AC Milan yafungiwa kushiriki michuano ya ulaya kwa kukiuka sheria ya Financial Fair Play(FFP)

Aaron Arsenal

JF-Expert Member
Jul 24, 2014
24,504
28,691
AC Milan will not take part in the Europa League next season after being banned by the Court of Arbitration for Sport

Nafasi yake itachukuliwa na Torino

Kesi nyingine inaendelea ya Manchester city ambayo nafasi yake itachukuliwa na Arsenal.

-------
Klabu ya soka ya AC Milan ya Italia yenye makazi yake katika uwanja wa San Siro, itatumikia kifungo cha mwaka mmoja kutokushiriki michuano ya Ulaya inayoandaliwa na UEFA ikiwa ni Klabu Bingwa Ulaya na Europa Ligi

Klabu hiyo iliyomaliza katika nafasi ya 5 kwenye ligi ya soka Italia, Serie A imekumbana na kifungo kutoka kwa Mahakama ya Usuluhishi ya Michezo baada ya kuvunja sheria ya 'Financial Fair Play' na hivyo haitashiriki michuano ya Europa ya msimu ujao

Kuna uwezekana mkubwa kuwa kwa sasa nafasi yao ya kushiriki Ligi ya Europa itachukuliwa na Torino, iliyomaliza katika nafasi ya 7 kwenye Ligi ya Serie A msimu uliopita. Roma iliyokuwa nafasi ya 6 ilishafuzu

Milan ilifanikiwa kukata rufaa dhidi ya kifungo cha miaka miwili ilichopewa awali na UEFA msimu wa majira ya joto uliopita baada ya kupatikana na hatia ya kuvunja sheria ya hiyo ya 'Financial Fair Play'
 
Man city akitolewa anachikua Arsenal? Nilifikiri akitolewa Chelsie ndiyo Arsenal wanapata fursa?
 
Tulia toa takwimu za uhakika... Kiwango cha pesa kilichotumika.. Watu waliosajili... Lini tukio lilibainika na mchakato nzima juu ya sheria hii upo vipi.

Sio unaandika tu torino.. Man city maara ffp..
Nin sasa mkuu?
 
Back
Top Bottom