Absalom Kibanda aaga rasmi Tanzania Daima

Status
Not open for further replies.

MADORO

Senior Member
Nov 12, 2011
198
117
Kama ilivyoanza kama tetesi ndani ya JF (ref https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...r-wa-new-habari-kuanzia-disemba-1-2012-a.html ),

Aliyekuwa mhariri mtendaji wa gazeti la Tanzania Daima, Absalom Kibanda, leo ameaga rasmi na kuachia nafasi yake mhariri mtendaji, kwa maelezo kuwa anaenda kujiunga na kampuni ya New Habari Corporation 2006, inayochapisha zaidi ya magazeti manne hapa nchini.

Akiongea na wafanyakazi wa gazeti la Tanzania Daima leo asubuhi, Kibanda alisema sababu kubwa ya kuondoka hapo ni kwa ajili ya kutafuta changamoto mpya katika majukumu yake ya uandishi.

Amewataka waandishi wa gazeti wanaobakia waendelee kufanya kazi kwa bidii, kwa ajili ya kulikomboa taifa kwa kuuanika ukweli pasipo kuogopa.
 
Karibu nyumbani Kinana Kafanya kazi

Uchumba ulianza hivi

images



images


images



Welcome Meeeeeeeeeeeeennnnnnnnnnnnnnnnn:target::target::target::target::pop2::pop2::pop2::pop2::pop2:
 
Hakuna anayeongelea maslahi hapa...wakati wengi wetu humu tushaacha kazi moja na kufuata nyingine yenye maslahi zaidi...kila la heri Kibanda!
 
Last edited by a moderator:
Bado , ataenda Fahamu baada ya kikao kizito kilichofanyika znz , ajenda kuu ni kuishambulia CDM kila kukicha, mark my words.....l
 
"Tukiwakamata Mafisadi, Uchumi wa nchi yetu utayumba".....Mizengo Kayanza Peter Pinda, Bungeni 2011

Acha uyumbe kwa muda, lakini baadaye utakuwa stable kama mwamba. Siku za mafisadi zinahesabika!

Kichaka chao, I mean chama chao, walimojihakikishia usalama wao kitakaposambaratishwa rasmi hakutakuwa na wa kusalimika!

Na wameanza kugombea fito wenyewe!

Siyo mbali sana Discipline itarudi Tanzania!
 
Mtu kuhama kampuni au muajiri sio ajabu. Tabu ni vile kulazimisha bifu na muajiri wako wa sasa ili upate sababu ya kuhama.

Kibanda pale ulichemsha kaka!!
 
Last edited by a moderator:
Hiyo ndiyo mikakati ya mtawala kila siku, kunyamazisha wanaoichokonoa. Si unamcheki maalim seif sharrif hamad alivyoingizwa kwenye payroll na kuikaanga cuf. Siku hizi kimyaaaa kama hayupo vile.
 
Kweli kazi ya uandishi wa habari Tanzania haina tofauti na uuza baa. Jamani Kibanda kama aliyokuwa akiandika yalikuwa yanatoka moyoni, huko ataandika nini au ni wale wale akina Salva Rweyemamu. Kweli namna hii hatuwezi kuendeleza nchi yetu. Yaani kila mtu anapigwa bei kienyeji hivi hivi.
 
Nchi yetu hii tamu kweli kweli! Nataka nione zile makala motomoto za kuichachafya serikali na CCM zikitoka kwenye magazeti ya New Habari! Ndugu Mwita Maranya yametia yaliyonenwa na manabii
Hawawezi mkuu labda iwe ni mkakati wa kambi yao.Pengine mkakati wa kumshughulikia Mbunge wa mtama na kiongozi ajaye wa upinzani (baada ya uchaguzi mkuu 2015)Sasa huko alikoenda kuna changamoto gani?
 
Kweli kazi ya uandishi wa habari Tanzania haina tofauti na uuza baa. Jamani Kibanda kama aliyokuwa akiandika yalikuwa yanatoka moyoni, huko ataandika nini au ni wale wale akina Salva Rweyemamu. Kweli namna hii hatuwezi kuendeleza nchi yetu. Yaani kila mtu anapigwa bei kienyeji hivi hivi.

Waandishi wengi hawana tofauti na wansiasa! Ukiona anaongea hadi povu linamtoka utaona huyu ndiye kumbe hana chochote!
 
Aliyekuwa mhariri mtendaji wa gazeti la Tanzania Daima Absalom Kibanda, leo ameaga rasmi na kuachia nafasi yake mhariri mtendaji, kwa maelezo kuwa anaenda kujiunga na kampuni ya New Habari Corporation 2006, inayochapisha zaidi ya magazeti manne hapa nchini.

Akiongea na wafanyakazi wa gazeti la Tanzania Daima leo asubuhi, kibanda alisema sababu kubwa ya kuondoka hapo ni kwa ajili ya kutafuta changamoto mpya katika majukumu yake ya uandishi.

Amewataka waandishi wa gazeti wanaobakia waendelee kufanya kazi kwa bidii, kwa ajili ya kulikomboa taifa kwa kuuanika ukweli pasipo kuogopa,

sababu kuntu hii ila hutumiwa sana na waajiriwa wanaoenda sehem nyingine,ingawa moyon huwa ni GREEN PASTURE
 
Kibanda ni mchumia tumbo siku nyingi hivo sishangai kama anaweza kuacha jukumu zito alilokuwa amejitwika kwa manufaa ya wengi na kwenda kuliko na maslahi zaidi!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom