Absalom Kibanda (Mwenyekiti wa Jukwa la Waharirii) avamiwa na watu wasiojulikana na kujeruhiwa

Tusiwe wepesi wa kuchora mstali na kuhitimisha kwenye jambo linalohitaji fikra pevu na uchunguzi mpana.
Cha kufanya ni kumtakia heri huku uchunguzi ukiendelea.
Watu wana draw such simple conclusion kwa sababu chunguzi nyingi zinazofanyika hazitoa majibu sahihi ya tatizo husika au hazitoa jibu kabisa,.refer utekwaji wa dr.Ulimboka so far majibu ni yep? Kifo cha mwangosi so far jibu ni lipi? ndio mana kwenye case kama hizi speculations zinakuwa nyingi sana
 
Watu wana draw such simple conclusion kwa sababu chunguzi nyingi zinazofanyika hazitoa majibu sahihi ya tatizo husika au hazitoa jibu kabisa,.refer utekwaji wa dr.Ulimboka so far majibu ni yep? Kifo cha mwangosi so far jibu ni lipi? ndio mana kwenye case kama hizi speculations zinakuwa nyingi sana
Mkuu sijui una maana gani unaposema MAJIBU SAHIHI. Tatizo watu wanakuwa tayari na conclusion zilizojengwa na theory or conjecture bila evidence, hata majibu sahihi (matokeo) ya chunguzi yanapotolewa na vyombo husika inakuwa ni vigumu kuamini. Tunahitaji jamii iwe na open eyes.
Taasisi zinazochunguza siyo maraika kwa maana kuwa navyo vinaweza kufanya makosa ya hapa na pale katika chunguzi zao lakini haiwezi kuharalisha kila tukio jamii iwe na majibu bila uchunguzi mbadala.
 
Tusubiri kova atuletee Mkenya mwingine na safari hii sijui ataenda kuungama kwa mama rwakatare!??, wanamvamia nyumbani kwake,wanamteka,wanamjeruhi kisha wanamkimbiza hospitali...!??
 
Kwa jinsi habari ilivyotolewa swala la kutekwa nadhani halipo. Tuseme tu amevamiwa na kujeruhiwa...
 
Ametekwa na kujeruhiwa nyumbani kwake???
How come utekwe hapo hapo na ujeruhiwe hapo hapo na ukimbizwe hospitali?
Je ni nani aliye mteka, na ni naliyemkimbiza hospitali na ni nani aliye muokoa?

Hata mimi nimesshtuka. Haiwezekani mtu kutekwa nyumbani kwake. Labda kavamiwa na majambazi.
 
Dada yangu Tina,
Samahani sana, napata mashaka na usahihi wa hii taarifa yako uliyoileta humu chini ya "habari mpasuko!".
Kwanza hukuweka source, ila kwa vile ni lady, kutoweka source kunahalalisha uwezekano wa connection fulani, kama member tuu mwenzake wa jf, mshirika wake newsroom, rafiki wa kike, mke, etc, that is understandable!, na tumevumilia kwa ahadi ya kupatiwa update!. Lakini tangu ilipopost ile first post, tunaelekea masaa 6 baadaye na hakuna update yoyote!.

Mara baada ya kuisoma humu, nilitembelea zile kumbi ambazo Kibanda huwa anashinda, sikukuta kitu, hii inamaana wewe Tina ndio the first to know hata barazani kwake wasijua, ilhali unadai ametekewa nyumbani kwake?!. Kutekwa ni kuhamisha toka sehemu moja hadi nyingine, kuna kuvamiwa nyumbani na kutekwa, lakini huku kuvamiwa nyumbani, kutekwa, kujeruhiwa na kupelekwa Muhimbili kunatia mashaka sana!.

Mode!.
Nashauri tuweke vigezo maalum vya "habari mpasuko", ili kupata uhakika wa habari mpasuko yoyote ambayo ni shoking, 1. lazima mleta habari atoe source, na kama ni yeye na ameshuhudia then
2. Aweke contact ili modes mumpigie simu ku verify hiyo habari, vinginevyo mtu yoyote anaweza kuleta uzushi wowote na kusail through hivyo kuligeuza jukwaa letu hili adhimu kuonekana kama kijiwe fulani, au genge la wazushi na wote kuonekana hatuna maana!.
 
Kwa kuwa habari yenyewe iliyoletwa hapa haijakamilika...

Sentensi moja tu ambayo naweza kuchangia kwa sasa ni; Mungu amjaalie uzima na urejeo wa afya Ndg Absalom Kibanda.
 
Habari hii kweli hata Clouds FM wamethibitisha asubihi hii wakati kipindi cha kupitia magazet kinaendelea kwa kutoa taarifa iliyowafikia kuhusu swala hilo na wamesema ametekwa na watu wasiojulikana na amelazwa muhimbili baada ya kujeruhiwa.
 
polisi waanze uchunguzi na gazeti la tanzania daima na chadema. kwani hatuelewi ni kwanini alikimbia huko alipokuwa mhariri wa hilo gazeti la mwenyekiti wa chama.

Inasemekana wamemuibia vipesa kidogo na simu, watakuwa vibaka hawa, jamani tuwe makini mateja wametapakaa sana
 
Back
Top Bottom