Aboud Jumbe na Siasa zetu

platozoom

JF-Expert Member
Jan 24, 2012
9,366
11,154
Sote tunajua amefariki leo.
Baada ya kifo chake mengi yamezungumzwa. Wapo wanaolaumu Mzee Jumbe `kutiwa kizuizini nyumbani kwake`, wengine kumsifu kwa uongozi wake na wengine kuilaumu Serikali kwa kumtelekeza.

Hili jamvi kubwa. Najua Mzee Jumbe alikuwa na uwezo/akitaka wa kwenda popote pale. Hakughasiwa na Serikali akiwa Maskani yake kilomita zisizozidi 15 toka Ikulu ya Rais wa JMT.

Alikula, kuishi na kuyaishi maisha yake ndani ya Tanzania "bara" pasipo bugdha. Aliamua kuchagua maisha ya kumcha Mungu na kuachana na Siasa active.

Iweje leo ilaumiwe Serikali kwa hayo? Mbona wengi wamepita kwenye tanuri la Kisiasa na wakachukulia kama mapito!

Hivi kutiwa Jumbe kunakoitwa kizuizini ni sawa na akina Han Su ki wa Burma au Mandela?

Ni ipi legacy ya Jumbe Zanzibar? Kwa Mtu ambaye alipigania Serikali tatu lakini baadaye akaishi Tanganyika kwa amani. Wakati flani Ahmed Rajabu akiandika kuwa Mzee Jumbe akiwa madarakani aliagiza pajama lake alilosahau Zanzibar akiwa Saudia!

Najiuliza tu, sijatekwa na emotions
 
Madhila aliyopitia Mzee Jumbe ni Makubwa kuliko ya kuwekwa kizuizini Kigamboni.

Muda huu tujadili hoja za Wasomi wa Zamani wa Makerere University, Aboud Jumbe dhidi ya hoja za Nyerere tujue nani alikuwa kiona Mbali kwa kuangalia muktadha wa leo. Nyerere aliamini serikal Mbili Jumbe akiamini Tatu!
 
Madhila aliyopitia Mzee Jumbe ni Makubwa kuliko ya kuwekwa kizuizini Kigamboni.

Muda huu tujadili hoja za Wasomi wa Zamani wa Makerere University, Aboud Jumbe dhidi ya hoja za Nyerere tujue nani alikuwa kiona Mbali kwa kuangalia muktadha wa leo. Nyerere aliamini serikal Mbili Jumbe akiamini Tatu!
Tueleze madhila gani aliyopata.
Hapa nilikuwa najaribu kuangalia waliogombana na Serikali katika Nchi nyingine na kilichowapata.

Nakumbuka Mzee Jumbe akiwa Uwanja wa Taifa kuaga Mwili wa Mwalimu Nyerere, picha haijaondoka mpaka leo japo umri ulikuwa mdogo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom