Abolish death penalty now! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Abolish death penalty now!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kevo, Oct 11, 2008.

 1. Kevo

  Kevo JF-Expert Member

  #1
  Oct 11, 2008
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,332
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Death Penalty was brought about in Tanzania by the colonialists 63 years ago; Tanzania incepted it under the provisions of the Penal Code, Cap. 16 and started to enforce it as from 28th September 1945 to date; as of 2008, 133 countries around the world has abolished the death penalty in law or practice, while only 64 countries (Tanzania and Zanzibar inclusive) still retain and use it. Since 1961 to March 2008 total number of 2,562 people were sentence to death, so far total of 238 Convicted Persons (9.3% of the Convicted persons) have been hung to death since the year 1961, out of whom 232 are men and the rest (6 of them) are women. While those who brought it, have abolished it and we still retaining it.

  Reasons for Abolishment of the Death Penalty

  * It is the ultimate, irreversible denial of human rights.

  * There is a possibility of innocence people on the Death Row.

  * It is NOT a Deterrent to Crime as numbers of crimes are on increase.

  * It is “Cruel and Unusual Punishment”.

  * It costs more than Life in Prison without Parole.

  * It is a barbaric remnant of uncivilized society.

  * It is immoral in principle, and unfair and discriminatory in practice because the burden of capital punishment falls upon the poor, the ignorant and the underprivileged members of society.

  * Death penalty laws falsely convince the world public that governments have taken effective measures to combat crime and homicide. In reality, such laws do nothing to protect human society or our communities from the acts of dangerous criminals.

  * It does not restore a person killed.


  Action to be taken by the Government of Tanzania

  * Ratification and domestication of the Second Optional Protocol to the International Covenant on Civil and Political rights (1989) which calls for abolition of the death penalty.

  * The amendment of the provisions of Penal Code, Cap. 16, which provide for the Death Penalty.


  Alternative Punishments
  In stead of it, life imprisonment without the possibility of parole plus restitution shall serve the purpose. This alternative not only costs much less than capital punishment, but also keeps the criminal in jail for the rest of his/her life - so he/she cannot return back to society. Restitution means that while the prisoner is in jail, he/she will be put to work - with all the money made going to the family of the victim.
   
 2. Kevo

  Kevo JF-Expert Member

  #2
  Oct 11, 2008
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,332
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Death Penalty has taken a toll in our country and today at the University of DSM great Human Rights Activist like Prof Haroub Othman,Issa Shivji and the the president of TLS among others had a forum discussing this critical issue against human justice.
  So we are all asked to participate and create awareness in our society against this issue.
  The Legal and Human Rights Centre is planning a trip to Climb Mount Kilimanjaro and they would like to appeal to all CSOs as human rights followers to encourage its staff, members and partners to participate in the campaign and in the mountain climbing for human rights and women human rights.
  It will be only 350,000 TShs and you can register at their website!

  http://www.humanrights.or.tz/index.php?option=com_eventlist&Itemid=93&func=sharchive&categid=5
   
 3. Nkamangi

  Nkamangi JF-Expert Member

  #3
  Oct 11, 2008
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 642
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kevo, I need a good lawyer in Arusha, any recommendations huko uzunguni? hate that description
   
 4. Calnde

  Calnde JF-Expert Member

  #4
  Oct 12, 2008
  Joined: Oct 7, 2008
  Messages: 1,373
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0

  I assure this to you.Mawala Advocates.
   
 5. Calnde

  Calnde JF-Expert Member

  #5
  Oct 12, 2008
  Joined: Oct 7, 2008
  Messages: 1,373
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Kevo,You are a good thinker.If you use your law skills effectively,not like 'vijisenti',You may reach far.ofkozi you can make it.
   
 6. K

  Kithuku JF-Expert Member

  #6
  Oct 12, 2008
  Joined: Nov 19, 2006
  Messages: 1,395
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  Inategemea na shida uliyo nayo. Kama ni shitaka la ujambazi waone Medium Mwale na Loom Ojare, ndio specialists wa fani hiyo. Hata kama jambazi akikamatwa "red-handed" kwenye tukio la ujambazi katika mapambano ya risasi na polisi, hawa jamaa huwa wanamtoa jambazi kama vile kasingiziwa vile!
   
 7. K

  Kithuku JF-Expert Member

  #7
  Oct 12, 2008
  Joined: Nov 19, 2006
  Messages: 1,395
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  Na kuhusu mada iliyoko hapa, msimamo wangu ni kwamba hukumu ya kifo inapaswa iendelee kuwapo nchini kwa sababu kuna watu wanaoistahili. Sasa mnataka hukumu ya kifo iondolewe, hao wanaostahili hukumu hiyo tuwafanyeje? Tuwachekee tu wakati wanatuumiza na kutuulia ndugu zetu? Hukumu ya kifo iwepo kwa ajili ya kuiasa jamii na kuondoa mijitu isiyotakiwa (sawa na kung'oa magugu shambani na kuyachoma moto). Yaani unataka jitu linalovamia nyumbani kwako na kuua wanao, kubaka mkeo nk lipelekwe jela likaendelee kulishwa na kutunzwa bure kwa gharama zako (kodi yako) wewe uliyedhurika? Hapana! Watu wa namna hii wafutwe kwenye uso wa dunia. Hukumu ya kifo idumu kwa wanaoistahili.
   
 8. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #8
  Oct 12, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Msingi wa hukumu ya kunyongwa ni kisasi. Ndiyo miongoni mwa sheria ambazo hazina lengo la kuadhibu ili mtu akome, ajifunze na asirudie tena. Hivyo ni sheria inayotolewa kwa msingi wa kisasi. Now, kisasi ni sehemu ya maisha ya watu.
   
 9. Kevo

  Kevo JF-Expert Member

  #9
  Oct 12, 2008
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,332
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Well I can suggest Mawalla and Associates Advocates.They are well covered and experienced in legal matters.
  They are situated near Burka Coffee Estate.
   
 10. Kevo

  Kevo JF-Expert Member

  #10
  Oct 12, 2008
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,332
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  So you suggest death penalty iendelee?kwa sababu its all about kisasi which is a part of lives za binadamu?
   
 11. Kafara

  Kafara JF-Expert Member

  #11
  Oct 12, 2008
  Joined: Feb 17, 2007
  Messages: 1,392
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  kweli adhabu ya kifo haipunguzi uhalifu.

  mara nyingi mhalifu anapodhamiria kutenda ouvu hafikirii adhabu inayoambatana na kosa/uovu atakaoutenda bali anapima uwezekano wa kukamatwa kwake. kama akiamini kwamba uwezekano wa kukamatwa ni mdogo basi atatekeleza ualifu wake na kama akiona uwezekano wa kukamatwa ni mkubwa basi ataacha au atasubiri wakati muafaka.

  kutokana na ukweli huo ndio maana pamaoja na kuwepo na adhabu ya kifo bado uhalifu wa kinyama bado unaendelea kuwepo. hivyo basi dawa ni kujenga mazingira ambayo wahalifu wataona uwezekano wa kukamatwa ni mkubwa na hivyo kuwafanya wasite kufanya uhalifu wao.

  labda ndio maana wahalifu wanajitahidi sana kutowadhuru polisi au kuwafanya polisi walengwa wa uhalifu wao kwani wanafahamu fika madhara ya kuwadhuru polisi kwani huwa hapakaliki.
   
 12. K

  Kithuku JF-Expert Member

  #12
  Oct 12, 2008
  Joined: Nov 19, 2006
  Messages: 1,395
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  Mkuu hii ni adhabu pekee ambayo inapotolewa kunakuwa na uhakika kuwa mhalifu huyo hatarudia tena! Si kila mhalifu anayepaswa kurekebishwa, wengine wanapaswa kuwa "eliminated". Hata tulipofundisha mashuleni kuna wanafunzi wakosaji tuliwaadhibu kwa viboko, kazi za ziada nk (ili wajifunze), lakini kuna wengine tuliwafukuza shule kabisa (wasiwepo eneo hilo, hawafai). Hata katika maisha halisi kuna watu ambao hawafai kuwepo miongoni mwa binadamu yeyote, sasa hao kuwafunga gerezani ni sawa na kuwatukana walioko gerezani kuwa wako sawa nao. Wanaostahili hukumu ya kifo waendelee kupata hukumu hiyo, watu waishi kwa amani.
   
 13. K

  Kithuku JF-Expert Member

  #13
  Oct 12, 2008
  Joined: Nov 19, 2006
  Messages: 1,395
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  Kwamba adhabu ya kifo haipunguzi uhalifu hilo sina uhakika nalo, linahitaji utafiti wa kina na wenye methodolojia nzuri kulithibitisha. Lakini moja ambalo nina uhakika nalo ni kwamba adhabu hiyo inapunguza wahalifu. Iendelee na tena idumu.
   
 14. Kafara

  Kafara JF-Expert Member

  #14
  Oct 12, 2008
  Joined: Feb 17, 2007
  Messages: 1,392
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  labda kuna tafiti zinazoonyesha adhabu ya kifo inapunguza wahalifu hilo nami sijui. ila naamini nchi nyingi ambazo hazina adhabu ya kifo na ambazo zimeboresha vyombo vyao vya kupambana na uhalifu wameweza kwa kiasi kikubwa kupunguza idadi ya wahalifu watendao makosa ambayo yangewapeleka kupata adhabu ya kifo kama ingekuwepo katika nchi hizo. kwa kweli sina data za kuthibitisha hili ila ni uthibitisho wa kimaisha tu.
   
 15. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #15
  Oct 13, 2008
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Una hakika gani kuwa ni wanaostahili pekee ndio wanaonyongwa? Katika nchi kama ya kwetu ambapo kila mmoja anakiri kuwa kubambikiwa kesi ni kawaida!

  Tatizo la hukumu ya kifo ni kuwa ni final na hakuna mahali pa kusahihisha makosa. Hata wamarekani wameona hilo na wanaangalia upya hukumu hii.

  Mpaka hapo tutakapokuwa na uwezo wa kuhakikisha kuwa hakuna asiyestahili atapewa hii hukumu, hukumu hii inastahili kupingwa.
   
 16. Ochu

  Ochu JF-Expert Member

  #16
  Oct 13, 2008
  Joined: May 13, 2008
  Messages: 972
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  katika kupinga adhabu hii nimekutana mahakani na mwanasheria wakili Alex Mgongolwa na wakili Fulgence Massawe wakifungua shauri la kikatiba kupinga adhabu ya kifo kwa niaba ya Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu na Tanganyika Law Society. kulingana na maelezo yao shauri hili limepewa namba 67/2008. nitakuwa nawasiliana nao wanipe taarifa jinsi kesi inavyoenda.
   
 17. Ochu

  Ochu JF-Expert Member

  #17
  Oct 13, 2008
  Joined: May 13, 2008
  Messages: 972
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  it depends the nature of the case and they are not good in litigations.they are so selective. try Maro Advocates
   
 18. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #18
  Oct 15, 2008
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Isome yote hapa:http://www.nytimes.com/2008/10/15/washington/15execute.html

  Hata Marekani kuna utata kuhusu haki kutendeka kwenye hukumu ya kifo. Hata huko, cha msingi, kama ilivyosemwa awali, ni kisasi.

  Hii hukumu haitakiwi kuwa na nafasi katika jamii inayojihesabu imestaaribika.
   
 19. K

  Kithuku JF-Expert Member

  #19
  Oct 15, 2008
  Joined: Nov 19, 2006
  Messages: 1,395
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  Kwa hiyo unamaanisha wauaji ndio wanaotakiwa kupewa nafasi katika jamii "iliyostaarabika"? Ni "ustaarabu" gani huo unaozungumzia? Jitu lifanye ujambazi, mauaji, tulichekee tu ati kisa "ustaarabu"? Huo si ustaarabu, labda tuite "udebwedo"! Anayeua apewe hukumu ya kifo, cha msingi kesi ziendeshwe kwa haki, asisingiziwe mtu, basi.
   
 20. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #20
  Oct 15, 2008
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Kithuku. Ukiweza kunihakikishia kuwa wote watakaonyongwa ni kweli wauaji na majambazi, nitakuelewa. Ukiweza kunihakikishia kuwa hakuna jambazi na muuaji atakaepuka hii adhabu, nitakuelewa. Kwa jinsi ilivyo, wengi wa wanaonyongwa ni wale wasio na uwezo wa kifedha au influence au wasio na hatia (wamebambikiwa). Mpaka hapo tutakapokuwa na uwezo wa kimungu wa kumtambua mwenye haki na asiye na haki, hii adhabu tumwachie yeye.

  Hakuna anayedai kuwa wauaji na majambazi waangaliwe tu. la, hasha, waadhibie tu. Wafungwe kifungo cha maisha na adhabu nyingine. Na kama tutagundua kuwa alionewa tu, tutamwomba radhi, na kumuachia. Hauwezi kufanya hivyo kwa uliyemnyonga.

  Hatujafika hapo tunapoweza kusema kesi zinaendeshwa kwa haki. Hatujafika hapo tunapoweza kusema watu hawabambikiwi kesi. Yote haya unajua yapo, lakini bado unadai wanyongwe! Waliokuwemo na wasiokuwemo. Iko kazi.
   
Loading...