Abnormal menstrual bleeding: Je nini chanzo na ni kwa namna gani tunaweza kutibu tatizo la kutokwa damu ukeni (kipindi cha hedhi) bila kukata?

Jul 21, 2019
52
64
Habari za wakati huu wana JF!

Ni matumaini yangu kuwa mko wazima na bukheri wa afya. Naomba kuuliza , ni nini chanzo cha kutokwa na damu ukeni (menstrual bleeding) kwa muda mrefu bila kukoma tukiangalia sanasana kwenye mazingira yetu ya kitanzania, na je tiba yake ni ipi?

Mwenye kufahamu naomba msaada.
 
Hedhi Kutoka Muda mrefu​

hedhi kutoka muda mrefu

hedhi nyingi kwanini hedhi yangu inachukua siku nyingi kuisha? Kikawaida hedhi huchukua siku tatu mpaka saba kuisha. Hedhi inayochukua zaidi ya siku saba tunachukulia kama ni hedhi ya muda mrefu sana. Kitaalamu hedhi kutoka muda mrefu zaidi ya siku saba huitwa menorrhagia.

Tafiti zinasema kwamba zaidi ya asilimia tano ya wanawake hupatwa na tatizo hili la menorrhagia katika maisha yao. Hedhi kutoka muda mrefu inaweza kuwa kiashiria cha changamoto fulani ya kiafya kama
  • kuvurugika kwa homoni
  • uvimbe kwenye kizazi na
  • saratani kwenye kizazi
Ni muhimu kumwona daktari mapema endapo unapata hedhi nzito ya mabonge na inaotoka kwa zaidi ya siku saba. Daktari atakufanyowa vipimo kujua chanzo cha tatizo lako.

Hedhi nzito ya muda mrefu inaweza kukukosesha amani na kuharibu mzunguko wako. Pia hali hii inaweza kukukosesha usingizi na ukashindwa kufaya kazi zako vizuri. Unaweza pia kupungukiwa na damu kutokana na kubleed kupita kiasi.

Soma zaidi kujifunza kuhusu hedhi kutoka muda mrefu, pamoja na chanzo cha tatizo na namna gani ufanye kupunguza dalili zake mbaya

Kinachosababisha Hedhi Kutoka Muda Mrefu​

Hedhi kutoka muda mrefu inasababishwa na changamoto nyingi ikiwemo:-

Kuvurugika kwa homoni na mayai kupevuka​

Mabadiliko ya homoni na mayai kupevuka inaweza kupelekea hedhi kutoka muda mrefu. Kwa mwanamke mwenye afya njema asiye na matatizo ya uzazi anaweza kuona mabadiliko haya hasa anapokaribia kukoma hedhi, au mwanzoni unapoanza kupata hedhi wakati wa kubalehe.

Lakini pia homoni zaweza kuvurugika kutokana na matatizo mbalimbali kama changamoto za tezi ya thyroid na vimbe kwenye mayai.
Kama homoni zako zimevurugika au kama mayai hayatolewi kwenye mifuko ya mayai wakati wa mzunguko wako, ukuta wa mimba utakuwa mnene sana . Na pale ukuta utakapobomoka na kutoka nje hehdi yako itakuwa ya muda mrefu sana na nzito.

Matumizi ya dawa yanaweza kupelekea hedhi kutoka muda mrefu​

Hedhi yako inaweza kutoka muda mrefu kutokana na dawa ulizotumia katika mwezi husika. Dawa hizi ni pamoja na
  • dawa za maumvu
  • kuzuia mimba(contraceptives) na
  • dawa za kupunguza uvimbe mwilini

Ujauzito​

Bleed ya muda mrefu inaweza kuwa kiashiria cha mimba kutunga nje yakizazi au mimba kuharibika. Unaweza pia kupata bleed ya muda mrefu endapo una tatizo la kondo la nyuma kwenye mimba yako.
Kama ulifanya kipimo cha mimba ukakuta kinasoma positive, na unapata bleed hakikisha unaenda hospitali haraka.

Uvimbe Kwenye kizazi(Uterine fibroids or polyps)​

Uvimbe kwenye kizazi unaweza kupelekea hedhi kutoka muda mrefu na ikaambatana na mabonge ya damu. Fibroids hutokea pale misuli ya kuta za kizazi zinapoanza kukua kupita kiasi.

Kutanuka kwa kizazi (adenomyosis)​

Adenomyosis ni tatizo lingine kwenye kizazi ambalo husababishwa na tishu kukua kupita kiasi. Tatizo linaweza kusababisha kizazi kutanuka na hedhi kutoka muda mrefu zaidi.

Matatizo ya tezi ya thyroid(tezi ya shingoni)​

Kama tezi ya thyroidi haifanyi kazi vizuri kuzalisha homoni zinazotakiwa kwa shughuli za mwili inaweza kupelekea hedhi kutoka muda mrefu sana.Tatizo hili la tezi ya thyroid huitwa hypothyroidism.

Uzito Mkubwa na Kitambi.​

Uzito mkubwa na kitambi husababisha hedhi nzito na kutoka kwa muda mrefu. Hii ni kwasababu seli za mafuta huzalisha zaidi homoni ya estrogen. Estrogen ikizidi sana huvuruga hedhi yako.

Pelvic inflammatory disease(PID)​

PID ni maambukizi ya bakteria kwenye njia ya uzazi. Tatizo lisipotibiwa mapema hupelekea hehdi kuvurugika na hivo upate hedhi ya muda mrefu. PID pia husababisha maumivu chini ya kitovu, maumivu kwenye tendo la ndoa na kutokwa na uchafu ukeni wenye harufu kali.

Saratani​

Hedhi kutoka muda mrefu inaweza kuwa ni kiashiria kwamba una saratani ya kizazi au saratani ya shingo ya kizazi.

Lini unatakiwa kumwona daktari?​

Usipuuze endapo unapata hedhi ya muda mrefu zaidi ya siku saba, maana unaweza kuwa na tatizo kubwa la kiafya. Kuchelewa kupata vipimo na kuanza matibabu inaweza kuongeza ukubwa wa tatizo linalosababisha.
Endapo unapata dalili zingine kama homa na mabonge makubwa ya damu kama limau unahitaji kwenda hospitali haraka. Kama unabadili zaidi ya pedi mbili kwa masaa mawili, unahitaji kumwona dakari.

Jinsi gani Daktari Atakufanyia Vipimo kujua Chanzo cha Tatizo?​

Kuna vyanzo vingi vinavyopelekea utokwe na hedhi kwa muda mrefu kama tulivoona hapo juu, kwahivo unapoenda hospitali ,daktari ataanza kwa kukuuliza maswali haya
  • lini hedhi yako imeanza kutoka?
  • unapadilisha pedi au tampni ngapi kwa siku?
  • dalili zingine unazopata?
  • historia ya afya yako kama umetumia dawa hivi karibuni na
  • historia ya familia yako kuugua magonjwa mbalimbali?
Daktari pia anaweza kupendekeza ufanyiwe kipimo cha utrasound kuona hali ya kizazi chako, na vipimo vingine kama
  • cha damu kucheki homoni
  • kipimo shingo ya kizazi kucheki kama kuna saratani(pap smear test) na
  • kipimo cha kuingiza ukeni kuona hali ya kizazi (Hysteroscopy)

Matibabu ya Changamoto ya hedhi kutoka muda mrefu​

Matibabu ya tatizo yanategemea na chanzo cha tatizo lako. Daktari anaweza kupendekeza dawa za kupunguza damu inayotoka , na dawa za kurekebisha homoni na maumivu.
Dawa za kurekebisha homoni zinaweza kuwa za vidonge, sindano au za kuweka ukeni. Zitakusaidia kupunguza uwezekano wa tatizo kujirudia katika hedhi ijayo.
Katika mazingira fulani daktari anaweza kupendekeza ufanyiwe upasuaji ili kutibu shida ya hedhi kutoka muda mrefu.
Kama hujitaji tena kushika mimba au kupata watoto kwa siku zijazo unaweza kuamua kutoa kizazi chote (hysterectomy).

Nini madhara ya muda mrefu ya kutokwa na hedhi nyingi​

Kuchelewa kupata tiba ya chanzo cha tatizo lako kutapelekea tatizo kuwa kubwa na kuhitaji tiba ya muda mrefu zaidi.
Pia hedhi inapotoka kwa muda mrefu zaidi hupelekea upoteze madini chuma mengi na hivo upungukiwe na damu.
Muone daktari mapema ili kufanya vipimo kujua chanzo cha hedhi yako kutoka kwa muda mrefu zaidi. Kuchelewa kupata tiba unafanya tatizo liwe kubwa zaidi na kuhitaji matibabu makubwa zaidi kwa siku za mbele.

Ukitumia Dawa za Hospitali hujapona Nione mimi nipate kukutibia maradhi yako na utapona uguwa pole.
 
Dawa za hospital Ni zip mke Wang hz tatzo analo
 
Back
Top Bottom