Abdulwahid Sykes na nduguze historia iliyopotea

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
15,589
2,000
ABDULWAHID SYKES NA NDUGUZE HISTORIA ILIYOPOTEA

Gazeti Raia Mwema la Ijumaa tarehe 21 Mei, 2021lilichapa taazia ya Abbas Sykes kwa bahati mbaya wakaweka picha za kaka yake, Ally Sykes badala ya Abbas Sykes.

Gazeti la leo likaomba radhi kwa kusema kuwa waliweka picha ya Kleist Sykes ilhali picha walizotumia ni za Ally Sykes.

Bila shaka kesho wataomba radhi kwa mara nyingine kwa kuandika kuwa picha walizotumia si za Kleist Sykes bali za Ally Sykes.

1621836549338.png

1621836284467.png
 
Kasomi

JF-Expert Member
Sep 3, 2014
7,944
2,000
Kwahiyo hapo Gazeti lao halina wahariri? Au ndo tatizo la kiufundi.

Ila kama wameliona hilo ni vyema, naamini watasamehewa
 
mdukuzi

JF-Expert Member
Jan 4, 2014
8,958
2,000
Hao wasaliti waliingia nchini kama mamluki kumsaidia mjerumani dhidi ya watanganyika pamoja na hayo mzee wangu nitashukuru ukitupatia family tree kuanzia kwa sykes mbuwane mpaka kizazi cha akina ebby au dully
 
Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
15,589
2,000
Hao wasaliti waliingia nchini kama mamluki kumsaidia mjerumani dhidi ya watanganyika pamoja na hayo mzee wangu nitashukuru ukitupatia family tree kuanzia kwa sykes mbuwane mpaka kizazi cha akina ebby au dully
Mdukuzi,
Halikadhalika babu yangu mkuu Samitungo Muyukwa aliingia Germany Ostafrika akitokea Belgian Congo akiwa askari katika jeshi la Wajerumani kuwasaidia kuitawala Tanganyika.

Kituo chake cha kwanza ilikuwa Boma la Shirati na ndipo alipozaliwa babu yangu.

Hakika hawa askari waliwasaliti ndugu zao Waafrika.

Hizi ndizo athar za ukoloni.

Lakini mtoto wake yaani babu yangu Salum Abdallah alisimama kupambana na ukoloni wa Waingereza akiwa mmoja wa wazalendo walioasisi TANU na kufanya mengi kwa maslahi ya nchi yake.

Na hivi ndivyo ilivyokuwa kwa mtoto wa Sykes Mbuwane Kleist.

Aliasisi AA chama kilichokuja kuunda TANU wanae watatu wakiwa waasisi wake na kupigania uhuru wa Tanganyika.

Mimi ni kizazi cha tatu cha Samitungo Muyukwa na mchango wangu ni kuwa nimeweza kutafiti na kuijua historia ya wazee wangu na kuiandika.

Leo tuko hapa tunaisoma na kuijadili.
 
Umeelewaka vema mzee wangu bado family tree ya huo ukoo wa akina sykes ili kuondoa mkanganyiko
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom