Abiria Atakayekutwa Amesimama Ndani Ya Basi Atatozwa Faini...,Huu Ni Utaratibu Mpya Unaoandaliwa Na

COARTEM

JF-Expert Member
Nov 26, 2013
3,565
2,000
POLISI Kikosi cha Usalama Barabarani, inaandaa sheria itakayosaidia kudhibiti ujazaji wa watu kwenye magari ya abiria, ambayo abiria atakayekutwa amesimama, atatozwa faini.


Kauli hiyo ilitolewa jana na Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohammed Mpinga, wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Alisema kabla ya sheria hiyo kutungwa na kutekelezwa, watatafuta njia ya kutatua tatizo la usafiri kwanza.

“Ni kweli kuna maeneo ambayo kuna tatizo la usafiri, kwa maana hiyo kabla ya sheria hii kuanza kutekelezwa, ni lazima itafutwe dawa ya tatizo la usafiri na baada ya hapo ndiyo sheria ianze kutumika,” alisema Mpinga.

Akizungumzia usalama katika msimu wa siku kuu za mwishoni mwa mwaka, Kamanda Mpinga alisema matukio ya ajali ya kutisha yametokea ndani ya mwezi huu.

Alitaja ajali ya mkoani Tanga katika eneo la Kwalaguru katika barabara ya Chalinze – Segera, ambako basi la Kampuni ya Burudani lilipinduka na kusababisha vifo vya watu 12 na majeruhi 76.

Pia mkoani Arusha gari aina ya Noah ilisababisha vifo vya watu sita na majeruhi 12, Tanga katika eneo la Segera magari yaligongana na kusababisha vifo vya watu nane na majeruhi 17.

Alitaja pia ajali ya mkoani Dodoma, ambako basi la Kampuni ya Simiyu Express lilipata ajali na kusababisha vifo vya watu wawili na majeruhi 14.

“Haya ni baadhi ya matukio yaliyotokea kwa mwezi huu wa Desemba, mwaka huu katika mikoa mbalimbali nchini, ambayo yamesababisha majonzi miongoni mwetu na vyanzo vya ajali hizi ni mwendo kasi,” alisema.
source:Abiria Atakayekutwa Amesimama Ndani Ya Basi Atatozwa Faini...,Huu Ni Utaratibu Mpya Unaoandaliwa Na Jeshi La Polisi ~ Mwanahabari Huru
 

kapuyanga mkware

JF-Expert Member
Nov 16, 2013
589
0
ndoto za alinacha. ule utaratibu wa kuwatoza faini wanaotanua uliishia wapi. Mohammed hiyo ni nguvu ya soda vijana wako wako radhi kupokea rushwa ya buku kuliko kuliingizia taifa. Pale Kibaha mkoa wa pwani kuna siri gani hebu pangua ile list kuanzia yule kaka mrefu mwenye nyota tatu pale opposite na stendi. kama hajamaliza ghorofa lake bac.
 

Rose M

Senior Member
Oct 3, 2013
129
225
1-Speed Gavana
2-milango ya dharura kama kutatokea moto..
3.seat belt
4.sasa si ruhusa kusimama duh!!!

Sijui wasipofanikiwa na hii watakuja na ipi..!!!..

Ajali nyingi ni uzembe wa madereva..na siyo watu kusimama..
 

FaizaFoxy

JF-Expert Member
Apr 13, 2011
71,602
2,000
Matatizo ya usalama barabarani yatapatiwa ufumbuzi iwapo tu sheria kali za rushwa zitatungwa na kutekelezwa. Mfano, yeyote atakaeshikwa anatoa au anapokea rushwa, iwe ndogo, kubwa au ya aina yoyote ile hukumu yake iwe ni kifo tu. Na hukumu zitolewe chini ya wiki mbili toka siku mtu amekamatwa.
 

ONDIECK OTOYO

JF-Expert Member
Nov 28, 2013
254
0
ulevi wa madaraka inayoleta isia za kujitungia sheria badala ya bunge amezoea kwani alijitungia sheria kwa mawazo yake ya kutoza watu faini kwa kupita service road ambayo siyo kosa kisheria na hakajifanya ajui maana ya service road na mahakima kama yeye akawakumu watu kwenda jela wiki mbili pamoja na faini ya tsh 200,000.00 sheria ambayo aikupitishwa na bunge huku walengwa wakiwa ni daladala pamoja na bajaj hii ni upuhuzi wa pili anafikiria
 

Android 00

JF-Expert Member
May 23, 2013
774
195
Serikal sikivu inawafanya wananchi wake mpk Leo wanawaza ni jinsi gani atafika mjini? huwa najiuliza serikal inapenda watu waendelee kuishi ivi ili wao waendeshe yao kwa nafasi.

Kwa kweli inauma unapowaona watu hususan kama wa mbagala wamejazwa kwenye gari kama mbuzi. hebu jamani wale mnaosafir tuambieni bado mpk leo kuna nchi nyengine zina utaratibu Huu mpk Leo?
 

Barraza

JF-Expert Member
Oct 10, 2011
482
500
Matatizo ya usalama barabarani yatapatiwa ufumbuzi iwapo tu sheria kali za rushwa zitatungwa na kutekelezwa. Mfano, yeyote atakaeshikwa anatoa au anapokea rushwa, iwe ndogo, kubwa au ya aina yoyote ile hukumu yake iwe ni kifo tu. Na hukumu zitolewe chini ya wiki mbili toka siku mtu amekamatwa.

Rushwa haiwezi kukoma kama miundo mbinu ni hii hii iliyopo..
Tuboreshe kwanza sekta za usafiri wa Umma kabla ya kukimbilia kutoza faini kubwa ama kuwinda watoa rushwa..
 

Daata

JF-Expert Member
Dec 24, 2012
4,535
2,000
Wakilitekeleza hili magari yatakuwa yanawapita watu ---- ila kwa vile rushwa bado haijadhibitiwa hali itabaki kama ilivyo
 

uvugizi

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
1,220
2,000
hili litakuwa ngumu kutekelezeka kwani itafikia mahali ,dereva , abiria na tingo watatupiana mzigo unaweza ukapanda kwa kutaraji utapata nafasi ghafla gari lina move na nafasi hiyo haipo na wakashindwa kukushusha ,kosa la nani na vipi itakuwa rahisi kupata ukweli wa jambo . ni dhahiri kuwa bado anayetakiwa kubanwa na sheria ni wamiliki wa gari (dereva, tingo) na si abiria
 

FaizaFoxy

JF-Expert Member
Apr 13, 2011
71,602
2,000
Rushwa haiwezi kukoma kama miundo mbinu ni hii hii iliyopo..
Tuboreshe kwanza sekta za usafiri wa Umma kabla ya kukimbilia kutoza faini kubwa ama kuwinda watoa rushwa..

Cheza na risasi za kisogo wewe. Nnakuhakikishia Watanzania wawili tu wakilambwa risasi za kisogo kwa rushwa wengine wote tutanyooka.
 

nitonye

JF-Expert Member
Dec 18, 2011
7,273
2,000
Cheza na risasi za kisogo wewe. Nnakuhakikishia Watanzania wawili tu wakilambwa risasi za kisogo kwa rushwa wengine wote tutanyooka.

Ingekuwa vizuri tukaanzia pale magogoni kwenye jumba jeupe ili uwe mfano
 

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
37,025
2,000
Matatizo ya usalama barabarani yatapatiwa ufumbuzi iwapo tu sheria kali za rushwa zitatungwa na kutekelezwa. Mfano, yeyote atakaeshikwa anatoa au anapokea rushwa, iwe ndogo, kubwa au ya aina yoyote ile hukumu yake iwe ni kifo tu. Na hukumu zitolewe chini ya wiki mbili toka siku mtu amekamatwa.

Yaani wewe ni kioja sana. Unawaza sheria ya rushwa kwa usalama barabarani kufikia adhabu ya kifo wakati rushwa za mikataba mikubwa inayoangamiza nchi hujawahi kuisemea? Hiyo mikataba mikubwa ya hovyo hovyo ndio inayozalisha maisha magumu yanayoleta rushwa hizo za barabarani.
 

kibaravumba

JF-Expert Member
Dec 21, 2012
6,639
2,000
Nimeona maelezo lakini ni ya kisiasa tu.Watawezaje kuboresha usafiri nchi nzima?Kama Kenya wameweza kwa nini hapa wasiamue tu hata sasa?Inawezekana sana kwani wakati mwingine abiria wenyewe huamua pasipo ba uharaka wala shida yoyote ya usafiri.Mf njia kama ya Mwanza Bunda.Utakuta watu wamesimama kwenye coaster ingawa kila baada ya dk 5 huwezi kukosa gari imepita.Hii sheria ni muhimu iletwe mapema na waache siasa

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 

Makamee

JF-Expert Member
Nov 29, 2013
2,021
2,000
Nimeongea naTrafick polisi anasema wameshaambiwa marufuku kukamata mabasi kuyapeleka polisi.kama wanataka wachukue hizo buku buku kama hawataki waache gari iende.
Hii maana yake matajiri wa mabasi wanamalizana na RTO's.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom