Abdu Kiba: Nipo tayari kufanya kazi na Wasafi WCB

mr gentleman

JF-Expert Member
Aug 1, 2012
3,223
4,681
Abdul Kiba amesema yupo tayari kujiunga na lebo ya WCB inayomilikiwa na Diamond kama hela itawekwa mezani.
Bifu la Alikiba na Diamond linaonekana kuathiri mpaka mfumo wa watu wa pembeni wanaowazunguka wasanii hao japo kila mmoja anakubali kuwa hana tatizo na mwenzake huku ukweli wa kila mmoja ukibaki moyoni mwake.

Akiongea kwenye kipindi cha Planet Bongo, kinachoruka kupitia EA Radio, Abdu Kiba alisema kuwa kama watakuwa na pesa za kutosha na makubaliano mazuri anaweza kufanya kazi chini la Label hiyo [WCB].

“Nipo tayari naangalia pesa, kama pesa zitakuwepo na wakihitaji kufanya kazi na mimi naweza nikafanya kazi chini ya lebo hiyo,” aliongeza.

Siku chache zilizopita Abdu Kiba ameachia video ya wimbo wake mpya ‘Bayoyo’.
 
Nisaidie jamaa Ana wimbo gani kwani? Maana wengine miziki imepita mbali
 
Eti "kama hela itawekwa mezani" !!!!!!!!!!!!!!! Kwa kipi anachoimba hadi iwekwe pesa mezani ????? ( hamsubirie braza si anaanzisha lebo siku si nyingi.)
 
Shida anayoipata huyu mtu, ni mashabiki wa Wema hawataki kumpa support (kwakuwa labda hayupo kwenye kushindanishwa na Diamond) ndio maana badala ya kwenda kuangalia video YouTube, wamekazana kumpigia kura Wizkid...
 
Abdul Kiba amesema yupo tayari kujiunga na lebo ya WCB inayomilikiwa na Diamond kama hela itawekwa mezani.

Bifu la Alikiba na Diamond linaonekana kuathiri mpaka mfumo wa watu wa pembeni wanaowazunguka wasanii hao japo kila mmoja anakubali kuwa hana tatizo na mwenzake huku ukweli wa kila mmoja ukibaki moyoni mwake.

Akiongea kwenye kipindi cha Planet Bongo, kinachoruka kupitia EA Radio, Abdu Kiba alisema kuwa kama watakuwa na pesa za kutosha na makubaliano mazuri anaweza kufanya kazi chini la Label hiyo [WCB].

“Nipo tayari naangalia pesa, kama pesa zitakuwepo na wakihitaji kufanya kazi na mimi naweza nikafanya kazi chini ya lebo hiyo,” aliongeza.

Siku chache zilizopita Abdu Kiba ameachia video ya wimbo wake mpya ‘Bayoyo’.
HUYO BOYA LABDA APIGE MAZOEZI YA KUTOSHA NA KUNYANYUA VYUMA AWE MLINZI WA WASAFI..HANA HADHI HATA CHEMBE YA KUIMBA PALE..
 
dah! Watu wana roho mbaya , mngekuwa mabosi wa wasafi sijui inegekuwaje?
Jigo
 
Back
Top Bottom