Abdulrahman Shimbo ateuliwa na Rais Kikwete kuwa Balozi wa Tanzania nchini China!

Shimbo ni mtu mhimu sana kwa JK, lazima amlipe fadhira, kumbuka kisa cha JK kuondoka Monduli.
 
JK hana aibu hata kidogo. Sijui yuko je. Hivi alishampa MJ.Gen Lupogo cheo toka amtoe TACAIDS?

Kipindi kile nilishindwa kuelewa kabisa, ile ilikuwa ni kuidharau ile Taasisi ya TACAIDS na shughuli zake!
 
isijekuwa kwa sababu anaitwa ABDULRAHMAN ndiyo sababu ya kumsakama. alikua mnadhimu mkuu wa majeshi. ana uzoefu wa kusoma katika nchi mbalimbali mambo ya kijeshi na diplomasia. ni mwana intelijensia. kwa ushawishi wa china ktk ulimwengu wa leo, shimbo ni chagua sahihi. mambo ya kukosoa kila jambo bila hoja yenye mantiki yamepitwa na wakati.
 
taarifa ya habari tbc1 ya saa mbili usiku huu wamesema rasmi kuwa jk kamteua shimbo kuwa balozi china.
Hivi rasimu ya katiba mpya inasemaje kuhusu uteuzi wa mabalozi?
 
taarifa ya habari tbc1 ya saa mbili usiku huu wamesema rasmi kuwa jk kamteua shimbo kuwa balozi china.

Ninahisi Serikali ya CCM haimini tena Vijana, wale vijana wanaoaminiwa na Serikali ya CCM ni kama disaini ya Nape tu. Yaani JK amekosa kabisa mtu wa kuaminika kuiwakilisha Tanzania China!
 
me mwenyewe nimeshangaa sana kale
kashotii na hela zote zile bado kanaajiriwa
haiwezekani.
 
Sasa kama mabilioni yake aliyoiba JWTZ yana share na wengine unafanyaje?
KUmpeleka china ni kumdhibiti.
Akijifanya mjanja walamKolimba, watamKombe, watamSokoine
 
Hv hapo Ikulu imejaa bogus tu,si ndio? Yani advisorz wote wameruhusu hili? Dah
 
Shimbo ni mtu mhimu sana kwa JK, lazima amlipe fadhira, kumbuka kisa cha JK kuondoka Monduli.

Afu by that time Ger Waitara ndio alikuwa mkuu wa kambi pale Monduli kabla hajawa mkuu wa majeshi,,,,,Waitara alimtesa sana Jk...hoply unajua kilichomkuta baada Ya Jk kuwa rais....Shimbo na kashiwa ya kulipua maghala ya siraha mbagala kupoteza ushahidi wa billions of money zilizo nunua silaha hewa
 
...Rais Kikwete amemteua mstaafu A. Shimbo kuwa balozi wa Tanzania nchini China.

Source: TBC1 Habari

Hivi hii teuzi ina merit kweli?....hivi hata tukiongelea diplomatic experience. Is it worthy to have Shimbo in China?....

Wahenga walisema 'Ukistaajabu ya Musa utaona ya firauni'. Mpaka 2015 tutaona maajabu mengi sana...
 
Hakika kama habari hii ni kweli basi nimechoka mwili na roho. Usiku mwema kwa wale wa pande za pande zetu na mchana mwema wenzetu wa dunia nyingine.
 
Haaaaaa...!!!
Shimbo??? Kweli hii nchi imekosa muelekeo kabisa. China inahitaji balozi mwenye mtazamo na career ya biashara na/ uchumi/uwekezaji.
Sasa hii habari ya kuteua teua tu watu kwasababu za ushikaji ni dalili za wazi za udhaifu wa kiuongozi.

Hizi sera za kuwawezesha wastaafu na kuwaweka pembeni vijana ndio chanzo cha umasikini kwa tabaka kubwa la vijana huku hawa wastaafu wenye pensheni kubwa wakiendelea kutumbua tu.

Falsafa ya JK ni kuona hawa wazee washikaji zake wanafaidi maisha yao, maisha ya watoto wetu na maisha ya wajukuu wetu!
 
Kwa wale wanaomfahamu Kamanda Shimbo, watakiri kuwa JK amefanya uteuzi makini sana. Shimbo ni jembe, anafaa sana kupelekwa Uchina ambako kunainukia na kuwa super power, kuwepo kwake kule kutaleta tija kwa Tz na JW kwa ujumla kutokana na mahusiano ya kimkakati kati yetu na China & jeshi lake PLA. Hongera Kamanda Shimbo. You deserve it Mkuu.
 
Ninahisi Serikali ya CCM haimini tena Vijana, wale vijana wanaoaminiwa na Serikali ya CCM ni kama disaini ya Nape tu. Yaani JK amekosa kabisa mtu wa kuaminika kuiwakilisha Tanzania China!

SSM vijana ni taifal la kesho na wazee ni taifa la leo!!! Ha ha ha!! Kweli hatari hii.
 
Kwa kweli kama ni laana hakika huyu mwenyekiti wa ccm anayo juzi tu amempandisha muaji wa Daudi Mwangosi cheo leo fisadi nambari moja kuwa Balozi Nchini China?
Ama kweli jakaya umetuona wanainchi wako hatuoni wala hatutambui unachofanya lakini siku zako na kabinet yako yote inahesabika na si ajabu mkawa wafungwa watarajiwa!

Hili la leo halikubaliki hata kidogo! Loh!
 
Back
Top Bottom