Abiria kuharibu vyoo Ferry ya Kigamboni ni aibu ya karne

Msanii

Platinum Member
Jul 4, 2007
22,603
29,743
TEMESA wanaoendesha mradi wa kuvusha abiria, magari na mizigo Kivuko cha Kigamboni, wamefanya upanuzi wa eneo la abiria upande wa Kigamboni.

Sambamba na upanuzi huo, wamejenga vyoo vya abiria eneo la banda la kusubiria kivuko.

Ujenzi bado unaendelea kukamilisha maeneo yaliyosalia lakini TEMESA wameruhusu sehemu hiyo kuanza kutumika. Tangu wameruhusu hadi sasa haijapita hata miezi miwili, lakini kwa aibu yetu watumiaji wa vyoo wamejitahidi kuharibu vyoo na mabomba ya maji kwenye sinki za kunawia mikono.

Hebu tujiulize, mtu unaenda haja ndogo kisha unakolokochoa pee pit sijui unafikiria mkojo unasukumwa kama.kimba au? Hali hii imesababisha maji na mikojo kusambaa chini eneo la.choo.
20210803_080101.jpg
pee pit kilichoharibiwa na abiria..

Hali hii pia utaikuta upande wa pili kwenye vyoo jirani na kituo cha mwendokasi. Hapo uharibifu ni wa kudumu maana ni mwaka wa tatu sasa yale mabomba ya chooni yameharibiwa bila kurekebishwa

Kuna wakati inabidi kamera ziwepo ili kujua nani anaharibu mali ya umma awapo mawalitoni.

Sitaki kuamini kwamba mpaka leo kuna waMikoani ambao wanashindwa kuelewa matumizi ya maliwato kistaarabu
 
Dah, hii imenikumbusha siku ya Uzinduzi wa Uwanja wa Taifa ( Mkapa Stadium) ,tumeingia uwanjani mpira umeanza lkn ile kufika Mapumziko ya baada ya Dakika 45 tunaenda vyooni tunakuta Bomba zishang'olewa!!🤣🤣🤣

Kusema ukweli kuna watu wana shida kubwa sanaa. Na watu wa aina hii wapo Dunia nzima. Kikubwa tunachotakiwa kufanya ni umakini katika kulinda hivi vitu pamoja na kuweka adhabu kali kwa watakaobainika kufanya uharibifu katika mali za umma.
 
TEMESA wanaoendesha mradi wa kuvusha abiria, magari na mizigo Kivuko cha Kigamboni, wamefanya upanuzi wa eneo la abiria upande wa Kigamboni.

Sambamba na upanuzi huo, wamejenga vyoo vya abiria eneo la banda la kusubiria kivuko...
Para ya mwisho ndo imeharibu mantiki yote ya bandiko lako. Dar sio mbinguni wajinga pia wapo
 
TEMESA wanaoendesha mradi wa kuvusha abiria, magari na mizigo Kivuko cha Kigamboni, wamefanya upanuzi wa eneo la abiria upande wa Kigamboni.

Sambamba na upanuzi huo, wamejenga vyoo vya abiria eneo la banda la kusubiria kivuko...
Toeni elimu ya matumizi yake, wengine wanajua hiyo ni ‘game’ ya ‘Playstation’, so anajaribu kuwasha ili acheze FIFA
 
hivyo vyoo vya vip wanawekaje hapo ferry.. walibidi waweke mitaro ya kukojolea kwenye vyoo vya wanaume.. na huko kwa wanawake angalau huwa wastaarabu. lakini pia nadhani ukiweka kiingilio chooni itasaidia kupata funds za ukarabati na kulimit watu kuingia hovyo hovyo
 
Nasema na nitalisema siku zote. Kosa kubwa alilofanya Mungu ni kumuumba Mwafrika. Huwa inanipelekea kusema Mungu hayupo, ni mastori, Mungu angelikuwepo na sifa/utukufu tunazompa Mungu asingelimuumba Mwafrika/asingelifanya kosa kama hilo.

Kila uwanja mwafrika ni najisi, Marais, wafalme, mawaziri. IGP Siro etc etc etc... hata viongozi wa dini (wajasiliadini) ni aibu tupu
TEMESA wanaoendesha mradi wa kuvusha abiria, magari na mizigo Kivuko cha Kigamboni, wamefanya upanuzi wa eneo la abiria upande wa Kigamboni.

Sambamba na upanuzi huo, wamejenga vyoo vya abiria eneo la banda la kusubiria kivuko...
 
kuna baa moja mpyaa ilifunguliwa kitaa fulanii ... haikupita wiki - KOKI zote za maji na accessories za bomba vilinyofolewa

unabaki kujiuliza alochukua anaenda uza bei gani?
 
hivyo vyoo vya vip wanawekaje hapo ferry.. walibidi waweke mitaro ya kukojolea kwenye vyoo vya wanaume.. na huko kwa wanawake angalau huwa wastaarabu. lakini pia nadhani ukiweka kiingilio chooni itasaidia kupata funds za ukarabati na kulimit watu kuingia hovyo hovyo
Kiingilio kipo lakini ndo hivyo unavyoona.

Mpaka mabomba ya kunawia mikono nayo yameharibiwa.

Leo hii ukienda majengo mengi ya umma kwenye maliwato unakuta mafundi maiko washapita.

Nenda pale Milleniun Tower A Makumbusho, vyoo vyote ni aibu.
 
Nasema na nitalisema siku zote. Kosa kubwa alilofanya Mungu ni kumuumba Mwafrika. Huwa inanipelekea kusema Mungu hayupo, ni mastori, Mungu angelikuwepo na sifa/utukufu tunazompa Mungu asingelimuumba Mwafrika/asingelifanya kosa kama hilo.
Kila uwanja mwafrika ni najisi, Marais, wafalme, mawaziri. IGP Siro etc etc etc... hata viongozi wa dini (wajasiliadini) ni aibu tupu
Naona mpaka akili imekuwa retired
 
Hawa ni kuwasimamia kama wanyama tu hakuna jinsi
Kama nao wamewekeza hivyo na wanajua fika kuna wenye tabia za wanyama
Kwanini wasiweke watu kusimamia hapo
Watu wanaiba mpaka mfuko wenye pampers kwenye train
Aibu sana
 
Watu weusi ni jamii ya ajabu sana ya binadamu

Ni Binadamu waliofundishwa ustaarabu kwa karne nyingi lakini hawastaarabiki

Wakikosa vitu vizuri wanalaumu, wakipata wanaharibu

Hovyo na Aibu kubwa kabisa hii
 
sasa wewe huoni unavyo comment, mwafrika huyo! I can assure you, I am normal than usual normality!
Hahahaha
Salute kwako kwa kuwa mkweli.

Lakini Mungu hajahusika na ujinga wa waafrika wenzetu
 
Back
Top Bottom