Abiy Ahmed ana njia moja tu kuitoa Ethiopia katika mzozo wa vita ya wenyewe kwa wenyewe

Yussufhaji

Member
Sep 9, 2018
35
28
Abiy Ahmed ana njia moja tu kuitoa Ethiopia katika mzozo wa vita ya wenyewe kwa wenyewe

04/11/2021

Novemba 6 mwaka jana, Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed alitangaza operesheni za Kijeshi katika mji wa Tigray dhidi ya vikosi vya T.P.L.F, kufuatia madai ya Serikali ya Ethiopia kuwa T.P.L.F ilivamia kambi ya jeshi la taifa hilo,

Huko nyuma, tayari kulikuwepo na sintofahamu ya kisiasa baina ya Serikali kuu ya Ethiopia iliyopo Adis Ababa na ile ya Mkoa wa Tigray kufuatia Serikali ya Mkoa wa Tigray kukaidi agizo la kutofanya uchaguzi wakati wa janga la Uviko-19 na kupelelea Adis Ababa kukatisha udhamini wa kibajeti kwa Mkoa wa Tigray,

Hakuna asiyejua nguvu kubwa waliyonayo T.P.L.F na udhibiti wake wa siasa za Ethiopia kwa miongo kadhaa, T.P.L.F ni kikundi kilichoshiriki kuunda Serikali Kuu ya Ethiopia kwa miongo mitatu mfululizo,

Pamoja na harakati za propaganda za Serikali ya Abiy Ahmed kuwa inaenda kushinda mzozo huu wa kivita, lakini inasemekana hali ni tofauti kabisa na picha inayo ionesha Adis Ababa kwa jamii ya kimataifa,

Kwa mujibu wa Mtandao wa New York times katika makala yake yenye kichwa cha habari "Kwanini Ethiopia ipo katika vita yenyewe kwa yenyewe?" inaeleza kuwa zaidi ya watu milioni 1.7 wameyahama makaazi yao kutokana na mzozo huu wa kivita, na zaidi ya 63,000 wamekimbilia nchi jirani ya Sudan huku watu zaidi ya 350,000 wakikumbwa na janga la njaa,

Huku T.P.L.F wakisemekana wakipata nguvu siku baada ya siku pamoja na uwezo mkubwa wa Jeshi la Ethiopia na mshirika wake katika vita hiyo, Eritrea!

Siku chache zilizopita Abiy Ahmed alitumia mtandao wa kijamii wa Facebook kuwataka raia wa nchi hiyo kuchukua silaha kupambana na waasi wa T.P.L.F aliyo waita ni magaidi, ikiwa ni dalili ya wazi kabisa ya kuzidiwa kwa Adis Ababa katika vita hiyo,

Waswahili wanasema, mtu mzima akivuliwa nguo huchutama!

Mwaka 2009, Abiy Ahmed alishinda tunzo ya amani ya Nobel baada ya kufanikiwa kusuluhisha mgogoro wa mpaka baina ya nchi yake Ethiopia na Eritrea kwa njia ya mazungumzo,

Iweje Abiy Ahmed aweze kupatana na jirani yake kwa njia ya mazungumzo ashindwe kupatana na ndugu zake kwa njia ya mazungumzo????

Tuseme Abiy Ahmed hazijui nguvu zilizokita mizizi za T.P.L.F katika siasa za Ethiopia kwa miongo zaidi ya mitatu? kwa maana aliamua kucheza na moto kwa kutumia mikono yake miwili???

Kwa uoni wangu njia pekee ya kutatua mzozo huu wa vita ya wenyewe kwa wenyewe ili isienee zaidi na kuleta madhara zaidi kwa Ethiopia ni mazungumzo!

Abiy Ahmed asijisahau kuwa tayari ana jalada jengine la kesi katika uwanja wa kimataifa kufuatia ujenzi wa bwawa la kufua umeme linalojengwa na Ethiopia katika mto Nile na kuzua mtafaruku na vuta nkuvute na jirani zake Misri na Sudan,

Abiy Ahmed aelewe kuwa, wakati huu Ethiopia inahitaji kuwa tulivu kuliko wakati wowote ule katika historia yake.

@Mtoto_wa_Mkulima

Karibu!
Yussuf H. Khatib
Email: hajjyussuf2@gmail.com
WhatsApp: Jaa WhatsAppissa

FB_IMG_16360257561257744.jpg

Sent from my SHV40 using JamiiForums mobile app
 
Ooooooh!! Sudan.. Sudani ina Historia yakupokea wakimbizi wengi na Kwa nyakati mfululizo ktk Afrika!!
God bless Sudan , Afrika na TZ
 
Watigray ndio kabila linadominate kila kitu wao ndio wasomi wakubwa, ndio wenye nyadhifa za kiutendaji kubwa kubwa ethiopia na ndio jamii ya matajiri ethiopia na ndio wengi wapo Abroad hata mkurugenzi wa WHO ni mtigray na kwa haraka nguvu za kiuchumi walizonazo ni kubwa sana kosa kubwa ilikua kuwaondolea ufhibiti wa mambo mengi kwa hila kama walivofanyiwa wachaga enzi ya jpm, lakini ngoma kule ni mbichi maana jamaa wanataka sasa kujitawala wawe na nchi yao
 
Abiy Ahmed ameichimbia kaburi Ethiopia, alitaka kujifananisha na dictator Meines Zenawi!

Sent from my SHV40 using JamiiForums mobile app
 
Watigray ndio kabila linadominate kila kitu wao ndio wasomi wakubwa, ndio wenye nyadhifa za kiutendaji kubwa kubwa ethiopia na ndio jamii ya matajiri ethiopia na ndio wengi wapo Abroad hata mkurugenzi wa WHO ni mtigray na kwa haraka nguvu za kiuchumi walizonazo ni kubwa sana kosa kubwa ilikua kuwaondolea ufhibiti wa mambo mengi kwa hila kama walivofanyiwa wachaga enzi ya jpm, lakini ngoma kule ni mbichi maana jamaa wanataka sasa kujitawala wawe na nchi yao
Upo sahihi mkuu, Abiy alifanya kosa kubwa sana kuingia vitani na Tplf huku akijua hata majenerali wengi wa jeshi la Ethiopia wametokana na kabila hilo.

Inashangaza namna majeshi ya Eritrea na Yale ya Abiy yalishindwa kuiangamiza Tplf mwanzoni walipoukamata mji wa Mekelle hii ilikuwa ni ishara tosha kwa Abiy kwamba ushindi wa kijeshi usingewezekana tena.
 
Abiy na serikali yake wana wakati mgumu sana wanapambana na watigray ambao wana asili ya vita ikikumbwa kwamba wenyewe ndio walioiangusha utawala wa kiimla wa Mengistu kwa njia ya mtutu.

Leo hii Ethiopia baada ya kukosana na Egypt pamoja na Sudan kufuatia mzozo wa bwawa waliojenga sasa inaonekana mataifa hayo hasimu pamoja na Marekani na nchi za magharibi ziko nyuma ya watigray ktk vita hivi vya wenyewe kwa wenyewe na Ethiopia inaonekana tayari wako "On the receiving end as far as this war is concerned".
 
Sio kweli kuwa jeshi la Ethiopia linashindwa kuangamiza kikosi cha TPLF ila wanaheshimu sheria za umoja wa mataifa wasije kuangukia kwenye kufuli za ICJ ndomana sasa Abiy Ahmed ameamua kusukuma mzigo kwa wananchi ili wazitwange na TPLF kwakua jumuiya ya madola haiwezi kushitaki wananchi.
Mbowe sio gaidi

Sent from my Infinix X606D using JamiiForums mobile app
 
Nani kakuambia haya? Huo mzigo kwanini hakuusukuma kwa raia toka mwanzo wa Vita?
 
Back
Top Bottom