Abdul Nondo na ACT Wazalendo acheni kuwalaghai vijana wa Tanzania

Abdul Nondo acha kuwalaghai vijana!

Baada ya chama cha ACT Wazalendo kutangaza mchakato wa kuchukua fomu za kuomba uteuzi wa kugombea nafasi za urais, ubunge na udiwani, Abdul Nondo, kiongozi mwandamizi wa vijana wa chama hicho alitoa shime kwa vijana kuchukua fomu kwa wingi kuwania uteuzi ndani ya chama cha ACT Wazalendo. Licha ya kutoa shime ya kuchukua fomu alienda mbali zaidi na kuwaambia vijana kuwa ‘tutawapigania kamati kuu katika kuthibitisha uteuzi wa wagombea.’ Huu ni ulaghai!

Vijana wa kitanzania nawaasa, tena nina wahusia kuwa na tahadhari kubwa linapokuja swala la ushiriki wenu katika vyama vya siasa, lazima mshiriki katika vyama vya siasa mkiwa na akili ya akiba. Msishiriki katika vyama vya siasa mkiamini huko ndiko kwenye ‘destiny’ yenu. Mtashangazwa, mntatumika kama tishu ya kuchambia, mwenye haja anafahamu umuhimu tishu kabla ya haja zake, akishamaliza haja zake, akishamaliza kunya huyo anaitupilia kwenye shimo la choo, hataki hata kuiona. Vijana kataeni kuwa ‘toilet paper.’

ACT Wazalendo haina haja ya vijana, haiwataki tena, imeshawatumia na kuifikisha hapa ilipo, sasa ACT Wazalendo inahitaji watu wazima, wenye fedha zao na majina makubwa kama akina Bwege, Ally Saleh na wabunge wale katika kundi la wabunge 21 waliotoka CUF, vijana nawaambia hamna chenu ACT! Tena akija yule ‘jasusi’ na kundi lake ndio mtapotezwa kabisaa! Kuna kijana gani kati yenu ambaye jina lake litapitishwa eti waheshimiwa waachwe? Wana fedha, wana kiinua mgongo hawa, wana majina ya kuheshimiwa na media, wewe mwenzangu na mimi utapitishwa kwa lipi? Kwa kujenga hoja? Kwa kuwa na maono? Thubutu!

Wakati vijana wakipambana na dola katika kampeni ya shusha tanga pandisha tanga, waheshimiwa wateule wenyewe waliufyta, kimya, kimya kabisaa. Wakaweka kiapo cha utii kwa mwenyekiti wao Lipumba, wasingetii waone cha moto, kiinua mgongo kingekwenda. Wale waliokaidi usaliti wamekiona cha moto, walitimuliwa na sasa hivi katika ACT Wazalendo wao si chochote, si lolotemashujaa tena, mashujaa hawa waliokuja na kitu, wamepokelewa kwa heshima na mwenyekiti. Siasa ni watu na watu wenyewe ndio kama hawa si ninyi vijana.

Kama yupo mtia nia katika jimbo ‘lake’ bwege basi ajifahamu kuwa kamwe, abadani asilani hawezi kupitishwa kuwa mgombea kuiwakilisha ACT Wazalendo. Vivyo hivyo kule upande wa pili visiwani. Licha ya malalamiko mengi ya wananchi wa eneo la mji mkongwe kuwa mbunge Ally Saleh hajafanya lolote kwa ajili yao, lakini mapokezi yake katika chama cha ACT Wazalendo yanaashiria Ally Saleh Albeto pamoja na mapungufu yake lukuki, ACT Wazalendo itamsimamisha Ally Saleh bila kujali vijana watia nia wana vipawa gani. Kama wapo, na wanabisha, japo siwashauri, waionje sumu kwa kulamba!

Vijana, nawasihi sana, tena sana, hasa vijana wenye taaluma zenu na shughuli zenu, kuweni makini na vyama vya siasa vitawahribia maisha. Maneno ya akina Abdul Nondo yasiwashawishi mkajiingiza kwenye moto. Kutia nia peke yake katika vyama vya siasa na kuingia kwenye vita. Huyo Abdul Nodno mwenyewe kavutwa ACT Wazalendo baada ya kuonekana ni tishio kwa jimbo la mtu kule Kigoma. Ukafufuliwa undugu ili kijana aweze kufugwa. Pasi shaka, amefugwa akafugika. Pamoja na kutoa wito vijana wachukue fomu yeye hajachukua. Anasubiri nini? Anasubiri kwanza ajue ‘baba wa ubatizo’ anagombea urais au anarudi Kigoma urais akimuachia Membe.

Endapo baba yake wa ubatizo akimuachia urais Membe, Abdul Nondo atakuwa katika mtihani mkubwa yeye mwenyewe agombee jimbo gani. Vijana, ukimuona punda juu ya mti jua huyo kapandishwa! Abdul Nondo na wenzake wengine wamepandishwa hapo walipo, je wewe mwenzangu na mimi pangu pakavu tia mchuzi unaye mtu wa kukupandisha? Vijana tuwe makini, vyama vina wenyewe hivi, la sivyo mtaishia kuwa karatasi ya kuchambia mpaka uzee utawakutia chooni mkiwachamba watu mavi.
Hatari...
 
Back
Top Bottom