Absalom Kibanda (Mwenyekiti wa Jukwa la Waharirii) avamiwa na watu wasiojulikana na kujeruhiwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Absalom Kibanda (Mwenyekiti wa Jukwa la Waharirii) avamiwa na watu wasiojulikana na kujeruhiwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Tina, Mar 6, 2013.

 1. Tina

  Tina JF-Expert Member

  #1
  Mar 6, 2013
  Joined: Jul 9, 2007
  Messages: 571
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 45
  Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri na Mhariri Mtendaji wa New Habari, Abdalom Kibanda, amekimbizwa Muhimbili baada ya kuvamiwa na kisha kujeruhiwa na watu wanaosadikiwa kuwa majambazi.

  Watu hao walimvamia na kumtoa katika gari kisha wakampiga kabla ya kumtupa na kumtelekeza umbali mdogo na nyumbani kwake.

  Aliokotwa na majirani na kukimbizwa hospitalini Muhimbili kwa matibabu ya haraka.

  Pamoja na kuumizwa hivyo, hakuna kitu hata kimoja kilichoporwa katika gari lake

  [​IMG]
  [​IMG]

  Taarifa zaidi baadae...
   

  Attached Files:

 2. g

  good2015 JF-Expert Member

  #2
  Mar 6, 2013
  Joined: Feb 4, 2013
  Messages: 888
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Polisi waanze uchunguzi na gazeti la tanzania daima na chadema. kwani hatuelewi ni kwanini alikimbia huko alipokuwa mhariri wa hilo gazeti la mwenyekiti wa chama.
   
 3. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #3
  Mar 6, 2013
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,622
  Likes Received: 7,081
  Trophy Points: 280
  Ooh boy.. tunamuombea apone.. ni matumaini yangu kuwa hili halihusiani na kazi yake ya uandishi.
   
 4. Falcon

  Falcon JF-Expert Member

  #4
  Mar 6, 2013
  Joined: Aug 16, 2010
  Messages: 250
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Funika kombe mwana harasha Apite
   
 5. MD25

  MD25 JF-Expert Member

  #5
  Mar 6, 2013
  Joined: Jan 28, 2012
  Messages: 3,078
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  bila shaka wale mende wa mombasa watakuwa wanakutekenya...
   
 6. H1N1

  H1N1 JF-Expert Member

  #6
  Mar 6, 2013
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 4,227
  Likes Received: 554
  Trophy Points: 280
  Ili uwapoteze lengo polisi,waache kuchunguza na kukugundua, unashauri waanzie mahala pengine ili wewe uendelee kufaidi fedha uliyolipwa kwa ufedhuli huo...
   
 7. IGWE

  IGWE JF-Expert Member

  #7
  Mar 6, 2013
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,806
  Likes Received: 1,385
  Trophy Points: 280
  Mmmmmmh....pole yake...twamuombea apone.
   
 8. sumasuma

  sumasuma JF-Expert Member

  #8
  Mar 6, 2013
  Joined: Jun 23, 2011
  Messages: 332
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35  Mambo ya ulimboka yameanza Tena
   
 9. Horseshoe Arch

  Horseshoe Arch JF-Expert Member

  #9
  Mar 6, 2013
  Joined: Aug 10, 2009
  Messages: 11,442
  Likes Received: 5,220
  Trophy Points: 280
  Tunaelekea wapi...Why Absalom? Anayesimamia anachokiamini,mwanahabari ...Majambazi! Haiingii akilini..kuna dots za kuunganisha hapa..
   
 10. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #10
  Mar 6, 2013
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 38,935
  Likes Received: 30,493
  Trophy Points: 280
  Ametekwa na kujeruhiwa nyumbani kwake???
  How come utekwe hapo hapo na ujeruhiwe hapo hapo na ukimbizwe hospitali?
  Je ni nani aliye mteka, na ni naliyemkimbiza hospitali na ni nani aliye muokoa?
   
 11. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #11
  Mar 6, 2013
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 38,935
  Likes Received: 30,493
  Trophy Points: 280
  Unamfahamu akliye chora zombie kwenye mtihani wa kidato cha nne?
   
 12. Filipo Lubua

  Filipo Lubua Verified User

  #12
  Mar 6, 2013
  Joined: Nov 18, 2011
  Messages: 333
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Kwa hali ya kisiasa ya nchi yetu, na ukinzani uliokuwepo baina ya serikali na Wanahabari, sidhani hapa kuna sababu nyingine zaidi ya hiyo. Absalom Kibanda, amekuwa msumari mkali kwa serikali, tangu alipokuwa Mhariri Mtendaji wa Tanzania Daima na sasa New Habari Coorporation.

  Ikumbukwe kuwa, hadi sasa ana kesi iliyoko mahakamani, kesi ya uchochezi kwa sababu ya makala iliyoandikwa na kamanda Samson Mwigamba na kuchapwa katika gazeti la Tanzania Daima wakati Bwana Kibanda akiwa bado Mhariri wa Tanzania Daima.

  Ngoja tuwasikie watakavyokuja na majibu ya upelelezi wao. Ila Tanzania kwa sasa, si mahali salama sana kwa wanahabari wanaojali uzalendo na weledi wa kazi zao
   
 13. Ng'wamapalala

  Ng'wamapalala JF Gold Member

  #13
  Mar 6, 2013
  Joined: Jun 9, 2011
  Messages: 6,332
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 145
  Tusiwe wepesi wa kuchora mstali na kuhitimisha kwenye jambo linalohitaji fikra pevu na uchunguzi mpana.
  Cha kufanya ni kumtakia heri huku uchunguzi ukiendelea.
   
 14. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #14
  Mar 6, 2013
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,143
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Wee mleta habari, hebu weka mambo sawa. Ametekwa au amevamiwa na majambazi nyumbani kwake? Tuambie wamechukua nini? Ukisema ametekwa ina maana walimpeleka kusikojulikana na kuanza kumshambulia? Hebu toa maelezo yanayojitosheleza bwana.
   
 15. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #15
  Mar 6, 2013
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,487
  Likes Received: 178
  Trophy Points: 160
  yaa, kwa sababu kule CHADEMA ndiko kumejaa majambazi. kama yale yaliyomteka ulimboka. una akili sana.
   
 16. N

  Ninaweza JF-Expert Member

  #16
  Mar 6, 2013
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 7,437
  Likes Received: 1,359
  Trophy Points: 280
  Amevamiwa nyumbani kwake, akatekwa na kukimbizwa hosp.???? Should we wait for another repenting 'Muhindi'?????
   
 17. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #17
  Mar 6, 2013
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 78,164
  Likes Received: 109,901
  Trophy Points: 280
  Kwa nchi yetu ilivyo sasa hivi kuna uwezekano mkubwa kwamba sababu kubwa ya kutekwa kwake inahusiana na kazi zake. Tusubiri tufahamu sababu, lakini inaweza kabisa isijulikane. Mungu amponye haraka.

   
 18. DALLAI LAMA

  DALLAI LAMA JF-Expert Member

  #18
  Mar 6, 2013
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 8,615
  Likes Received: 402
  Trophy Points: 180
  Hili la kutekwa nyumbani kwake linanipa shida..huyu atakuwa mnyatiati wa mashine za watu
   
 19. sumasuma

  sumasuma JF-Expert Member

  #19
  Mar 6, 2013
  Joined: Jun 23, 2011
  Messages: 332
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Yule Mkenya Amerudi tena kuwadhulu na kuwateka watu @ kova
   
 20. f

  fredrickshango Member

  #20
  Mar 6, 2013
  Joined: Jun 3, 2009
  Messages: 12
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mungu akujalie upone haraka utueleze kilichotokea Absolom. Haya mambo ya utekwaji na kujeruhiwa yanachefua sana nchini mwetu kwa sasa.
   
Loading...