama za kulazwa na chakula, akasema wanawapigia simu Acacia, mpaka kaka yake Joseph Feza akoromeane nao ndo wanatuma elfu 30 ya chakula, wakati mwingine hawapokei simu.

Lakini pia amesema tokea 2015 hawezi kuinama,kufua na kufanya kazi za nguvu, muda wote ananunua dawa alizoandikuwa MOI ili kupunguza maumivu ya mgongo na miguu, dawa hizo ni Neurotone, Prigabalin na ketoprofen gel ya kuchua.

SASA WANAJAMVI, TUMSAIDIE BI JANE, HILI SUALA LIFIKE KWA RAIS MAGUFULI NA WIZARA YA KAZI ILI BI JANE FEZA APATE OPERATION NA ACACIA WAENDELEE KUMTIBU. NTASOMA KILA MAONI YENU, PICHA CHINI NI MKATABA WA KAZI, MAJIBU HALISI YA MOI, MOJA YA RUFAA YA BUZWAGI KUMPELEKA MOI, PIA NA MAJIBU YA OSHA.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Baadhi ya document za bi jane feza ,0753 576956
2019-01-11%2010.25.25.jpeg
2019-01-11%2010.24.02.jpeg
2019-01-11%2010.22.42.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ivi Geita GGM inamilikiwa na Acacia kweli ?
ACACIA,ABG wanahisa kubwa GGM.
na hata hili suala la kupeleka wagonjwa kuja Dar kwa vipmo, ndege ya ACACIA, hubeba hao wagonjwa kuanzia Buzwagi kisha inaenda kuwabeba na wa Bulyanhulu, kidha Geita gold mining , mwsho inawapitia na wa North Mara gold mining, Then safar ya kuja Dar ndo inaanza, wakifika Dar huwa wanawapeleka hotelin, Tiffany Diamond hotel Dar es salaam ,
kwa nyongeza tu, suala la kuwabeba wahanga/waathirika kiafya na kaz za mgodini na kuwaweka hoteli moja Dar, lilipelekea wagonjwa kutoka migodi yote kuwa na umoja, na wakawa wanafany mikutano kisiri hotelini ili wasaidiane wasidhulumiwe, ISHU HII WATENDAJI WA ACACIA WAKAIJUA, hivo kwa sasa wakileta wagonjwa wanawasambaza ktk hoteli tatu tofauti, hoteli hzo ni DURBAN HOTELI(Karibu na stend ya mnaz mmoja ) , Tiffany diamond hoteli(posta) na SAPHIRE HOTEL (Posta)

lkn ktk hizi hotel, wanafanyiwa unyanyasaji wa malazi tofauti na miaka ya nyuma, wahudumu wakiulizwa' wanasema waajiri wenu ndo wameelewana hivo na menejiment ya hotel

I doubt, you might have a mental problem as well
 
mkuu, kuhusiana na hili , hujaelewa nn? ts better to ask, don't jump into conclusion without observation. coz once someone quoted that , "EXPLANATION CAN BRING US TO GOOD CONCLUSION IF THERE IS NO SUFFICIENT OBSERVATION"

Sent using Jamii Forums mobile app
My understanding, GGML is owned by AngloAshanti and some few minorities, neither Acacia nor ABG have a single share in GGML. Hapo ndio ninapoanzia kutilia shaka lalamiko lako. From the attached letters, the underlined sentence exonerates your employer from any liability. Najiuliza spati jibu
 
accaccia wanamimiki ggm?? maelezo mengiii lakini uongoo mtupu! kama mfanyakazi amepata occupational diseases sheria inasemaje, tuanzie hapa
 
ACACIA,ABG wanahisa kubwa GGM.
na hata hili suala la kupeleka wagonjwa kuja Dar kwa vipmo, ndege ya ACACIA, hubeba hao wagonjwa kuanzia Buzwagi kisha inaenda kuwabeba na wa Bulyanhulu, kidha Geita gold mining , mwsho inawapitia na wa North Mara gold mining, Then safar ya kuja Dar ndo inaanza, wakifika Dar huwa wanawapeleka hotelin, Tiffany Diamond hotel Dar es salaam ,
kwa nyongeza tu, suala la kuwabeba wahanga/waathirika kiafya na kaz za mgodini na kuwaweka hoteli moja Dar, lilipelekea wagonjwa kutoka migodi yote kuwa na umoja, na wakawa wanafany mikutano kisiri hotelini ili wasaidiane wasidhulumiwe, ISHU HII WATENDAJI WA ACACIA WAKAIJUA, hivo kwa sasa wakileta wagonjwa wanawasambaza ktk hoteli tatu tofauti, hoteli hzo ni DURBAN HOTELI(Karibu na stend ya mnaz mmoja ) , Tiffany diamond hoteli(posta) na SAPHIRE HOTEL (Posta)

lkn ktk hizi hotel, wanafanyiwa unyanyasaji wa malazi tofauti na miaka ya nyuma, wahudumu wakiulizwa' wanasema waajiri wenu ndo wameelewana hivo na menejiment ya hotel

Sent using Jamii Forums mobile app
umeharibu uzi wako wote , siku zote uwongo + ukweli = uwongo
 
My understanding, GGML is owned by AngloAshanti and some few minorities, neither Acacia nor ABG have a single share in GGML. Hapo ndio ninapoanzia kutilia shaka lalamiko lako. From the attached letters, the underlined sentence exonerates your employer from any liability. Najiuliza spati jibu
may b ndo iko hivyo kwenye suala la umiliki, mimi nafikiria somehow ACACIA wako connected na GGM, coz ktk usafirishaji wa hawa wagonjwa huwa wanawabeba kwa pamoja kuja Dar kwa ajili ya vipimo na physiotherapy.

Ok tuache hilo suala la wamiliki wa GGM, turudi kwenye suala la Bi Jane Feza, attached photos, mojawapo ni mkataba wa kazi baina yake na kampuni, kwenye dotted lines, mkataba unasema Bi Jane Feza amefuzu vipimo vya Afya,

sasa turudi kwenye barua hii ya OSHA, wamesema tatzo lake halijatokana na kazi aliyofanya Buzwagi.

how come? mwanzo kabisa wakati anaajiriwa vipmo vilifanywa na hakuwa na tatizo, iweje sasa ana tatizo , tena dalili zote kazipata meanwhile anafanya kazi Buzwagi, Na kwa nini vipmo vilivyoratibiwa na kampuni vikanushe suala ka ugonjwa kuhusiana na kazi? lakin alipojigharamia yeye mwenyewe arudie vipmo, matatzo yanajulikana zaidi ya moja(more than one provisional diagnosis) na Daktari anasema moja ya sababu ya huu ugonjwa ni kufanya kazi nzito na zenye mitikisiko.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom