Abiria 15 bila barakoa kati ya abiria 28 ni kutojali au watu wanajua corona imeisha?

kindikwili

JF-Expert Member
Oct 5, 2016
1,862
2,871
Habari iwe kwenu wakuu!

Leo nilikuwa nimepanda gari kwenda kazini (huwa napanda magari 2 hadi kufika kazini) cha kushangaza kwenye gari la kwanza mpaka nashuka nilihesabu watu wasio na barakoa wakafika 15 na kuna wakati gari ilikuwa na jumla ya watu 28 huku watu 15 wakiwa hawana barakoa kabisa. Njiani kuna wengine walikuwa wanashuka na wengine kupanda ila hata hao waliokuwa wanapanda wengine hawakuwa na barakoa kabisa.

Kwenye gari la pili ambalo huchukua watu wengi zaidi (kivukoni -tegeta) watu kama 6 hawakuwa na barakoa na wengine walikuwa wamevishikilia tu mikononi badala ya kuvaa. Inasikitisha kwamba hayo yanatokea hapa Dar es Salaam ambako matangazo ya corona yamejaa maeneo mbali mbali huku Radio zikitangaza sana juu ya corona. Hata pale ferry kwenye kuvuka baadhi ya watu hawanawi na siku hizi wale walinzi wa SUMA waliokuwa wanasimamia hawasimamii tena wakati mwingine maana si kwamba kila saa niko hapo ila hili nimelishuhudia wakati wa kuvuka wengine hawanawi tena.Kama hali hii ya watu kuzembea kuvaa barakoa wakiwa kwenye usafiri wa umma, kama watu watazembea kunawa mikono na kama wananchi hawatajua kwa uhakika kama ugonjwa bado upo au haupo basi huenda wakati nchi nyingine wanamalizana na tatizo hili sisi tutakuwa ndiyo kwanza tuko kwenye peak.

Ushauri!
1. Kwa wananchi wenzangu jua tu kwamba ikitokea umeugua huu ugonjwa ni wewe na familia yako ndiyo mtahangaika na ikitokea umefariki au umefiwa ni wewe ndiye umefiwa, hivyo tuvae barakoa na kunawa bila kusubiri kushurutishwa.

2. Kwa abiria wengine kukaa kimya wakati mtu wa jirani yako kwenye gari hajavaa barakoa ni kuhatarisha maisha yako. Mwambie bila kumuogopa kuwa avae barakoa hata akinuna wewe mwambie.

3. Tunapoendelea na kampeni ya kufukiza (kwa wanaojifukiza) tusisahau pia kuwasisitiza watu waendelee kuvaa barakoa, kunawa na kukwepa kukaa kwenye vikundi vya watu

4. Kwa jeshi la polisi na mamlaka endeleeni kukagua magari ya abiria na kama mtu atakutwa hana barakoa ashurutishwe kuvaa kwa nguvu

5. Bila taarifa za uhakika na za kuaminika tena ndani ya muda sahihi wananchi wataendelea kuzembea na ugonjwa unaweza ukaenea zaidi

Information is power wapendwa

Kindikwili
 
KILA MMOJA AJICHUNGE YEYE NA ANAOWAJALI, HAYA NI MAPAMBANO YA NAFSI YAKO NA CORONA
 
Tatizo tulio mtandaoni tunaona hali sio swari ila hawa wa redio na Tv wanajua maambukizi yapo kwa wingi Zanzibar maana wao ndo wanatoa update za mara kwa mara
 
KILA MMOJA AJICHUNGE YEYE NA ANAOWAJALI, HAYA NI MAPAMBANO YA NAFSI YAKO NA CORONA

Kuna kuambukiza na kuambukizwa. Unaweza kuchukua tahadhari wewe na jamii yako lakini ukaambukizwa na mtu wa nje ya jamii yako.

Hivyo ni muhimu kumkumbusha mtu ambaye hajavaa barakoa hata kama humfahamu anaweza kukuambukiza. Kumbuka barakoa hasa zinazotengenezwa mitaani sio 100% protective.
 
KILA MMOJA AJICHUNGE YEYE NA ANAOWAJALI, HAYA NI MAPAMBANO YA NAFSI YAKO NA CORONA

Sure man bila kila mtu kujijali kivyake itakula kwa familia wakati wengine wakiendelea na maisha , hili ni suala la mtu binafsi kabla halijawa la jamii kwa ujumla.
 
Taarifa zinazotolewa zinatakiwa zikidhi sifa za taarifa bora yaani ziwe taarifa sahihi (zakweli) au zinazoelekeana na usahihi yaani Accurate /relevant,. ziwe taarifa zinazojitosheleza(complete), ziwe zinapatikana (available) , ziwe za kuaminika (Reliable), ziwe fupi lakini zinajitosheleza (Concise) , ziwe zinapatikana ndani ya muda muafaka (timely) na zipatikane kwa gharama nafuu (cost effective)
 
Taratibu tunaelekea kunako njia salama. Ni suala la muda tu sasa.

Mola na atujalie uzima.
 
Back
Top Bottom