Absalom Kibanda (Mwenyekiti wa Jukwa la Waharirii) avamiwa na watu wasiojulikana na kujeruhiwa

Mungu amjalie heri na apone haraka arudi kwenye mapambano. Adui yetu watanzania ni umaskini, ujinga na maradhi,,, ni bora kuelekeza nguvu kupambana na hao maadui badala ya kupambana na watu kama Kibanda. Mpumbavu pekee huwaza kumdhuru mtu ili kufifisha fikra zake.
 
Waanzilishi wa JF na Moderators,

Nina ushauri ninataka niutoe kwenu leo, nimejiunga na JF tangu mwaka 2008 na mambo yalikuwa yanakwenda sawa ni hivi karibuni tu baada ya kuibuka wimbi la vijana wanaomaliza elimu ya kidato cha nne kwa kuchora mazombie ndipo uchangiaji wa mada hata kwa masuala nyeti umekuwa ni wa mzaha, matusi na hoja dhaifu zisizokuwa na mashiko, haiwezekani habari ya kushtusha, kusikitisha, kuhuzunisha na kughadhabisha kama hii baadhi ya watu waandike mambo ya hovyo hovyo kama haya.

Nionavyo mimi ni kuwa perception za baadhi ya watu kuhusu JF kwa ujumla ni kwamba hii ni forum ya recreation kwa ujumla wake na hivyo unapokuwa umechoka basi unarelax kwa kuja huku na kufanya mzaha ( Ninaelewa yapo majukwaa ya mizaha lakini yapo mengine ambayo sio ya mizaa mathalani JF Doctor, Habari za Kisiasa, Jamii Intelligence n.k)

USHAURI WANGU:

Futeni membership zote JF na watu wajiandikishe tena lakini this time kwa kutoa kamtihani fulani hivi cha kutest IQ za wanaotaka kujiunga. Imenisikitisha sana tukio kama hili na mengine kama haya yaliyowahi kutokea then watu wanacomment mzaha, mbaya zaidi unakuta wengi ni vijana wenzangu ambao walitakiwa wawe smart kwenye kufikiria, kuongea, kuandika na hata kutenda kila jambo.
 
Natamani Jeshi letu la polisi lingekuwa na uwezo wa kuchunguza masuala kama haya. Pia natamani angekuwa mtu mkubwa serikalini kwani tungekodi FBI. Poor bro Kibanda. Wish you a quick recovery

......

Its everyone's wish, kinana will help him as he has been promoting him
.
 
Mungu amuokeo na aendelee na kazi yake ya kuukomboa umma, jamani hao watu watalaaniwa xanaa!!
 
habari hii imenistua sana ,pole sana ABSALOM KIBANDA MUNGU atakuponya haraka uendelee na majukumu yako
 
Kumbe ilikuwa hivi....
Haya ni maneno kutoka kwa mtu wanaekaa naye nyumba moja.
ametekwa akirudi nyyumbani getini km saa sita na nusu mlinzi alipomfungulia aliona watu wawili wamembeba wanakimbia nae,ndo akaja kutuamsha hawakuchukua kitu chochote kwenye gari kulikuwa na lap top nk,baadaye amekutwa amepigwa sana alikuwa hawezi hata kusema,inaonekana hao hawakuwa majambazi ni watu waliotumwa kumdhuru but not proffesional kwa sababu hawakupoteza malengo km wangechukua v2 kwenye gari tungesema ni
majambazi any way ngoja tusubiri ila Police wanakatisha tamaa wamechukua muda kuja
 
Watu tusiwe tunahisi hisi vitu ambavyo hatuvijui waacheni wafanye uchunguzi inakuwaje watu wa judge moja kwa moja kuwa mtanzania daima ichunguzwe? Hata mke wa mtu ni sumu pia so subirini uchunguzi
 
Hii ni kudhihirisha tu kwamba wananchi hatuko salama kabisa. Kama wananchi wanavamiwa, wanapigwa, wanajeruhiwa na wengine kuuwawa kila mara na serikali kupitia vfyombo vyake vya dola wameshindwa kabisa kudhibiti hali hiyo ni dhahiri kwamba kama taifa tunahitaji kujipanga na kuchukua mwelekeo mpya kwa ajili ya usalama wetu.

Hii inadhihirisha pasipo shaka yoyote kwamba usalama wa taifa pamoja na jeshi la polisi wameshindwa kabisa kutekeleza majukumu yao ya msingi kwa raia wa nchi hii, na kimsingi hatuoni umuhimu wa kuwa na usalama wa taifa tulio nao kwa sasa kwakuwa wameshindwa kabisa kazi waliyotumwa kuifanya.

Na kwahali hii tunalazimika kuhitaji overhaul ya idara hii nyeti kwa ustawi, usalama na maendeleo ya watanzania. Major overhaul kwa TISS ni kitu kisichoepukika kwa sasa.
 
Kama ya ulimboka,sisi wa tz tuko tofauti na nchi nyingine tukio hili ni kubwa sana,tulitakiwa tusikubali watu kuteswa kufanyiwa vitendo vya kinyama,lkn tunaona kama jambo la kawaida,oh my God
 
Tusiwe wepesi wa kuchora mstali na kuhitimisha kwenye jambo linalohitaji fikra pevu na uchunguzi mpana.
Cha kufanya ni kumtakia heri huku uchunguzi ukiendelea.

Mkuu unatarajia nini endapo walio mteka ndo hao hao wanao takiwa kufanya uchunguzi ? Kweli nime amini hiki kizazi cha tume ni problem.
 
Polisi waanze uchunguzi na gazeti la tanzania daima na chadema. kwani hatuelewi ni kwanini alikimbia huko alipokuwa mhariri wa hilo gazeti la mwenyekiti wa chama.

Mnatengeneza filamu ili muisingizie CDM!, sie hatuna mda mchafu kama huo. Wanaofanya hayo matukio wanajulikana (ref Dr. Ulimboka)
 
Tina,

Ujumbe uliotutumia, tumeupata! Umekamilika haujakamilika mimi sijui, ninalolijua mimi ni kuwa ujumbe umepokelewa kama ulivyoutuma.

Pole sana Kibanda kwa yaliyokusibu kama ni kweli, na Asante sana Tina kwa kutuletea habari!
 
Hii ni kudhihirisha tu kwamba wananchi hatuko salama kabisa. Kama wananchi wanavamiwa, wanapigwa, wanajeruhiwa na wengine kuuwawa kila mara na serikali kupitia vfyombo vyake vya dola wameshindwa kabisa kudhibiti hali hiyo ni dhahiri kwamba kama taifa tunahitaji kujipanga na kuchukua mwelekeo mpya kwa ajili ya usalama wetu.

Hii inadhihirisha pasipo shaka yoyote kwamba usalama wa taifa pamoja na jeshi la polisi wameshindwa kabisa kutekeleza majukumu yao ya msingi kwa raia wa nchi hii, na kimsingi hatuoni umuhimu wa kuwa na usalama wa taifa tulio nao kwa sasa kwakuwa wameshindwa kabisa kazi waliyotumwa kuifanya.

Na kwahali hii tunalazimika kuhitaji overhaul ya idara hii nyeti kwa ustawi, usalama na maendeleo ya watanzania. Major overhaul kwa TISS ni kitu kisichoepukika kwa sasa.

Mwita Maranya unatuangusha mkuu, Usalama wa taifa alizikwa nao Mwl. Nyerere, na hivyo kutafuta jina sahihi la TISS ambalo ni UHASAMA WA TAIFA.
 
Hii ni kudhihirisha tu kwamba wananchi hatuko salama kabisa. Kama wananchi wanavamiwa, wanapigwa, wanajeruhiwa na wengine kuuwawa kila mara na serikali kupitia vfyombo vyake vya dola wameshindwa kabisa kudhibiti hali hiyo ni dhahiri kwamba kama taifa tunahitaji kujipanga na kuchukua mwelekeo mpya kwa ajili ya usalama wetu.

......

Acha kujiaibisha kwa kuongea mambo ya ajabu ajabu. Yaani unaona udhaifu wa usalama wa taifa baada ya Kibanda kupigwa na vibaka. Mbona huwa huongei hayo dada zetu wanapoibiwa pochi kila siku pale ''mtego wa panya?''
 
Makubwa tena jamani....mzee wa fastijeti upo??Una cha kujivunia??tanzania si mahali salama tena pa kuishi...
 
Polisi waanze uchunguzi na gazeti la tanzania daima na chadema. kwani hatuelewi ni kwanini alikimbia huko alipokuwa mhariri wa hilo gazeti la mwenyekiti wa chama.

......

Lakini hata wewe pia unaweza kusaidia katika uchunguzi kwa kuanzia kwako inawezekana unahusika kwa namna moja au unawafahamu waliofanya hivyo au umehusika kumteka ili lengo lako lakulichafua gazeti la Tanzania daima litimie!
 
Back
Top Bottom