Absence ya Lowassa kama PM inaiathiri CCM kila uchwao


The Hunter

The Hunter

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2010
Messages
1,050
Points
1,225
The Hunter

The Hunter

JF-Expert Member
Joined Dec 25, 2010
1,050 1,225
Naikumbuka 1995 pale Nyerere alipotikiswa na Nguvu ya jamaa huyu,japo alionekana kijana nguvu yake ilikuwa ni kubwa sana, wengi hawakumtegemea maana taswira nyingi ziliwaelekea Malecela Sr, Dr.Salm,Kigoda na wengine..Mkapa hakupewa nafasi kubwa na hii nikutokana na kutokufahamika kwake
Lowassa japo hakupita lakini aliacha foot prints ambapo ilipokuja tena 2000, nguvu yake ikaonekana dhahiri, yawezekana ni makubaliano ama maafikiano baina yake na swaiba yake yaliyompelekea kuondoa jina lake..
Wengi tunajua kilichotokea..wengi tunafahamu mwaka ule ndipo hasa chuki, makundi na fitna ndani ya CCM zilipochipuka, mtakumbuka haya
MKAPA; Alimsaliti Malecela Sr
Ikumbukwe Malecela alishajiaminisha kuwa raisi ajaye,..ikumbukwe kizingiti cha yeye kuwa raisi kilishaondoka (NYERERE)
Lakini dakika ya mwisho kabla kikao cha Halmashauri kuu pale Chimwaga kuanza Raisi Mkapa alimlazimisha Malecela kukalia kiti chake kama makamu wa ccm, na hivyo kumyima fursa ya yeye kugombea maana isingewezekana tena..

KIKWETE; ALIMSALITI SITTA
Ikumbukwe Sitta alishaahidiwa nafasi ya U Waziri Mkuu kama Kikwete angepita,..hii ilitokea baada ya Lowassa kusimama kama mgombea thou alijitoa, na kujitoa huku kutokana na makubaliano yake na Kikwete kuliathiri nafasi ya Sitta kuwa PM ajaye

Lowassa alipokalia kiti cha u PM; wengi tunakumbuka mambo yalivyoanza kwenda mchakamchaka, nani asiekumbuka jinsi huduma zilivyoanza kuboreka na hii ni kutokana na wengi kuhofia nafasi zao kuwaponyoka wasipofanya kazi kwa bidii

Ni wazi; kama binadamu wengine Lowassa hakuwa mkamilifu.. lakini tujiulize na tutende haki mangapi yalianza kufanyika aliposhika hatamu

Leo tunapomshuhudia Nape na kina Malecela Jr... wakija na siasa za kitoto, za kijinga na zisizo productive lazima tumkumbuke Jembe Lowassa na Think Tank wengine waliokuwa watenda kazi zaidi ya hawa vijana-hovyohovyo wasiojua chama cha ccm kifanyeje ili kijijenge upya

NB
kumshambulia Silaa hakutaisaidia ccm kamwe zaidi kunamjenga, na kumfanya kukumbukwa na jamii inayomjua na isiyomjua kila uchwao.
 

Forum statistics

Threads 1,284,537
Members 494,169
Posts 30,830,983
Top