Abiria wapanda mabasi ya UDART kwa kugombea

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,557
21,495
Abiria wanaotumia mabasi yaendayo haraka ya kampuni ya UDART wamepata adha ya usafiri baada ya magari zaidi ya 20 kuharibika kutokana na mvua iliyonyesha wiki iliyopita.

Kwa mujibu wa UDART, mvua iliyonyesha Jumatano Oktoba 25 na Alhamisi Oktoba 26,2017 imesababisha mabasi 29 ya kampuni hiyo kuharibika.

Leo Jumatatu Oktoba 30,2017 asubuhi abiria wakitumia nguvu kupanda mabasi ili kuwahi kwenye shughuli zao.

Waliokuwa wakihangaika zaidi ni wanafunzi wa kidato cha nne ambao wameanza mitihani yao ya Taifa leo.

Baadhi ya vituo ambavyo abiria wamekuwa wakigombea mabasi ni vya Kimara, Mbezi na Ubungo.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jafo ameshaagiza watoa huduma ya mabasi hayo kuhakikisha yaliyoharibika yawe yametengenezwa ifikapo Alhamisi Novemba 2,2017 ili kuwaondolea adha abiria.



Mwananchi
 
Nasikia eti jiji la dar lilishika nafasi ya nane kwa Huduma bora za usafiri duniani
 
Back
Top Bottom