Abdul Kambaya: Mtazamo na ushauri binafsi kwa vyama vya siasa Tanzania kuhusu uchaguzi mkuu Oktoba na gonjwa la Corona/covid-19 nchini

CUF Habari

JF-Expert Member
Dec 12, 2019
239
234
Screenshot_20200406-150825.png



COVID-19 NA UCHAGUZI

Tunafikirishwa na

Abdul Kambaya

Mtazamo na Ushauri Binafsi Kwa Vyama vya Siasa Tanzania Kuhusu Uchaguzi na COVID -19 .

Nimefuatilia Maelezo na hatua mbalimbali Kuhusu janga hili la Corona linavyotishia sio tu uhai wa Wananchi Duniani bali hata Uchumi wa Nchi zetu Kwa ujumla wake .

Nimefuatilia maelezo ya awali ya Profesa Lipumba Kuhusu Corona ikiwa ni Mwenyekiti wa kwanza wa Chama Cha Siasa kuonyesha kushitushwa na Gonjwa hili kisha kufuatiwa na Kiongozi Mkuu wa Chama Cha ACT na baadae pia nikaona maelezo ya Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo -Chadema.

Kisha Mwenyekiti wa ACT Wazalendo nae akapaza sauti na kuonyesha jinsi Gonjwa hili lilivyokua tishio Kwa Nchi yetu.

Jana Tarehe 05-04-2020 Profeaa Lipumba ameibuka tena kuliangazia Gonjwa hilo na athari zake kiuchumi kupitia Hotuba ya Waziri Mkuu aliotoa Bungeni.

Kimsingi maelezo ya Viongozi wote hawa yanaonyesha wasiwasi mkubwa mno aidha wa uwezo wetu mdogo katika kulikabili janga hili kitaalamu au kutokana na mazingira halisi ya Nchi zetu za Afrika sio tu Tanzania.

Lakini kila mmoja miongoni mwa Vyama tajwa hapo juu vina himiza Wananchi kufuata maelekezo ya Wataalamu katika jitihada za kupunguza kama si kuzuia kabisa maambukizi ya Virusi hivi vya COVID - 19 ambavyo vinasababisha maradhi ya homa ya mapafu ambayo inajulikana kwa jina la Corona.

1 . Kimsingi sote tunakubaliana kuwa hili ni Gonjwa hatari ambalo linaambukiza Kwa kasi kubwa kupitia mikusanyiko , Misingamano ya watu na athari zake kwenye mwili wa Binadamu zinajitokeza haraka mno na madhara yake si maamivu ya kimwili tu Bali ni kupoteza maisha Kwa muathirika wa Virus hivyo.

2 . Katika hali kama hii inaonyesha zaidi Kwa Inchi kama yetu inayotegemea Utalii Kwa kiwango kikubwa ili kiwezesha Bajeti zetu , na Kwa Inchi ambayo pia Baheti yake pia inategemea zaidi misada toka Kwa Wafadhili ni wazi kwamba patakuwa na tatuzo la Kiuchumi Kwa namna moja au nyingine katika kukamilisha mambo kadhaa ya Kibajeti Kwa Mwaka wa Fedha 2020/2021.

Wasiwasi ambao Profesa Lipumba ameueleza Jana wakati anachambua hotuba ya Waziri Mkuu sio tu utaathiri bajeti za Miradi au shughuli za kimaendeleo na hasa ukizingatia athari za Gonjwa hili zinaonyesha zimeikumba hata Bandari yetu ya Dar es Salaam ambapo inaonyesha kwamba uingiaji wa Meli za Mizigo Kwa kipindi hiki tangu kuibuka Kwa Gonjwa hili umekuwa wa Kiwango cha chini sana maana juzi nilikuwa pale TRA nasikia watumishi wakiambiana Corona kiboko Kwa kweli ya tuna meli za Mizigo 7 tu ndio zimeegesha kusubiri kushusha.

3 Kitendo Cha Serikali kuchukua hatua za kusitisha Masomo hapa Nchini na Mikusanyiko ya Kimichezo na hata Sherehe mbalimbali japo hatujafikia kuzuia watu wetu wasitoke ndani ya Majumba yao na kwenda kutafuta kipato Kwa ajili ya familia zao , kinaonyesha namna Gonjwa hili lilivyokuwa tisho.

Baada ya kuyaangalia hayo niliorodhesha hapo juu sasa naomba kutoa ushauri Binafsi.

Ushauri wangu Kwa Wadau wa Uchaguzi nikianza na Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ambalo limeundwa na Vyama ambavyo Viongozi wake sio tu wameshiriki kuona athari za Gonjwa hili Bali pia kutoa ushauei Kwa Serikali namna ya kudhibiti Gonjwa hili , kuangalia suala la Uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Mwezi October Kwa kuzingatia hali tuluonayo kama Taifa kwenye Gonjwa hili lakini pia uwezo wetu kitaalamu na Kiuchumi wa kukabiliana nalo pale litaposhika kasi kutoka Wagonjwa 17 tuliobaki nao na kuongezeka Kwa kasi kupitia Mikusanyiko ya Kiuchaguzi Kwa maana ya Mikutano ya Hadhara , Vikao vya Ndani na Kampeni mbalimbali kuelekea siku ya Kupiga Kura na siku ya Upigaji Kura yenyewe.

Pamoja na dhamira yangu ya Kugombea Ubunge itapofika Mwezi October 2020 lakini nawaomba wadau wafuao Bunge , Vyama vya Siasa, Tume ya Uchaguzi, Msajili wa Vyama na Wadau mbalimbali ikiwemo sina hakika Wizara ya Afya au Chama Cha Madaktari Tanzania na Serikali Kwa ujumla kufanya tathimini ya kina kuhusu Taarifa za sahihi za Gonjwa hili na kuona au kufikia maamuzi je kuna haja ya kuendelea na Uchaguzi Mwezi October ?

Binafsi nashauri , kama hali hii iliozungumzwa na Viongozi wa Vyama Vyetu na Wabunge pale Bungeni na Serikali yetu pia ndio taarifa sahihi , basi nashauri Uchaguzi usogezwe mbele Kwa Miezi sita zaidi ili kuangalia au kulinda Maisha ya Watanzania .

Bunge liweke utaratibu Maalum wa kipindi cha Mpito na nina hakika Katiba ya Jamuhuri ya Muungano itakuwa inajieleza vizuri kutokana na dharura hiyo.

Ni Mawazo Binafsi tu yasihusishwa na Chama Changu bali yahusishwe na Utanzania wangu Kwa ndugu zangu.

Abdul Kambaya

Mwananchi wa Kawaida na Mtanzania
 
Muda wa kusema uchaguzi uharishwe bado sana ,lolote linaweza kutokea hivyo ni vyema tunajiandaa na uchaguzi kwa kiwango kinachohitajika.
 
..ccm wasije wakasema wanataka miaka 7.

..tatizo ni wana ccm ndani ya bunge.
 
Ndugu Kambaya ana hoja za msingi, cha maana ni maisha ya Watanzania endapo gonjwa hili la maambukizi likishindikana kuthibitiwa. Mimi naona itakuwa vyema kama ifikapo kikao cha mwisho cha mkutano wa bunge hili la bajeti linaloendea, na ikiwa bado kuna tishio zaidi itapasa serikali iahirishe zoezi zima la uchaguzi.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi Mwenyekiti wa Taifa wa KAFU ni nani?? Ni yule aliejihudhuru mwenyewe na baadae akarudi kwa amri ya Mahakama. Je safari hii tena hiki chama mnataka kuwa sehemu ya ushindi wa Kishindo??. Hivi bado watu wana Imani Nanyi tena au "used' Uchanguzi umefika ni wakati wa Mavuno Kwenu........ KAFU bila Maalim Seif hakuna kitu....
 
Kambaya sikutegemea utoe maoni tofauti na haya, na hujayatoa kwa bahati bali ni maelekezo maalum. Wenye hiyo ajenda wanaona soni kuitoa wakwanza, hivyo ww na chama chako mnatumika maana Lipumba alipokutana na Magufuli mlipewa ahadi fulani. Kwa maneno marahisi huu ushauri wako sio maoni yako binafsi, bali ni ajenda maalumu kwa malipo fulani iwapo mtafanikiwa kwenye ushawishi huu.

Sisi wapinzani wengine tunataka tume huru ya uchaguzi, maana tunaona wazi uchaguzi ukinajisiwa, na hakuna maneno yoyote ya kudanya eti rais kasema uchaguzi utakuwa huru, kwani yeye ndio mnajisi uchaguzi namba moja ndani ya nchi hii. Ila kwakuwa nyie CUF mmeahidiwa viti kadhaa ya ubunge, hivyo mnakalia kimya hiyo hali kwa manufaa binafsi. Hakuna tume huru, wala katiba mpya, mbona hamtaki hivyo vipatikane kwanza kabla ya uchaguzi, lakini mnaona huo ugonjwa ndio wa kusogezea uchaguzi mbele? Ni kweli huo ugonjwa ni hatari, lakini ni hali ya kupita, ila tume huru na katiba mpya sio tukio la kupita, bali linahitaji utekelezaji, na sio wakati mwingine bali sasa.
 
"MaCuf" katika ubora wao😂😂
Kwa kifupi bro wewe na chama chako mshaupoteza uhalali wa hata kusikilizwa kwa kile mnachokiongea yani!
Lipumba akinyanyua tu limdomo lake, watu tunaanza kuulizana "hili lijamaa linataka kuchangia nini nalo"🙉🙉
 
ongelea Tume huru Mzee - kwani kwa sasa si option tena ni lazima.... maandalizi ya muswaada wa sheria yanatakiwa yawe yameshaanza sasa hivi ili kabla bunge halijavunjwa sheria ya kuundwaji wa Tume huru yapitishwe....hata kama ni kwa hati ya dharura.......
 
Back
Top Bottom