Abiria kujaa kwenye mabasi: Mwangalie huyu polisi

EMT

Platinum Member
Jan 13, 2010
14,483
15,303
Hii picha inadaiwa kuchukuliwa tarehe 16 Septemba 2011 ndani ya basi la Aboud lililokuwa likitokea Morogoro kwenda dar ambapo tiketi zilikuwa zinagawiwa kama njugu bila kujali manifest ya abiria. Kama vile haitoshi polisi wa trafiki nae aliomba lift na kuwa miongoni mwa abiria wasiokuwa na viti vya kukaa kama picha inavyoonyesha. Inadaiwa huyu polisi aliomba lift kwenye hili basi ambalo tayari lilikuwa limeshasheheni abiria kinyume na sheria katika maeneo ya Mwidu ambapo basi la Glazia lilipata ajali hivi karibini. Kwa habari zaidi tembelea: http://issamichuzi.blogspot.com/2011/09/mzee-wa-feva-na-lift-ya-bus-lililojaa.html#comments

 
Kuna polisi bongo? mimi wote nawahisi ni waganga njaa tuu, huwezi ukawa serious mtu kama polisi unamlipa laki2 kwa mwezi ili afanye kazi yake kwa uadilifu
 
Huyu askari na viongozi wake wote " akili box" katika kila ajali Police traffic wanachangia asilimia 70%, Tazama alivyokaa kizembe hivi wewe mwana JF ukipewa ukamanda wa Traffic Mkoa askari kama huyu utamfanya nini. Poleni Watanzania mtaendelea kufa kwa ajali mpaka hapo mtakapofiikiri vizuri. ni wajibu wa kwanza wa serikali serikali yeyote duniani kuwalinda raia wake kwa staili hii utaamini kuwa serikali yetu iko makini kutulinda?
 
Jamani hili litawagharimu sana hawa MATRAFIKI sana hashwa wa huu mji wetu wa Arusha wenye kupenda fedha kushinda UTU wa binadamu,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,Mi cjui hata Watanzania tutaelimika lini.
 
Aaah mbona huyo Traffic alishafinyiwa saa nyingi! mnapoteza muda kuiDiscus hii mada?
 
Hiyo 06xx 777 444 ni nmabari ya simu ya mmiliki wa basi au Police?
nadhani ni namba ya ofsini hiyo mkuumana iipo ndani ya basi juu kabisa sa sijiui wantakiwa kupiga wakishapata ajali au gari ikiwa mwendo kasi,au wanapoona gari inajaza kupitiliza
 
Hapana haikuzidisha abiria... kwani hao waliozidi ni Wamasai... Hata likipata ajali utasikia Walikuwepo Abiria 55 na WAMASAI 7...
 
inaboa hile mbaya.unalipa hela hili usafiri kwa starehe halafu basi linasanya abiria utafikiri daladala
 
Mi nafikiri amelikamata gari na analipeleka kituoni, kama angeomba lift angevua kofia kuashiria kuwa hayuko kikazi, tujue hata kanuni ndogo za kipolisi si kulaumu tu.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom