Abdul Nondo na ACT Wazalendo acheni kuwalaghai vijana wa Tanzania

domokaya

JF-Expert Member
Apr 22, 2010
3,473
2,000
Abdul Nondo acha kuwalaghai vijana!

Baada ya chama cha ACT Wazalendo kutangaza mchakato wa kuchukua fomu za kuomba uteuzi wa kugombea nafasi za urais, ubunge na udiwani, Abdul Nondo, kiongozi mwandamizi wa vijana wa chama hicho alitoa shime kwa vijana kuchukua fomu kwa wingi kuwania uteuzi ndani ya chama cha ACT Wazalendo. Licha ya kutoa shime ya kuchukua fomu alienda mbali zaidi na kuwaambia vijana kuwa ‘tutawapigania kamati kuu katika kuthibitisha uteuzi wa wagombea.’ Huu ni ulaghai!

Vijana wa kitanzania nawaasa, tena nina wahusia kuwa na tahadhari kubwa linapokuja swala la ushiriki wenu katika vyama vya siasa, lazima mshiriki katika vyama vya siasa mkiwa na akili ya akiba. Msishiriki katika vyama vya siasa mkiamini huko ndiko kwenye ‘destiny’ yenu. Mtashangazwa, mntatumika kama tishu ya kuchambia, mwenye haja anafahamu umuhimu tishu kabla ya haja zake, akishamaliza haja zake, akishamaliza kunya huyo anaitupilia kwenye shimo la choo, hataki hata kuiona. Vijana kataeni kuwa ‘toilet paper.’

ACT Wazalendo haina haja ya vijana, haiwataki tena, imeshawatumia na kuifikisha hapa ilipo, sasa ACT Wazalendo inahitaji watu wazima, wenye fedha zao na majina makubwa kama akina Bwege, Ally Saleh na wabunge wale katika kundi la wabunge 21 waliotoka CUF, vijana nawaambia hamna chenu ACT! Tena akija yule ‘jasusi’ na kundi lake ndio mtapotezwa kabisaa! Kuna kijana gani kati yenu ambaye jina lake litapitishwa eti waheshimiwa waachwe? Wana fedha, wana kiinua mgongo hawa, wana majina ya kuheshimiwa na media, wewe mwenzangu na mimi utapitishwa kwa lipi? Kwa kujenga hoja? Kwa kuwa na maono? Thubutu!

Wakati vijana wakipambana na dola katika kampeni ya shusha tanga pandisha tanga, waheshimiwa wateule wenyewe waliufyta, kimya, kimya kabisaa. Wakaweka kiapo cha utii kwa mwenyekiti wao Lipumba, wasingetii waone cha moto, kiinua mgongo kingekwenda. Wale waliokaidi usaliti wamekiona cha moto, walitimuliwa na sasa hivi katika ACT Wazalendo wao si chochote, si lolotemashujaa tena, mashujaa hawa waliokuja na kitu, wamepokelewa kwa heshima na mwenyekiti. Siasa ni watu na watu wenyewe ndio kama hawa si ninyi vijana.

Kama yupo mtia nia katika jimbo ‘lake’ bwege basi ajifahamu kuwa kamwe, abadani asilani hawezi kupitishwa kuwa mgombea kuiwakilisha ACT Wazalendo. Vivyo hivyo kule upande wa pili visiwani. Licha ya malalamiko mengi ya wananchi wa eneo la mji mkongwe kuwa mbunge Ally Saleh hajafanya lolote kwa ajili yao, lakini mapokezi yake katika chama cha ACT Wazalendo yanaashiria Ally Saleh Albeto pamoja na mapungufu yake lukuki, ACT Wazalendo itamsimamisha Ally Saleh bila kujali vijana watia nia wana vipawa gani. Kama wapo, na wanabisha, japo siwashauri, waionje sumu kwa kulamba!

Vijana, nawasihi sana, tena sana, hasa vijana wenye taaluma zenu na shughuli zenu, kuweni makini na vyama vya siasa vitawahribia maisha. Maneno ya akina Abdul Nondo yasiwashawishi mkajiingiza kwenye moto. Kutia nia peke yake katika vyama vya siasa na kuingia kwenye vita. Huyo Abdul Nodno mwenyewe kavutwa ACT Wazalendo baada ya kuonekana ni tishio kwa jimbo la mtu kule Kigoma. Ukafufuliwa undugu ili kijana aweze kufugwa. Pasi shaka, amefugwa akafugika. Pamoja na kutoa wito vijana wachukue fomu yeye hajachukua. Anasubiri nini? Anasubiri kwanza ajue ‘baba wa ubatizo’ anagombea urais au anarudi Kigoma urais akimuachia Membe.

Endapo baba yake wa ubatizo akimuachia urais Membe, Abdul Nondo atakuwa katika mtihani mkubwa yeye mwenyewe agombee jimbo gani. Vijana, ukimuona punda juu ya mti jua huyo kapandishwa! Abdul Nondo na wenzake wengine wamepandishwa hapo walipo, je wewe mwenzangu na mimi pangu pakavu tia mchuzi unaye mtu wa kukupandisha? Vijana tuwe makini, vyama vina wenyewe hivi, la sivyo mtaishia kuwa karatasi ya kuchambia mpaka uzee utawakutia chooni mkiwachamba watu mavi.
 
Retired

JF-Expert Member
Jul 22, 2016
25,709
2,000
kujali vijana watia nia wana vipawa gani
Vipawa vipi? Someni science mvumbue vitu, siyo kutegemewa vipawa vya siasa! Kila mtu anataka siasa za ubunge, this is rubbish! Pader anataka siasa, Gwajima siasa, Lwakatale siasa, Pope siasa, Sheikh siasa, mama ntilie siasa, RC siasa, DC siasa, DED siasa, wanafunzi siasa, mkulina siasa. This is shit!
 
kantasundwa

JF-Expert Member
May 25, 2020
1,559
2,000
Hao wabunge 21 ndo wamekutisha ?? Majimbo yako mangapi nchi nzima? Acha watu wagombee maana ni haki yao kikatiba, hv ninyi lumumba mnashida gn kwenye vichwa vyenu?
 
Mkaruka

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
13,471
2,000
Nenda SAU au APPT Maendeleo kule hawana wagombea.

Tatizo hakuna anayetaka kuanzia sifuri, kila takataka inachungulia wapi kuna Kitonga ndio inajichomeka.

Kila pimbi anajichomeka CCM, CHADEMA au ACT kwa kuwa wanaona mwanga.

Unafiki
 
Savimbi Jr

JF-Expert Member
Sep 23, 2011
6,742
2,000
Mtaji wa vyama vya siasa ni watu, sasa kama anakuja mtu mwenye mtaji wa watu unataka wamuache?
 
Bishweko

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
2,601
2,000
Mada mzuri sema umeishia kati...ungetoa suluhu kua vijana wafanye nini sasa? Kumbuka Siasa za Afrika ni Biashara kama ilivyo biashara ya viroba,bangi nk
 
Lyaka Mlima Jr

JF-Expert Member
Mar 24, 2020
295
500
Abdul Nondo Acha kuwalaghai vijana!

Baada ya chama cha ACT Wazalendo kutangaza mchakato wa kuchukua fomu za kuomba uteuzi wa kugombea nafasi za urais, ubunge na udiwani, Abdul Nondo, kiongozi mwandamizi wa vijana wa chama hicho alitoa shime kwa vijana kuchukua fomu kwa wingi kuwania uteuzi ndani ya chama cha ACT Wazalendo. Licha ya kutoa shime ya kuchukua fomu alienda mbali zaidi na kuwaambia vijana kuwa ‘tutawapigania kamati kuu katika kuthibitisha uteuzi wa wagombea.’ Huu ni ulaghai!

Vijana wa kitanzania nawaasa, tena nina wahusia kuwa na tahadhari kubwa linapokuja swala la ushiriki wenu katika vyama vya siasa, lazima mshiriki katika vyama vya siasa mkiwa na akili ya akiba. Msishiriki katika vyama vya siasa mkiamini huko ndiko kwenye ‘destiny’ yenu. Mtashangazwa, mntatumika kama tishu ya kuchambia, mwenye haja anafahamu umuhimu tishu kabla ya haja zake, akishamaliza haja zake, akishamaliza kunya huyo anaitupilia kwenye shimo la choo, hataki hata kuiona. Vijana kataeni kuwa ‘toilet paper.’

ACT Wazalendo haina haja ya vijana, haiwataki tena, imeshawatumia na kuifikisha hapa ilipo, sasa ACT Wazalendo inahitaji watu wazima, wenye fedha zao na majina makubwa kama akina Bwege, Ally Saleh na wabunge wale katika kundi la wabunge 21 waliotoka CUF, vijana nawaambia hamna chenu ACT! Tena akija yule ‘jasusi’ na kundi lake ndio mtapotezwa kabisaa! Kuna kijana gani kati yenu ambaye jina lake litapitishwa eti waheshimiwa waachwe? Wana fedha, wana kiinua mgongo hawa, wana majina ya kuheshimiwa na media, wewe mwenzangu na mimi utapitishwa kwa lipi? Kwa kujenga hoja? Kwa kuwa na maono? Thubutu!

Wakati vijana wakipambana na dola katika kampeni ya shusha tanga pandisha tanga, waheshimiwa wateule wenyewe waliufyta, kimya, kimya kabisaa. Wakaweka kiapo cha utii kwa mwenyekiti wao Lipumba, wasingetii waone cha moto, kiinua mgongo kingekwenda. Wale waliokaidi usaliti wamekiona cha moto, walitimuliwa na sasa hivi katika ACT Wazalendo wao si chochote, si lolotemashujaa tena, mashujaa hawa waliokuja na kitu, wamepokelewa kwa heshima na mwenyekiti. Siasa ni watu na watu wenyewe ndio kama hawa si ninyi vijana.

Kama yupo mtia nia katika jimbo ‘lake’ bwege basi ajifahamu kuwa kamwe, abadani asilani hawezi kupitishwa kuwa mgombea kuiwakilisha ACT Wazalendo. Vivyo hivyo kule upande wa pili visiwani. Licha ya malalamiko mengi ya wananchi wa eneo la mji mkongwe kuwa mbunge Ally Saleh hajafanya lolote kwa ajili yao, lakini mapokezi yake katika chama cha ACT Wazalendo yanaashiria Ally Saleh Albeto pamoja na mapungufu yake lukuki, ACT Wazalendo itamsimamisha Ally Saleh bila kujali vijana watia nia wana vipawa gani. Kama wapo, na wanabisha, japo siwashauri, waionje sumu kwa kulamba!

Vijana, nawasihi sana, tena sana, hasa vijana wenye taaluma zenu na shughuli zenu, kuweni makini na vyama vya siasa vitawahribia maisha. Maneno ya akina Abdul Nondo yasiwashawishi mkajiingiza kwenye moto. Kutia nia peke yake katika vyama vya siasa na kuingia kwenye vita. Huyo Abdul Nodno mwenyewe kavutwa ACT Wazalendo baada ya kuonekana ni tishio kwa jimbo la mtu kule Kigoma. Ukafufuliwa undugu ili kijana aweze kufugwa. Pasi shaka, amefugwa akafugika. Pamoja na kutoa wito vijana wachukue fomu yeye hajachukua. Anasubiri nini? Anasubiri kwanza ajue ‘baba wa ubatizo’ anagombea urais au anarudi Kigoma urais akimuachia Membe.

Endapo baba yake wa ubatizo akimuachia urais Membe, Abdul Nondo atakuwa katika mtihani mkubwa yeye mwenyewe agombee jimbo gani. Vijana, ukimuona punda juu ya mti jua huyo kapandishwa! Abdul Nondo na wenzake wengine wamepandishwa hapo walipo, je wewe mwenzangu na mimi pangu pakavu tia mchuzi unaye mtu wa kukupandisha? Vijana tuwe makini, vyama vina wenyewe hivi, la sivyo mtaishia kuwa karatasi ya kuchambia mpaka uzee utawakutia chooni mkiwachamba watu mavi.
Sisiemu vipi kwani??
 
tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
35,655

Hoja yako ni nini hapa we dogo? Chama Chenu kilichokuwa kinampaka rais mafuta kwa mgongo wa chupa, kuwa kaidhibiti rushwa, ndio hicho kinagawa rushwa kama vichaa huko mtaani. Huo ushauri wako ni vyema mngekaa na chama chako, muoene hiyo rushwa mnayovika Magufuli kilemba cha ukoka kuwa kaimaliza ni ipi?
 
Bavaria

JF-Expert Member
Jun 14, 2011
48,627
2,000
Kuna majimbo mangapi ya kugombania ubunge?

Kuna kata ngapi za vijana kutafuta udiwani?

Bado ACT hawana man power ya kutosha kujaza hizi nafasi.

Hata Chadema nayo haikuwa na watu wa kutosha ndio maana kulikuwa na vijana kama wakina Lijualikali wakapewa nafasi wakashinda bila kufanyiwa vetting ya kutosha.

Hata aje Membe na timu ya CCM, kujaza nafasi zote za Ubunge na Udiwani ni ndoto. Kuna sehemu hawataweza kusimamisha mgombe kabisa.
 
Cvez

JF-Expert Member
May 19, 2018
1,125
2,000
ACT bado ni changa sana katika siasa ndio kuna watu wakubwa waliohamia na wanaotarajia kuhamia. Ila kutokana na uchanga wake kila mtu ana nafasi ya kuingia si kama ilivyo ndani ya CCM au CDM.
 
komamgo

JF-Expert Member
Sep 14, 2012
2,103
2,000
Vipawa vipi? Someni science mvumbue vitu, siyo kutegemewa vipawa vya siasa! Kila mtu anataka siasa za ubunge, this is rubbish! Pader anataka siasa, Gwajima siasa, Lwakatale siasa, Pope siasa, Sheikh siasa, mama ntilie siasa, RC siasa, DC siasa, DED siasa, wanafunzi siasa, mkulina siasa. This is shit!
Uko sahihi
 
mbu wa dengue

JF-Expert Member
Jun 2, 2014
5,159
2,000
Nenda SAU au APPT Maendeleo kule hawana wagombea.

Tatizo hakuna anayetaka kuanzia sifuri, kila takataka inachungulia wapi kuna Kitonga ndio inajichomeka.

Kila pimbi anajichomeka CCM, CHADEMA au ACT kwa kuwa wanaona mwanga.

Unafiki
Naona siku hizi wameanza kuikimbia CUF kwa vile imeanza kupoteza umaarufu sasa hii ni siasa au unafki tu
 
vposterior

JF-Expert Member
Jul 19, 2018
787
1,000
Hao wazee walianza siasa katika ujana wao wakajenga majina yao na kazi yao inaonekana. Vijana wawe na uthubutu kujifunza zaidi na kugombea ili kutafuta uzoefu kama hawatapata mwaka huu watapata mwaka mwengine. Kijana wa leo ndio mzee wa kesho.
 
domokaya

JF-Expert Member
Apr 22, 2010
3,473
2,000
Sisiemu vipi kwani??
Hao wote wanakimbilia majimbo angalau yaliyowahi kupigia kura wapinzani. Hawaendi kwenye majimbo mengine na hawajiungi na TADEA ambao hawana vijana, hawana wagombea, wanakwenda katika vyama ambavyo vijana wamefanya kazi kubwa tayari
 
domokaya

JF-Expert Member
Apr 22, 2010
3,473
2,000
Hao wazee walianza siasa katika ujana wao wakajenga majina yao na kazi yao inaonekana. Vijana wawe na uthubutu kujifunza zaidi na kugombea ili kutafuta uzoefu kama hawatapata mwaka huu watapata mwaka mwengine. Kijana wa leo ndio mzee wa kesho.

Wengine wala hawakuwa katika harakati. Walikuwa katika Nazi zao ambazo zimewapa umaarufu, kama vile uandishi wa habari, Mara hao, kwa kutumia umaarufu wait, na chama kuona ni rahisi kuuzika basi wanawatosa vijana kwenye imani ya dhati na itikadi husika na wengi wa vyama vya huwa ndio itakadi yao ya kwanza maishani
 
domokaya

JF-Expert Member
Apr 22, 2010
3,473
2,000
ACT bado ni changa sana katika siasa ndio kuna watu wakubwa waliohamia na wanaotarajia kuhamia. Ila kutokana na uchanga wake kila mtu ana nafasi ya kuingia si kama ilivyo ndani ya CCM au CDM.

Kweli ACT kuna fursa, lakini katika maeneo ambayo ACT imejijenga, na vijana wake wametoka nayo mbali, yanaelekea kukabidhiwa kwa wahamiaji wenye majina na wajenzi wa chama, vijana, wakaachwa patupu. CCM wenzao walau wanaweza kuwakuza kwa kuwapa nafasi mbalimbali katika ngazi za chini na kati za uongozi.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom