Abiria Mabasi yaendayo Mwanza & Bukoba Tunanyanyasika! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Abiria Mabasi yaendayo Mwanza & Bukoba Tunanyanyasika!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Andre02150, Jun 15, 2012.

 1. A

  Andre02150 JF-Expert Member

  #1
  Jun 15, 2012
  Joined: Feb 2, 2010
  Messages: 270
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 45
  Siku za hivi karibuni nilisafiri kwenda Mwanza na Bukoba kwa kutumia bus. Wasafiri tulipatwa na adha nyingi njiani ukianzia kusimamishwa bila mpango na maaskari usalama barabarani, mizani, na mbaya zaidi - pengine kuliko zote ni sheria ya kuyataka mabasi yaingie kwenye Stendi za kila Wilaya! Sielewi TABOA, SUMATRA na Wananchi kwa ujumla walikuwa/tulikuwa wapi kutafafuta njia mbadala ya kuwezesha Halmashauri kukusanya mapato bila kutubugudhi cc wasafiri.

  Kero nyingine ambayo kusema ukweli wadau inawabidi waitupie macho ni sheria ya kuzuia mabasi ya abiria kusafiri ifikapo saa nne usiku, na mikoa mingine ifikapo saa 5 usiku (sasa cjui hii discrepancy inatoka wapi!). Inawezekanaje bus linatoka mkoani kuja jijini Dar, kisha likifika Morogoro saa nne usiku linazuiliwa kutembea masaa mawili yaliyobakia? Au bus linasafiri kutoka Dar na kisha likifika Kahama saa tatu usiku linazuiliwa kuendelea na safari kisa kuna maharamia njiani!! Yaani kweli cc Watanzania, na Viongozi wetu wa serikali tumekubali kuwa terrorized na maharamia kiasi kwamba hatuwezi kusafiri hadi kukesha!!

  Binafsi nafikiri viongozi wabuni mikakati ya kuondoa karaha kwa wasafiri tunaosafiri safari hizi ndefu badala ya kutuongezea sheria zilizojaa adha (au zenye kulinda maslahi ya watu wachache) na pengine sasa wakati muafaka umewadia wa ku-revise Sheria ya Usalama barabarani na ikibidi wa-institute Public Safety Act?! Duniani kote, usafiri wa uhakika na salama ni usiku. Ni hapa Tanzania peke yake ambako kusafiri usiku inaonekana hatari...ni imani yangu kwamba ukiwekwa utaratibu makini, tena utaratibu shirikishi mabasi yatasafiri safe usiku.
   
 2. Mshuza2

  Mshuza2 JF-Expert Member

  #2
  Jun 15, 2012
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 4,119
  Likes Received: 1,749
  Trophy Points: 280
  Ngoja tusubiri watu wa SUMATRA WAJE WALIZUNGUMZIE! Hata hivyo binafsi,napenda sana kusafiri usiku! Wakati sisi usiku tunalala, majirani zetu Kenya ndio kumekucha..mabasi ndio muda wao wa kujidai! Lakini kwetu huku dah! Eti usalama! Amani tunayojivunia iko wapi?
   
 3. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #3
  Jun 16, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,785
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  Ni kweli mizani,vizuizi njiani na matuta ya kugunguza mwendo ni kero kubwa ktk barabara za Tanzania kwa abiria na madereva wanaosafiri umbali mrefu. Kuna haja ya kuangalia upya taratibu za usalama barabarani kuanzia utoaji wa leseni wa makapuni ya usafirishaji,udereva na aina ya mabasi ya masafa marefu.
   
 4. Dhuks

  Dhuks JF-Expert Member

  #4
  Jun 16, 2012
  Joined: Mar 15, 2012
  Messages: 1,471
  Likes Received: 350
  Trophy Points: 180
  Ni maharamia gani hao wako Tanzania ambao nchi jirani hamna?
   
 5. vipik2

  vipik2 JF-Expert Member

  #5
  Jun 16, 2012
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 1,175
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Safiri usiku koooote lakini sio Kahama-Bukoba au Kahama-Kigoma, siku ukijaribu tu unavunjwa ungo! hawanaga utani majambazi wa huko
   
 6. Dhuks

  Dhuks JF-Expert Member

  #6
  Jun 16, 2012
  Joined: Mar 15, 2012
  Messages: 1,471
  Likes Received: 350
  Trophy Points: 180

  Askari huajiriwa wa kazi gani?
   
 7. n

  ndomyana JF-Expert Member

  #7
  Jun 16, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 4,732
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Toka arusha to dar es saalam,. Stend lazma uingie kila wilaya tengeru, boma,moshi mjini, moshi vijijin'himo',mwanga, korogwe, kibaha kote unalipia yani nikero hizi halmashauri ,. Afu stend zenyewe hazina hata huduma
   
 8. Dhuks

  Dhuks JF-Expert Member

  #8
  Jun 16, 2012
  Joined: Mar 15, 2012
  Messages: 1,471
  Likes Received: 350
  Trophy Points: 180
  Wow:frusty:
   
 9. Narubongo

  Narubongo JF-Expert Member

  #9
  Jun 16, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,922
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 135
  njia nzuri ni kuwa na escort ya polisi may be kila mabasi 3-5 yawe na escort ya gari ya polisi ambapo si mbaya sana iwapo wenye mabasi wakalipa escort charges. Najua kisingizio ni ukosefu wa fedha na hili ndio suluhisho
   
 10. Dhuks

  Dhuks JF-Expert Member

  #10
  Jun 16, 2012
  Joined: Mar 15, 2012
  Messages: 1,471
  Likes Received: 350
  Trophy Points: 180
  Naomba kuuliza Kwani hali ya usalama imezoroteka kiasi gani? mchana escort inahitajika?
   
 11. Narubongo

  Narubongo JF-Expert Member

  #11
  Jun 16, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,922
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 135
  tunazungumzia safari za usiku "sheria ya kuzuia mabasi ya abiria kusafiri ifikapo saa nne usiku, na mikoa mingine ifikapo saa 5 usiku"
   
 12. Dhuks

  Dhuks JF-Expert Member

  #12
  Jun 16, 2012
  Joined: Mar 15, 2012
  Messages: 1,471
  Likes Received: 350
  Trophy Points: 180
  Naelewa kinachozungumziwa ila najiuliza mbona escort ihitajike hayo masaa unayotaja?
   
 13. A

  Andre02150 JF-Expert Member

  #13
  Jun 18, 2012
  Joined: Feb 2, 2010
  Messages: 270
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 45
  Dhuks: escort kwa njia ya Kahama - Bukoba ni mchana. Usiku askari hawakubali hata kidogo kukusindikiza. Hivyo basi, ni dhahiri kwamba vyombo vyetu vya Usalama, kwa maana ya Jeshi la Polisi, wameshindwa kudhibiti wimbi la maharamia/majambazi/ majangili katika hii njia. Nafikiri ni wakati mwafaka kwa JWTZ kutusaidia sisi wananchi na kusafisha hilo pori. Pengine kuna umuhimu wa vyombo vya Ulinzi kuanzisha kambi za mazoezi kwenye maeneo 'korofi' ili kunusuru na kulinda UHURU NA USALAMA WETU!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
Loading...