Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,197
- 25,516
Klabu ya AC Milan jana ilidhihirisha umwamba wake katika soka ya ulaya ( Klabu Bingwa barani humo) baada ya kuwa timu pekee ya Italia kusonga mbele katika hatua ya mtoano wa michuano hiyo.Milan imesonga mbele na Barcelona kutoka kundi lao.
Klabu za Juventus na Napoli zimepiwa kumbo katika michuano hiyo. Juventus ilizamishwa 1-0 na Galatasaray ya Uturuki huku Napoli,pamoja na jana kuishinda Arsenal 2-0, ilizidiwa ujanja na Arsenal na Borussia Dortmund.
Katika mechi ya jana dhidi ya Ajax ya Uholanzi, Milan ilicheza pungufu tangu dakika ya 22 ambapo Nahodha Ricardo Montolivo alitolewa kwa kadi nyekundu. Mwisho mwishoni AC Milan ilifanikiwa kupata suluhu ya 0-0 iliyoivusha Milan.
Forza Milan!
cc Gang Chomba