"Abiria chunga mzigo wako" hii kweli ni kazi ya abiria?

Stevemike

Senior Member
Mar 12, 2011
117
15
Ukiingia ndani ya basi unaweza ukakutana na maandishi, "abiria chunga mzigo wako". Na katika tiketi pia utakutana na mwandishi hayohayo na wanaongeza kuwa kampuni haitahusika na upotevu wowote wa mzigo. Nauliza, hii kweli ni kazi ya abiria? Vipi juu ya mizigo iliwekwa na konda kwenye buti? Mzigo kama huu ukipotea, who will be responsible? Haya wana JF!
 
Kama mzigo umewekwa kwenye buti na umelipiwa gharama ya kuusafirisha hapo hakuna swala la abiria chunga mzigo wako.Hapo linakuwa tu ni swala la poor customer services za watoa huduma!
 
Abiria chunga mzigo wako wa ndani ya bus sio kwenye buti cos wa kwenye buti unalipiwa na risiti wanakupa. nafaham hilo sijui wewe?
 
Ule unaoingia nao kwenye basi ni jukumu lako kuulinda. Uliopo kwenye buti wenye usafiri ndio wanaotakiwa kuulinda, mimi hua kila basi linaposimama nachungulia kuhakikisha hamna mtu anaebebana na begi langu.
 
Back
Top Bottom