Abdul wa maisha plus | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Abdul wa maisha plus

Discussion in 'Celebrities Forum' started by Msongoru, May 14, 2009.

 1. Msongoru

  Msongoru JF-Expert Member

  #1
  May 14, 2009
  Joined: Apr 16, 2008
  Messages: 306
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Na Juliet Kulangwa

  Waswahili wanasema mguu wa kutoka mtume kaubariki na hivi ndivyo ilivyokuwa kwa Abdulhalim Hafidh Salim ambaye mwishoni mwa wiki iliyopita alijinyakulia kitita cha shilingi za Tanzania Milioni 10.


  Mbali na kujishindia pesa hiyo katika shindano la Maisha Plus anakuwa Mtanzania wa kwanza kuibuka kidedea katika mashindano yaliyowahi kufanyika nchini akiwakilisha pande za Visiwani.


  Kubwa kuliko zote ni kwamba wakati akikabidhiwa ushindi na pesa Tanzania ilikuwa ikitimiza miaka 45 ya muungano wake....Miasha Plus nayo iliwaunganisha kimtindo.


  Mwananchi ndiyo gazeti la kwanza nchini lililopata nafasi ya kwanza ya kufanya mahojiano 'exclusive' na mshindi huyu........ kama hutaki haya lakini habari ndiyo.


  Starehe- Unajisiakiaje kuwa mshindi katika shindano hili?


  Abdul- Kila mmoja alikuwa na ndoto ya kuibuka kidedea, lakini kubwa kuliko zote nolifurahi sana kwa kuwa ushindi unamaanisha pia niliweza kushinda kila jaribio lililokuwapo ndani ya kijiji.

  Kula maharage kila siku, kukata kuni, kupika, kuosha vyombo, task za hatari na mambo mengine ndio yalikuwa maisha yetu ya kila siku, kushinda yote haya ndiyo kushinda milioni kumi. Nimefurahi kwa kuwa lengo langu la kwanza limetimia.


  Starehe- Kwanini unasema lengo lako la kwanza limetimia


  Abdul- Lengo la kwanza lilikuwa ni kushinda na kutwaa milioni kumi lakini hiyo milioni kumi ina mipango yake ambayo pia inahitaji kuyafikia.


  Starehe- Ni malengo gani hayo


  Abdul- Its too soon to tell


  Starehe-Wewe ni mmoja kati ya washiriki waliokuwa vinara katika shindano hilo tangu mwanzo kabisa, kuna siri yoyote ya ushidni wako.


  Abdul- Nilikuwa na kontena la vituko na kwa bahati mbaya shindano limeisha nikiwa nimetumia robo tuu ya vituko vyangu......lakini kura moja ya Mtanzania ndiyo imenisimisha hapa naiheshimu sana.


  Starehe- Umejifunza nini katika kijiji cha Maisha Plus.


  Abdul- Nimejifunza mambo mengi lakini kubwa zaidi ni kuishi na watu kutoka sehemu tofauti,


  Starehe- Upendo, mshiriki kutoka Mwanza aliwahi kusema kuwa wewe ndiye uliyeiweka ile hirizi ****** , je ni kweli ilikuwa ya kwako na kama sio uliipokeaje tuhuma zile.


  Abdul- Kila kilichokuwa kikitokea kwenye kijiji cha Maisha Plus kilikuwa kinareflect maisha yetu ya huku majumbani mwetu, iliniuma kwa kuwa nilikuwa siwezi kuprove kuwa sihusiki katika lile, lakini nililipokea na kulichukulia kama changamoto katika maisha ya kila siku na niliweza kulishinda.


  Starehe- Unauzungumziaje ushindi wako


  Abdul- Baada ya Mungu na wazazi wangu nawashukuru sana Watanzania kwa kunipigania, siwezi kugawana nao hii zawadi lakini wajue ushindi wangu ni wa kwao, ile kura waliyopiga imewapa ushindi, nawashukuru sana na nina waombea mema kila siku.


  Starehe- Unaushauri wowote kwa Rais


  Abdul- Kwanza naomba aitambue Maisha Plus....hii ni zaidi ya taasisi ya elimu. Watanzania ni mashahidi wanaweza kunisaidia katika hili. Pili atimize ahadi alizotoa kwenye kampeni zake mwaka 2005.


  Abdul alizaliwa miaka 25 iliyopita huko kwenye kisiwa cha marashi ya karafuu, ni mhitimu wa shule ya sekondari Vikokotoni .........ushanifahamu
   
 2. Mwana wa Mungu

  Mwana wa Mungu JF-Expert Member

  #2
  May 14, 2009
  Joined: Aug 14, 2008
  Messages: 1,007
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  yule jamaa si mfano mzuri wa kuigwa pamoja na kwamba nilipenda azichukue zile hela, si kwasababu anafaa sana, ila kwasababu alivyotoa stori yake kuhusu kuzamia south,mozambique nk, nilivyoona maisha yake ni magumu sana na akajitambulisha kuwa yeye kule zenji ni mlinzi wa ufukweni, nilimwonea huruma kwamba ana hali ngumu ya maisha, nilipenda achukue.

  ila, alinikera sana kwa kujifanya yeye ni mjuzi wa kumtongoza Tedi, alikuwa na stori za mapenzi kila wakati, alikuwa anajifanya kujua kiingereza kumbe bom, alikuwa anatembea na kisu kama chinjachinja, alikuwa na pete la majini kama mganga, alisema kuwa anapoenda kulinda ufukweni kuna majini hivyo lazima waende kwa wazee kwanza(waganga wa kienyeji), aliposingiziwa kuwa mchawi wa hirizi alisema wakawalete mashehe(ana maana gani, mashehe wana uhusiano gani na hirizi?)aliwaaibisha waislam kwasababu pale aliwawakilisha sana waislam, hakuwa neutral, alikuwa consevative kabisa kwenye dini na mara nyingi alikuwa akitaja mistari ya koran. ni bom kwa kifupi ila alitakiwa kupata zile hela kwasababu ya hali ngumu ya maisha ukilinganisha na ya wenzie ukiondoa kingunge.alionyesha kugombana na upendo hadharani, alikuwa anaongelea puani kama teja.

  siku ya mwisho alipopewa hela, badala ya kumshukuru Mungu na kumpa Mungu sifa na utukufu, alisema "kabla ya kuondoka zenji, aliaga kwa bibi yake na mama yake" akimaanisha kama walimpa baraka fulani ya manuizo either ya kimadawa na mambo yanayofanana na hayo pamoja na kwamba hakueleza vizuri.

  haya ndo yaliyomo moyoni kuhusu yeye, nisiwe mnafiki.
   
  Last edited: May 14, 2009
 3. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #3
  May 14, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Duh mmesha anza mwacheni jamaa aongeze mademu huko Zenji mmesha anza kukandia.
   
 4. Mwana wa Mungu

  Mwana wa Mungu JF-Expert Member

  #4
  May 14, 2009
  Joined: Aug 14, 2008
  Messages: 1,007
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  sasa ndo mfano gani mzuri akifanya hivyo? Mungu amsaidie jamani.
   
 5. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #5
  May 14, 2009
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,306
  Likes Received: 5,596
  Trophy Points: 280
  Muacheni kabisa.....apumzike na vihela vyakeee
   
 6. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #6
  May 14, 2009
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  kama tumuache, wasingemleta hapa. najua kuna maisha plus ingine itaanza miezi miwili ijayo, ndo kina masoud walitangaza. judgement ya huyu itasaidia kuimodify hii kitu ya kina masoud. jamaa hafai nakubaliana na wengine.tusilembe, penye uzuri tuseme penye ubaya vilevile, ila kusema ukweli hata mimi nilipenda achukue zile pesa kwasababu ya hali yake kiuchumi.
   
 7. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #7
  May 14, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  hehehehe
  waswahili wana uswahili kweli kweli
  hata tukimlaani vipi lakini ndo ashachukua vijisenti vyake na atajua nini cha kufanyia mbeleni.
   
 8. Sonara

  Sonara JF-Expert Member

  #8
  May 14, 2009
  Joined: Oct 2, 2008
  Messages: 730
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Maisha ndivyo yalivyo mtu hujuwi nini kipo au kitatokea usoni au baada ya dakiaka chache zijazo.
   
Loading...