AC Milan ni 'kidume' wa kitaliano

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Dec 27, 2012
10,196
25,516
Klabu ya AC Milan jana ilidhihirisha umwamba wake katika soka ya ulaya ( Klabu Bingwa barani humo) baada ya kuwa timu pekee ya Italia kusonga mbele katika hatua ya mtoano wa michuano hiyo.Milan imesonga mbele na Barcelona kutoka kundi lao.

Klabu za Juventus na Napoli zimepiwa kumbo katika michuano hiyo. Juventus ilizamishwa 1-0 na Galatasaray ya Uturuki huku Napoli,pamoja na jana kuishinda Arsenal 2-0, ilizidiwa ujanja na Arsenal na Borussia Dortmund.

Katika mechi ya jana dhidi ya Ajax ya Uholanzi, Milan ilicheza pungufu tangu dakika ya 22 ambapo Nahodha Ricardo Montolivo alitolewa kwa kadi nyekundu. Mwisho mwishoni AC Milan ilifanikiwa kupata suluhu ya 0-0 iliyoivusha Milan.

Forza Milan!

cc Gang Chomba
 
Haya tumejua kidume wa kitaliano tutajie sasa na kijike wa kitaliano.
 
Forza Milan...
Ingawa kuna waandishi washambenga pale Ulaya wameandika Headlined zinasema 'the wrong italy team went through'
 
Ac Milan hakuna kitu mule, mwisho wao mtoano, wamejitahidi sana robo. Kama Milan angepangwa ktk Makundi aliyopo Juventus au Napoli basi yeye ndo angekuwa wa kwanza kuaga mashindano.
 
ALEYN napingana na wewe kabisa. Ac Milan angepangwa kundi lolote angeweza kupita 7bu Milan wanauzoefu na kombe la UEFA alafu wanajua wanafanya nini na wakati gani. Alafu Juventus tuliwekwa kundi jepesi tu sema ni uzembe wa Conte kushindwa kusoma mchezo. Milan natumaini watafika mbali tu kwenye CL.
 
Ivi mbona tmu za italia miaka ya karibuni zimekuwa hazifanyi vzuri?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom