Absalom Kibanda amnanga Tundu Lissu, asema Zitto amechezewa mchezo mchafu

Status
Not open for further replies.
Kama Kibanda kajitambua poa,si wengi tupo barabarani tunamsubiri LOWASA yupo MASASI leo,RAISI 2015.Trafiki kibabo kila kona.
 
Utalaaniwa wewe unayetetea wezi,wauza unga,mafisadi,wabakaji na majangili ili uweze kushibisha tumbo tu.unashabikia dhuruma kwa maskini wengi wa taifa hili wanaodhurumiwa haki zao na mafisadi wa ccm,hakika kuna siku utalia kilio cha kusaga meno ASEMA BWANA WA MAJESHI.AMEN
Peleka upumbavu wako huko, mnamwagiabwatu tindikali, mnalisha watu sumu, mnalipua watu na mabomu halafu mnajifanya watu wa mungu? Labda mungu wa mabox.
 
Kibanda kwanza alitakiwa aseme ni nini
chanzo cha kuvamiwa na wale sijui
majambazi,hawa watu wenye nafasi ni kero.


ZZK
Alisema atawataja kwa majina watu wenye
pesa Uswis lakini mpaka sasa kimya,mbaya
anasema mpaka kikao cha Bunge

Kusema kama ushahidi upo hakuhitaji Bunge.

KIBANDA
Alituaminisha kuwa mara afya yake itakapo
nawiri baada ya kuzorota kutokana na kipigo
angewasema wote walumtendea ufedhuri ule

Kibaya na cha ajabu mpaka leo kawa kimya
kana kwamba hajawahi kuumizwa sana
kiasi kwamba angeweza kupoteza maisha

ULIMBOKA
Nae ni vile vile tu.


Sasa kuhusu hili la ZZK bora angekaa kimya.

Matukio yote haya yametekelezwa na chadema kwa ustadi mkubwa
 
Mkuu walaniwe mara ngapi hawa washalaniwa ndo mana kutwa kuongea vitu wasivyoviamini
Utalaaniwa wewe unayetetea wezi,wauza unga,mafisadi,wabakaji na majangili ili uweze kushibisha tumbo tu.unashabikia dhuruma kwa maskini wengi wa taifa hili wanaodhurumiwa haki zao na mafisadi wa ccm,hakika kuna siku utalia kilio cha kusaga meno ASEMA BWANA WA MAJESHI.AMEN
 
Naliona anguko la Zitto Kabwe!


Absalom Kibanda


NAOMBA nianze makala yangu hii kwa
kuwaomba radhi sana wasomaji wa
safu hii, ambao wiki iliyopita
niliahidi kuendelea na hoja yangu
kuhusu tatizo la ushabiki wa
kisiasa, ambalo limekuwa
likiliandama taifa hili kwa miaka
mingi sasa.
Nimelazimika kuomba radhi kutokana
na ukweli kwamba, nimejikuta
nikipaswa kuachana na mada hiyo ya
ushabiki wa kisiasa , baada ya
kuibuka kwa moja ya mambo mazito
katika siasa za ushindani na
hususan katika medani ya ujenzi wa
demokrasia madhubuti ndani ya vyama
vya siasa vya upinzani .
Kikubwa kilichosababisha nifikie
uamuzi huo, ni tukio kubwa na la
kihistoria lililojitokeza wiki hii,
ambalo mwanzo wake uko ndani ya
Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA), ambacho hakuna shaka
kwamba, afya yake ya kisiasa ya
jana, leo na kesho ina mchango
mkubwa katika maendeleo ya kisiasa
katika taifa letu.
Tukio hili ambalo baadhi ya watu
wanaweza wakaliona kuwa ni dogo na
pengine lisilo na maana kubwa, ni
lile la uamuzi wa mwanasiasa
mchanga na kipenzi cha watu, Zitto
Zubeir Kabwe, kuamua kujitoa mhanga
na kugombea nafasi ya uenyekiti wa
taifa wa CHADEMA.
Niseme bayana kwamba, uamuzi huo wa
Zitto, mwanasiasa kijana
aliyejizolea umaarufu mkubwa tangu
alipoingia katika siasa za kitaifa
ndani ya Bunge mwaka 2005,
unaonekana waziwazi kuitikisa
CHADEMA, na kwa kiwango kikubwa
kugusa hisia za viongozi na
wanachama wake na wale walio nje ya
chama hicho.
Kikubwa kinachoonekana kuzusha
maswali vichwani mwa watu wengi,
nikiwamo mimi mwenyewe, ni uamuzi
wa kijana huyo kuamua kugombea
nafasi hiyo pasipo kujali iwapo
Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho,
Freeman Mbowe anayemaliza muda wake
atachukua fomu au la.
Ingawa watu wanaofahamu ujasiri wa
Zitto katika kuchukua maamuzi
mazito tangu akiwa shuleni na
baadaye Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam wanaweza wakawa
hawajashtushwa na uamuzi wa kijana
huyo , ni wazi kwamba, hatua yake ya
safari hii itakuwa imewafanya waanze
kujiuliza mara mbili mbili
kulikoni!
Katika hili la uenyekiti wa taifa
wa CHADEMA, naweza kusema waziwazi
kwamba, hata kwangu mimi ambaye
mara kadhaa nimepata fursa ya
kushiriki katika mawazo na maamuzi
kadha wa kadha ya Zitto, nimejikuta
nikishtushwa na namna alivyofikia
uamuzi huu na kuutekeleza.
Ingawa nilikuwa nikijua japo kwa
sehemu ndogo kuwa, Zitto alikuwa
akipita katika tanuri gumu la
kimaamuzi juu ya ama kugombea
uenyekiti wa CHADEMA au kutogombea,
bado sikuweza kujiaminisha kwamba,
kijana huyu niliyemuunga mkono
wakati wote alipokuwa akisimamia
baadhi ya mambo makubwa ya kisiasa,
angefikia hitimisho la kuwashtua
watu wengi kwa uamuzi wake huu.
Watu wanaojua masuala ya CHADEMA ni
mashahidi wazuri kwamba, uamuzi huu
wa Zitto kuchukua fomu kupambana na
Mbowe ambaye yeye mwenyewe (Zitto),
mara zote amekuwa akimtambulisha
kuwa ni ‘ mentor’ wake wa kisiasa
ndani ya chama hicho cha upinzani,
tena kwa staili ya kumshtukiza,
umesababisha mtafaruku mkubwa wa
mawazo.
Ni wazi kwamba, uamuzi huu wa Zitto
kuchukua fomu , kwa kiwango kikubwa
umekuwa ni wa faraja kubwa kwa wana
CCM, ambao siku zote wamekuwa
wakitaka kuiona CHADEMA
ikisambaratika na kukipa fursa
chama hicho tawala kupumua.
Watu tunaolifahamu hilo kwa ndani,
tunatambua vyema kwamba, kwa CCM na
kwa maofisa usalama wa taifa
waliolelewa katika mfumo wa siasa
za chama kimoja, kuanguka au
kuporomoka kwa uimara wa CHADEMA wa
leo hii, ni jambo la kuliwekea
mikakati na kwa kiwango kikubwa
kulishangilia.
Kwa wana CCM na wapambe wao hao wa
‘kiusalama’, hatua yoyote ya
kuwang’oa kutoka katika madaraka ya
CHADEMA au ya kuwadhibiti watu wa
aina ya Mbowe, Dk. Willbrod Slaa,
John Mnyika na wanasiasa wengine
madhubuti wengi tu wa ndani ya
chama hicho cha upinzani, ni ya
kushangiliwa na kuungwa mkono.
Ni wazi kwamba CHADEMA chini ya
uenyekiti wa Mbowe na ukatibu mkuu
wa Dk. Slaa , pamoja na kuwapo kwa
kasoro zake nyingi za kiutendaji,
kiutawala, kimfumo, kisera na
pengine hata kiitikadi, imepiga
hatua kubwa katika medani ya
ushindani wa kisiasa ndani ya nchi
hii.
Watu wanaofuatilia historia ya
CHADEMA ya siku na miaka ya hivi
karibuni, ni mashahidi wazuri
kwamba, chama hicho kimeweza
kujijengea misingi bora na imara
kisiasa, kiasi cha watu wengi
kukijengea imani na matumaini
makubwa kwamba, kinaweza kikafanya
mambo makubwa wakati wa Uchaguzi
Mkuu wa mwakani.
Dalili hizi za CHADEMA kujijengea
uhalali ambao umejidhihirisha wakati
wa chaguzi mbalimbali ndogo
zilizofanyika katika miaka ya hivi
karibuni, kama zile za Tunduru,
Kiteto, Tarime, Mbeya Vijijini,
Busanda na Biharamulo, zimekuwa
zikikifanya CCM na majemedari wake
wa mikakati kujipanga na kukesha
wakikiwinda, usiku na mchana.
Mawindo hayo dhidi ya CHADEMA
yamekuwa yakijionyesha waziwazi
kupitia katika vyombo vya habari,
ambako kila mara taarifa za kupikwa
na kufinyangwa dhidi ya chama hicho
na viongozi wake, kama akina Mbowe,
zimekuwa zikiandikwa mfululizo na
kupewa uzito mkubwa.
Kwa ustadi mkubwa wa kufinyanga
uongo, mawakala wa CCM wamefanya
kila linalowezekana kumchimba Mbowe
wakitumia falsafa ya Kibiblia
isemayo; ‘Mpige mchungaji, kondoo
watawanyike’ ili kufanikisha malengo
yao haya ambayo matokeo yake
hayatamgharibu mwenyekiti huyo pekee
yake, au chama anachokiongoza, bali
mafanikio yote tuliyopata
kidemokrasia kama taifa.
Ni kwa sababu hiyo basi, Mbowe
amepewa sifa mbaya kila wakati,
akihusishwa na ukabila, ufisadi,
udikteta, ubinafsi na kila aina ya
sifa mbaya, lengo likiwa ni lile
lile la kukivuruga chama hicho na
kudumaza nguvu ya kiushindani ya
vyama vya upinzani.
Mbinu hiyo haramu ya kutumia vyombo
vya habari kumchafua Mbowe
iliposhindikana, hata wakati ule
ikafikia hatua ya kutumia hoja za
aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa
Taifa wa chama hicho, Chacha
Wangwe, mawakala hao wa CCM wakaja
na mbinu nyingine mbadala.
Mbinu hii haikuwa nyingine bali ile
ya kujaribu kuwagombanisha na
kuwachonganisha viongozi wa kitaifa
wa chama hicho kwa mbinu na staili
tofauti.
Wakati fulani mwaka jana, Zitto
alipofanya mahojiano na gazeti hili
na kuulizwa kuhusu kusambazwa kwa
habari za viongozi wa CHADEMA
kugombanishwa, alikiri kulifahamu
hili.
Wakati huo (Desemba mwaka 2007),
vyombo kadhaa vya habari vilianza
kuandika habari za kumpamba Zitto,
zikimsifu kwa kuwa mwanasiasa
kijana machachari na ambaye uwezo
wake wa kiuongozi ulikuwa ukikizidi
chama hicho na pengine viongozi
wengine wa chama hicho.
Taarifa hizi za vyombo vya habari
zilinikutanisha na Zitto na
tukazijadili naye kwa muda mrefu
kabla ya wote wawili kukubaliana
kwamba, zilikuwa na lengo la
kukihujumu CHADEMA na kuua dhana
nzima ya upinzani hapa nchini.
Tulipofikia hatua ya kukubaliana
naye, alifanya mahojiano na gazeti
hili na akatoa tamko zito ambalo
kwa kiwango kikubwa lilisababisha
mawakala wa CCM kuachana na ajenda
hiyo. Kwa maneno yake mwenyewe
wakati huo akirejea taarifa za
vyombo mbalimbali vya habari
alisema: ‘‘Tumegundua kuwapo kwa
juhudi za makusudi za kutaka
kutugombanisha CHADEMA. Hiki ni
chama makini, kimezibaini njama
hizo na kwa hakika hakiwezi
kusambaratishwa.
“...CHADEMA ndiyo imenipa umaarufu
mimi… mimi si maarufu kuliko chama.
CHADEMA ni taasisi, ni chama
ambacho kina misingi ya uanzishwaji
wake.
“…(Wanasema) eti nilishinda kwa
umaarufu wangu binafsi, si kweli.
Niligombea ubunge nikitokea shule,
sikuwa najulikana. Nilikuta
‘grassroots network’ ya chama,
(chama) hakikujengwa na mimi.
“CHADEMA ilijengwa na uongozi
uliokuwepo, nilikuta uongozi
‘intact’ (imara) . Katika kila
kijiji kulikuwa na uongozi na hata
katika vitongoji vyote. Wakati
naingia kugombea ubunge kulikuwa na
wanachama wa CHADEMA wenye kadi
wanaofikia 10,800 katika jimbo
zima. Hawa sikuwatafuta mimi,
niliwakuta na ndio waliofanikisha
ushindi wangu.
“...Katika mazingira kama haya
utasemaje kuwa mimi ni maarufu
kuliko chama wakati chama ndicho
kimenipa umaarufu?
“...CHADEMA ni chama ambacho
wenyeviti wake wastaafu wanaendelea
kuenziwa na kuhudhuria vikao vyote
vya chama… ‘institutional memory’
ipo kuliko katika vyama vingine vya
upinzani.
“...Alipohama (Dk. Aman Walid)
Kabourou, wengi walidhani ndiyo
mwisho wa CHADEMA Kigoma, lakini
leo hii CHADEMA ni moto Kigoma
kuliko ilivyokuwa awali.”
Ni jambo la ajabu kwamba , karibu
miaka miwili tangu Zitto mwenyewe
akiri kutambua kuwapo kwa njama
hizo za kumkosanisha na viongozi
wenzake na pengine kukihujumu chama
chao, anaonekana akiingia katika
mtego ambao miaka kadhaa iliyopita
ulipata kukinasa chama kingine cha
NCCR Mageuzi kiasi cha kukifanya
leo hii kushindwa kufurukuta hata
kufananishwa na baadhi ya watu kuwa
ni sawa na shirika lisilo la
kiserikali (NGO).
Ni jambo la kusikitisha sana
kwamba, leo inapofikia hatua ya
mwanasiasa kijana aliyekuwa
akionekana kuwa moja ya mazao ya
kuigwa ndani ya kambi ya upinzani
tangu kukwama kwa akina James
Mbatia, Mabere Marando, Augustine
Mrema na wenzao wengine wengi,
akifuata mkondo ule ule, basi ni
wazi Watanzania wanaweza wakajikuta
wakilazimika kukata tamaa zaidi na
zaidi.
Ingawa ni kweli kwamba pengine
nyuma ya Zitto wako watu wengi
ndani ya CHADEMA na nje, waliojitoa
mhanga kumuunga mkono katika
mapambano haya, mwanasiasa huyo
anapaswa kutambua wazi kwamba,
uamuzi wake huu wa sasa,
unamuandalia anguko ambalo si mimi
wala mwingine yeyote atamwepusha
nalo .
Ni wazi kwamba katika umri wa miaka
33 aliyonayo Zitto na tena akiwa na
akili zinazochemka na afya njema,
mwanasiasa huyo mchanga anayo fursa
kubwa mbele ya safari ya kuwa
mwenyekiti wa taifa wa CHADEMA na
Mungu akipenda kupanda zaidi ya
hapo alipo leo.
Anapaswa kujifunza kuwa na subira
waliyonayo vijana wengi ndani ya
CCM na serikalini, ambao pamoja na
kuwa na fursa nyingi za
harakaharaka, wameamua kuwa
watulivu na wenye subira , wakiwa na
uhakika kuwa, wakati wao utafika .
Wakati atakapokuwa akiyatafakari
hayo , Zitto anapaswa kuyarejea
maneno aliyoyatoa Rais Jakaya
Kikwete siku alipoteuliwa kuwa
mgombea urais kwa tiketi ya CCM
pale Dodoma, Mei mwaka 2005,
alipokiri yeye mwenyewe kwamba
lilikuwa jambo jema kwake kuukosa
urais mwaka 1995.
Naliona anguko la kihistoria la
Zitto.
 
Kibanda kwanza alitakiwa aseme ni nini
chanzo cha kuvamiwa na wale sijui
majambazi,hawa watu wenye nafasi ni kero.


ZZK
Alisema atawataja kwa majina watu wenye
pesa Uswis lakini mpaka sasa kimya,mbaya
anasema mpaka kikao cha Bunge

Kusema kama ushahidi upo hakuhitaji Bunge.

KIBANDA
Alituaminisha kuwa mara afya yake itakapo
nawiri baada ya kuzorota kutokana na kipigo
angewasema wote walumtendea ufedhuri ule

Kibaya na cha ajabu mpaka leo kawa kimya
kana kwamba hajawahi kuumizwa sana
kiasi kwamba angeweza kupoteza maisha

ULIMBOKA
Nae ni vile vile tu.


Sasa kuhusu hili la ZZK bora angekaa kimya.

ULIMBOKA ameingiaje hapa?Halafu nani alikwambia kwamba mtekwaji lazima amtambue mtesaji na mtekaji wake?Omba yasikukute!
 
Wote ni walewale tu. Kuna wakati Zitto alijulishwa kuwa ndani ya chama chake kuna wabaya wake na walifanya njama za kumuwekea sumu, aliwaruka na kuwafedhehesha wale waliompigania. Akawapamba na viongozi wake. Leo anatuambia ana maadui wanaomtafuta siku nyingi chamani.

Kibanda anawajua waliomdhuru na sababu ya kifanya hivyo ameamua kuwalinda iko siku nae ataropoka tu.
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom