Abood wamefika pabaya sasa...

DSC04710.JPG

MAHUTA EXPRESS.....MASAA KADHAA TU UPO MAHUTA TOWN!!! Hii inapitia junction moja karibu na nyangao pale..nikumbushen hapa
 
Mkuu hiyo safari ni moja kwa moja au utarudi tena mjini.... dah maana maisha ya hapa dar sii mchezo watu wanaukimbia mji kila kukicha

Mjini shule, shamba kilimo. Niko jijini tangu 80's, siwezi give up that easily! Ila alama za nyakati zikitaka tuhame tutahama...
 
nimewahi panda shabiby kwenda Dodoma nikiamini yote yako bomba, ebwana eeh, nilijuta. Ile kuingia ndani ya basi tu nikashuka na kuwaomba warudishe hela yangu kwa jinsi lilivyochoka tofauti na nilivyoambiwa kabla. waligoma tukaondoka kwa mwendo mdogo mdogo likiwa linakoroma njia nzima. kufika Gairo likaharibika kabisa na hatukuambiwa bali wahusika walipotea zao. Tulipiga simu zilizopo ktk tiketi tukapewa majibu ya kuridhisha japo msaada bado hatukuuona. baada ya saa 1 pasipo majibu wala kuwaona ndipo tulipovamia kituo na kuwabana wenye ofisi ya Gairo tukaelezwa wanamtafuta fundi aje atengeneze. hawakutaka kufungua buti tuchukue mizigo tujitafutie usafiri mwingine. Baadaye tuliendelea na safari na likaharibika km 4 toka gairo stand. toka saa 6 Dsm tulifika Dom saa 5 usiku. ASiku hizi nisipopata luxury mabasi yao mengine sipandi. ni mabovu mno huenda fedha nyingi wametumia ktk chaguzi hata kushindwa kutengeneza magari yao.
 
Next time kama unaenda Mbeya na unataka kupanda aboud, basi panda aboud linaloelekea Tunduma kisha utashuka Mbeya.
La Tunduma ndio zima maybe kwa sababu safari yake ni ndefu zaidi, mimi nina uzoefu nalo.
 
Ila mwendo wake, usiwe na presha!
 
Nimekuwa nikisafiri na mara nyingi ninaona kuna mapungufu mengi katika huduma ya usafirishaji na inaonekana kama serikali inashindwa hata kusimamia na kila mfanyabiashara kujifanyia anavyotaka. Serikali ilipaswa kuweka standard za mabasi na kuwaelimisha wananchi kuhakikisha kwamba mbasi wanayopanda yanakidhi hizo standard na huduma zitolewazo.

Pale Ubungo basi terminal ni uhuni mtupu; mpaka leo nashindwa kupata majibu kazi ya WAPIGA DEBE ni nini? hivi mpaka leo watanzania hatujui kusoma na kuandika? mpaka awepo mtu wa kukuelekeza ofisi za basi fulani; wale ni wezi na ndiyo mara nyingi wanapotosha abiria. Siku moja nilikuwa na safari ya kwenda Arusha, nikamwagiza kijana kunikatia tiketi ya Dar Express, alipofika Ubungo mpiga debe mmojawapo akamweleza kwamba mabasi yote ya Dar Express kwa siku hiyo yatakuwa katika matengenezo eti wanabadilisha milango na aliitwa mpiga debe mwingine ambaye alionekana kuvaa uniform za Dar express na kuthibitisha kauli hii. Walimpeleka ofisi ya basi jingine (nimesahau jina lake) na kumpatia tiketi. Aliponiletea hiyo tiketi nilifahamu hayo mabasi ni mabovu na nilishaanza kuona safari itakuwa mbaya, siku ya safari nilisubiri basi njiani kwa masaa 2 baadae nilipopiga simu nikaelezwa wamekamatwa na sasa nitasafiri na basi la sai baba ambalo ni 2 & 3; safari likuwa mbaya kwani nilisafiri na basi ambalo sikulipenda na haliendani na thamani ya fedha nilizolipa.

Tuunganishe nguvu kuhakikisha kwamba:
  • wapiga debe katika vituo vya mabasi wanaondolewa na badala yake kuwe na mawakala wa kuuza tiketi na wote wawe na ofisi.
  • Serikali kuweka standard za mabasi na wananchi kupatiwa elimu ya kutosha.
  • Wananchi kuelimishwa juu ya haki zao za msingi katika huduma ya usafirishaji

Huu ni mtazamo tu!
 
Next time kama unaenda Mbeya na unataka kupanda aboud, basi panda aboud linaloelekea Tunduma kisha utashuka Mbeya.
La Tunduma ndio zima maybe kwa sababu safari yake ni ndefu zaidi, mimi nina uzoefu nalo.

Yeeah, hata mimi nimeliona. Lina uafadhali kidogo!
 
nakutakia safari njema, check sana kona za Iyovi mle. wendawazimu wanalala nazo kama hawana akili nzuri. usafiri wa uhakika angalau ni Dar express, sema nao nia hiyo ya mbeya hawana magari. wakati unarudi sasa chukua Happy Nation wanaziita "sauti ya manka" ni balaaa hizo, chassis za lori
 
Mwenzangu kukimbizwa hata sitaki, nikirudi nitachukua Sumry, tena ile high class!
 
Back
Top Bottom