johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 82,752
- 139,555
Halmashauri kuu ya CCM imemsamehe Katibu mkuu mstaafu kanali Kinana ambaye alipewa onyo kali na kuwekwa katika matazamio.
Halmashauri kuu pia imemfukuza kabisa yule mwingine ( Membe) ambaye hakufanya juhudi yoyote ya kuomba msamaha.
Membe alirudisha kadi yake CCM badala ya kutubu.
Maendeleo hayana vyama!
======
Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi, Abdulrahman Kinana
Akizungumza wakati wa kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM cha kumteua mgombea Urais wa Zanzibar, Rais Magufuli amsamehe aliyekuwa Katibu Mkuu wa chama hicho, Abdulrahman Kinana. Rais Magufuli amesema:
Ilikuwa mwezi wa wa pili Central Committee iliamua kutoa adhabu kwa baadhi ya wanachama wetu ambao walikiuka maadili na misingi ya chama chetu.
Kikao kile kilitoa mapendekezo ya adhabu kwa baadhi ya wanachama wetu kutokana na misingi na Katiba halali ya chama chetu. Lakini ni hivi karibuni baada ya miezi kama minne au mitano, mwenzetu mmoja ambaye ni Former Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi alijitokeza hadharani kule Arusha, na nafikiri shahidi ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha – akaomba radhi., akajutia kwa kitendo alichokifanya. Na kikubwa zaidi, ndugu yetu huyu aliomba radhi hadharani.
Ni kitendo kigumu sana kwa mtu kukifanya. Kinahitaji nguvu ya Mwenyezi Mungu tu kutubu hadharani. Mimi alinigusa sana. Nina uhakika hata ninyi wajumbe mliguswa sana. Alikuwa amepewa adhabu ya miezi 18. Hakukataa kutumikia adhabu ile.
Sasa niliona Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama tawala, chama chenye huruma. Chama chenye mapenzi mema. Chama dume. Niwaombe kwa huruma yenu kama itawezekana, huyu ndugu yetu ambaye amekubali mpaka sasa kutumikia adhhabu miezi mine, tumsamehe.
Kupitia kikao hiki napenda kusema Abdulrahman Omari Kinana amesamehewa rasmi. Niwashukuru wajumbe wa kikao hiki kwa huruma ya upendo.
Yule mwingine ambaye hata jina lake sitaki kulitaja yeye ameshaondoka moja kwa moja. Adhabu yake si mnaikubali?
Zaidi, soma:
1). Imevuja sauti inayodaiwa ni Maongezi ya Simu ya Nape Nnauye na Abdulrahman Kinana kuhusu njama za kuichafua CCM
2). CCM yamfukuza uanachama Bernard Membe, Kinana apewa karipio kali huku Makamba akitoka salama
3). Msamaha: Mzee Kinana amuangukia Rais Magufuli kufuatia mazungumzo yake na makada wenzake wa CCM yaliyovuja