Abiria wa daladala Dar hupoteza Dakika 110, vibonge husota zaidi vituoni

Casuist

JF-Expert Member
Jul 23, 2014
1,179
2,940
Katika toleo lililopita tuliona jinsi ambavyo abiria wanapoteza muda mwingi kituoni na kwenye daladala jijini Dar es Salaam kutokana na foleni. Endelea…

Uchunguzi wa gazeti hili, umebaini daladala katika jiji hilo hupoteza wastani wa tripu mbili kuanzia siku ya Jumatatu hadi Jumamosi.

Kwa mujibu wa Sumatra, jiji hilo lina daladala zipatazo 10,154 na kutokana na upotevu wa tripu mbili kwa foleni, daladala moja ndogo inakadiriwa kupoteza Sh 40,000 kwa siku wakati kubwa hupoteza Sh 150,000. Maana yake ni kwamba kuna wastani wa Sh 80,000 ambazo hupotea kwa siku kwa kila daladala.

Hii inamaanisha kwamba endapo daladala zote 10,154 zitabeba abiria kwa siku katika jiji hilo, wastani wa mapato ya Sh800 milioni yatapotea kwa siku katika usafiri huo.

dALADALA.jpg

Vibonge husota zaidi vituoni

Kondakta wa Tegeta Nyuki-Ubungo, Barante Thomas anasema kutokana na changamoto ya foleni inayosababisha kupungua kwa ruti zake, imesababisha makondakta na madereva wengi kuwa na uchaguzi wa abiria wakati wa abiria wengi asubuhi na jioni.

Thomas anasema hukwepa abiria mnene asubuhi kwa sababu anachukua nafasi kubwa ndani ya daladala. Mbali na hilo, anasema watu wanene hususani wanawake wamekuwa si ‘shapu’ kujipanga ndani ya daladala.

“Si mimi tu kila konda huwa anaangalia sana mtu mnene, afadhali nichukue wembamba watatu nitawapanga vizuri kuliko mmoja mnene, ni hasara kwenye hesabu yangu,” anasema.

Anasema hatua hiyo hujitokeza zaidi katika mazingira ya kuchukua abiria vituoni baada ya daladala kuondoka kituo kikubwa cha Tegeta Nyuki. Anasema hulazimika pia kupanga abiria watatu hadi wanne katika ngazi moja ya mlango pamoja na kuchagua abiria wembamba.

Tahadhari za kiuchumi

Pamoja na usafiri wa daladala, kuna usafiri wa treni mbili za Mwakyembe usiotosheleza. Pia kuna usafiri wa kukodi kama taksi, Uber na bodaboda ambao hautumiki kwa wakazi wengi wa Dar.

Kwa mujibu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), makadirio ya idadi ya watu jijini Dar es Salaam hadi Desemba mwaka jana ilikuwa ni milioni 5.7 lakini idadi hiyo inatajwa kukua kwa kasi huku usafiri wa daladala ukitumika zaidi.

Profesa wa uchumi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Humphrey Moshi anasema muda unaopotea umeathiri kiwango cha ufanisi wa kazi na kuathiri mchango wake katika Pato la Taifa (GDP).

Kwa mujibu wa ripoti ya NBS, mchango wa jiji la Dar es Salaam katika GDP kwa mwaka 2016 ilikuwa ni asilimia 17.02 na mchango huo unaonekana kukua tangu mwaka 2007.

Anasema zipo tafiti zinazoonyesha jiji la Dar kupoteza Sh4 bilioni kwa siku kutokana na foleni. “Kwa tatizo la muda unaopotea, inawezekana mtumiaji usafiri huo anatumia saa nne tu badala ya nane kufanya kazi, kwa mantiki hiyo productivity (uzalishaji) inapungua, inapelekea hata kiwango cha GDP kilichotarajiwa kukosekana, kiwango hicho (asilimia 17) ni kidogo kwa shughuli za jiji hilo,” anasema Profesa Moshi.

Profesa Moshi pia anasema athari zinazojitokeza ni kubwa kuliko gharama za kuwekeza miradi ya kuondoa foleni. Anasema Serikali inatakiwa kuwa na mipango ya mudda mrefu katika miradi ya miundombinu kutokana na kasi ya ukuaji wa jiji.

Mwaka 2040 wakazi Dar huenda wakafikia hadi 12 milioni, kama inavyoelezwa katika utafiti wa Februari mwaka huu wa wataalamu wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (Jica).

“Kwanza Plan ya zamani ilivurugwa kwa watu kujenga holela, lakini hata kwa sasa Plan bado ina shida, barabara ya njia mbili iliyojengwa na Mwalimu Julius Nyerere, haiwezekani tena leo kujenga njia mbili, lazima tuwe na Plan ya miaka 50 mbele, mfano barabara ya Bagamoyo hakukuwa na sababu ya kujenga njia mbili ila ilitakiwa njia nne kutokana na kasi ya ukuaji wa jiji,”anasema Profesa Moshi.

Mwendokasi bado

Gazeti hili limefanya mahojiano na baadhi ya madereva wa usafiri huo walioomba kuhifadhiwa majina yao. Dereva wa mwendokasi wa Kimara-Kivukoni anasema katika njia hiyo wamepangiwa kutumia dakika 35 tu lakini kutokana na matumizi ya trafiki amekuwa akitumia wastani wa dakika 45.

“Si peke yangu tu, hata wewe unaweza kuwa
 
Madereva huchangia kutupotezea dakika nyingi tu, yani umekaa unasubiri li UDART lije, unakuta mda wa kazi yenyewe yana paki unakuta mi UDART imepangana kituoni then hapo hapo abiria wengi wanasubiria magari hiki nn?

au unakuta li UDART linapita kituoni litupu halina abiria linaenda kusimama kituoni kingine kisicho na abiria kama Jangwani au Argentina hasa hiki nn?
 
Back
Top Bottom